Hivi meno ya tembo ni malighafi ya nini?

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,303
2,000
Naomba mnijuze hayo meno ya tembo yanatumika kama malighafi ya kutengeneza nini? Au yana kazi gani?
Wanapokamata hizo wanazoziita nyara hawaziharibu au huziharibu kwa kificho?
Kama hawazihatibu huzipeleka wapi?
 
Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
718
500
Hello Mkuu, meno ya tembo huwa yanatumika kutengenezea mapambo kama vile vidani, pete, heleni na vitu vingine vya kuvaa kwenye miili ya binadamu. Vilevile, hutumika kutengenezea sanamu za viongozi au watu mashuhuri wenye michango mikubwa katika maendeleo ya nchi. Katika nchi za mashariki ya mbali, bidhaa hizo hununuliwa kwa bei kubwa na wanao nunua ni watu wenye ufahari kama vile wafalme, ma rais na watu wengine kama hao. Kumiliki bidhaa zilizotengenezwa kutokana na malighafi ya meno ya tembo ni jambo la ufahali kwa mataifa hayo na mtu anayemiliki malighafi hizo huthaminiwa katika jamii. Kwa hiyo ni utamaduni tu uliojengeka katika jamii hizo kumiliki bidhaa zilizotengenezwa na malighafi ya meno ya tembo kuwa ni wa kifahali.
 
paparazzi

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
572
195

Mengi yamefichika hapa....

Kwanza tuanze na hili,
Kwanini meno ya tembo tu na wala si ya fisi ama kenge...
 
Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
718
500
Mengi yamefichika hapa....

Kwanza tuanze na hili,
Kwanini meno ya tembo tu na wala si ya fisi ama kenge...

Nafikiri wanatumia meno ya tembo kwa kiasi kikubwa kwa sababu tembo anasifa ya kipekee ya kuwa mnyama mkubwa kuliko wote katika nchikavu. Malighafi inayopatikana kutoka kwa tembo inaubora wa hali ya juu na uadimu wake unazifanya ziwe za thamani!

Wangetumia hata pembe za ng'ombe kwani zinapatikana kirahisi na zote zinatokana na keratini katika miili ya wanyama sawa na tembo
 
Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
718
500
Naomba mnijuze hayo meno ya tembo yanatumika kama malighafi ya kutengeneza nini? Au yana kazi gani?
Wanapokamata hizo wanazoziita nyara hawaziharibu au huziharibu kwa kificho?
Kama hawazihatibu huzipeleka wapi?

Baada ya kesi kumalizika meno yote hupelekwa 'Ivory Room' na baadaye huchomwa moto! Umoja wa mataifa walipiga marufuku serikali za dunia kuyauza meno hayo kwani inaweza kusaidia kuenea kwa ujangili wa tembo!
 
double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,303
2,000
Asanteni kwa mwanga kidogo. Hii biashara inaonekana ni ya thamani kuliko dhahabu.
 
Jim007 2

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
395
250
Mkuu biashara kuu c kutengenezea product za urembo.....pembe hizo ni dawa nzuri sana kuongeza nguvu za kiume nadhani unajua jinsi gn watu walivyo desperate kupata hizo dawa
 
Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
718
500
Mkuu biashara kuu c kutengenezea product za urembo.....pembe hizo ni dawa nzuri sana kuongeza nguvu za kiume nadhani unajua jinsi gn watu walivyo desperate kupata hizo dawa

Pembe ya Faru ndiyo hutumika kutengenezea dawa za kuongeza nguvu za kiume. Haya meno ya tembo ni mapambo tu na nakshi za mapambo. Najua huwezi amini, lakini watu wamefanya utafiti na wameingia hadi kwenye hivyo viwanda vya kutengenezea hayo mapambo na wakawahoji wahusika kama kuna cha ziada kinachotokana na meno ya tembo wakakiri wenyewe hakuna.
 
Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
718
500
Asanteni kwa mwanga kidogo. Hii biashara inaonekana ni ya thamani kuliko dhahabu.

Biashara zote za magendo kama meno ya tembo, unga and the like, zinalipa kuliko biashara zingine zozote. Ndiyo maana unakuta watu wenye nyadhifa za juu nchini ni ma dealer wakubwa!
 
Jim007 2

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
395
250
Pembe ya Faru ndiyo hutumika kutengenezea dawa za kuongeza nguvu za kiume. Haya meno ya tembo ni mapambo tu na nakshi za mapambo. Najua huwezi amini, lakini watu wamefanya utafiti na wameingia hadi kwenye hivyo viwanda vya kutengenezea hayo mapambo na wakawahoji wahusika kama kuna cha ziada kinachotokana na meno ya tembo wakakiri wenyewe hakuna.

Mkuu siwezi kukupinga maana source ya data zangu ni kijiweni!!sina data za uhakika kuhusu nililozungumza
 
kidonto

JF-Expert Member
Jan 5, 2014
941
500
Naomba mnijuze hayo meno ya tembo yanatumika kama malighafi ya kutengeneza nini? Au yana kazi gani?
Wanapokamata hizo wanazoziita nyara hawaziharibu au huziharibu kwa kificho?
Kama hawazihatibu huzipeleka wapi?

Moja ya kazi yake ni kurudisha nguvu za kiume, nimepata oda kwenye nchi 1 kusini wanataka niwapelekee hata jino moja tu ila sijui ntayapata wapi?
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,355
2,000
Meno ya tembo hutengenezewa masanamu ya kuabudia huko China, kwani hudumu mda mrefu pia wanatengenezea pool balls, na piano, vitako vya bastola nk naona itasaidia kwa utafiti wako
 
Good Guy

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
3,780
2,000
Naomba mnijuze hayo meno ya tembo yanatumika kama malighafi ya kutengeneza nini? Au yana kazi gani?
Wanapokamata hizo wanazoziita nyara hawaziharibu au huziharibu kwa kificho?
Kama hawazihatibu huzipeleka wapi?

.

.
 
FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,366
2,000
Mengi yamefichika hapa....

Kwanza tuanze na hili,
Kwanini meno ya tembo tu na wala si ya fisi ama kenge...

Meno ya Tembo hutumika sambamba na meno ya kiboko na seal (wanyama wa baharini waliochomoza meno kwa mbele, kama Ngiri) ila wahitaji huthamini zaidi meno ya Tembo kwani yana ukubwa unaozalisha bidhaa bora na nyingi zaidi kulinganisha na hayo meno mengine......

Zaidi ya kutengeneza urembo meno ya Ndovu pia hutengeneza keyboards za piano na baadhi ya bidhaa za asili za kiasia (haswa Japan) ambazo hutumiwa na familia za kifalme na hizo hazina malighafi mbadala za kutengenezea zaidi ya meno ya Tembo.

Bidhaa karibia zote zinaweza pia kutengenezwa kwa malighafi mbadala kama plastics...lakini kwa bidhaa hizo hizo zikitokana na meno ya Tembo huuzwa kwa watu maalum (matajiri au familia za kifalme) kwa bei ya juu sana kama dhahabu na ni fahari kwa mwenye uwezo kumiliki kifaa kilichotengenezwa na meno ya Tembo kwani bidhaa zinazofanania hizo zinamilikiwa pia na wengine lakini hazina thamani hiyo.

Hata kama zitatengenezea mipira ya pool table kama mchangiaji mmoja alivyoeleza hapo juu...lakini kamwe sio hii mipira tutakayoikuta dukani...mipira hii itakuwa ni kwa ajili ya watu maalum kama matajiri, watu maarufu n.k.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom