Hivi mbona CCM wako kimya mpaka sasa?

Hivi mbona CCM wako kimya mpaka sasa?

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
12,055
Reaction score
16,509
Tangu kuanza kwa drama za watu waliokatwa na wasiotakiwa ndani ya chama kuhama na wengine kutishia kuhama chama..naona ccm wako kimya tu,ukimya wao utakua unaashiria nini?

Tokea siku ya Jumatatu pale ambapo makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba walipewa taarifa za mhshimiwa Lowasa kuhama chama na kutimkia UKAWA.

Kwa kuwa vijana wa masuala ya propaganda chini ya katibu mwenezi Nape Mnauye walidhani ulikuwa utani au masihara wakapuuzia onyo hilo sasa imekuwa ngumu kutoa taarifa ya kupokea uamuzi huo.

Katika ulimweigu wa sasa wanasiasa nao wakiwa kama binadamu wengine nao wana utashi na moja ya matunda ya utashi huo ni kuweza kufanyamaamuzi na kuyatakeleza.

Pia katika nchi mbalimbali duniani vyma vya siasa vinakuwa na washauri wao ambao moja ya kazi zao ni kujaribu kuoanisha taarifa zinazopishana kuhusu sera, itikadi na suala Zima la mbinu na mikakati.

Lakini Chama cha Mapinduzi wamekuwa kimya hata baada ya kuona kwenye mitandao kwamba Tumaini Makene, mkuu G Sam na wengine walikuwa wakifanya kazi usiku na mchana, na Nape Nnauye akawa hajajiandaa angalu kujibu uamuzi huo wa mzee Lowasa kuhama CCM.

CCM si chama lelemama na kipo kinatawala nchi hii tangia ilipokuwa TAA, TANU hadi CCM ilozaliwa tarehe 5 mwezi wa 7 mwaka 1977.

CCM mtaa wa Lumumba vipi mmekaa kimya au Nape Nnauye bado ametahayari?

CCM mtaa wa Lumumba isiwaache vijana wasofahamu siasa kuja jamii forums kujaza taarifa za kizushi kuhusu UKAWA na Dr Slaa, au mjinga mmoja anakuja na kichwa cha habari kinachosema Dr Slaa is dead!.

"Spin Doctors" wa CCM wapo wapi?
 
Tangu kuanza kwa drama za watu waliokatwa na wasiotakiwa ndani ya chama kuhama na wengine kutishia kuhama chama..naona ccm wako kimya tu,ukimya wao utakua unaashiria nini?
Hata wewe mkuu ukipigwa kofi la nguvu la usoni lazima akili zikuhame..CCM ilikuwa ina "mbipu" Lowassa na mwenzao kapiga simu …hawakutegemea kabisa kuwa Lowassa angechukua maamuzi kama haya…Huku mtaa wa Lumumba hakukaliki…makundi yanalaumiana na wanazidi kugwayana..hivi kalibuni kila mtu atachukua mbao zake….
Mimi nawaonea huruma sana akiana Ritz,fauzyfox,Lizabon Nape etc sijui wataishije mjini bila CCM
:cheer2:
 
Lowassa kashaibadilisha Chadema.

1. Kabadilisha ratiba yao ya uchaguzi.

2. Kabadilisha mgombea wao. Dr. Slaa anakatwa kwa sababu ya Lowassa.

3. Kabadilisha bajeti yao ya uchaguzi.

4. Kabadilisha kauli zao kuhusu ufisadi.

5. Kabadilisha ilani yao ya uchaguzi.

Sasa tujiulize, nani anayebadili mwenzie? Chadema itambadili Lowassa au Lowassa anaibadili Chadema?

Lowassa yuko kwenye siasa muda mrefu kuliko umri wa Chadema. Kuamini kuwa Lowassa atabadilika ghafla ni kujidanganya kulikopitiliza.

Mpaka sasa Chadema haijabadili chochote kwa Lowassa, yeye ndio anawabadili.

Chadema badala ya kuleta mabadiliko, yenyewe ndio inabadilishwa...
 
CCM wamemaliza mchakato wa kumpata mgombea. Sasa waongee nini? na nani? Wa kuongea ni wale waliokatwa na kwa bahati mbaya badala ya kuongea kwenye vikao wanazungumza na magazeti ambayo mengi wanamiliki wenyewe. Halafu mbona anayelalamika ni mmoja tu na ndiye aliyekuwa na hofu tangu mwanzo kuwa jina lake litaondolewa? Mara likikatwa patachimbika, mara hakuna atakayethubutu kukata jina mara huwezi kuzuia mafuriko kwa mkono n.k. Kinachoonekana sasa baada ya kukatwa badala ya kuchimbika yeye ameanza kuchimba kaburi lake kwa kifo chake cha kisiasa.
 
Subiri siku Lowassa atakapokabidhiwa kadi ya CHADEMA ndiyo utawaona CCM.

MaCCM huwa hayakurupuki katika mashambulizi ya kisiasa.

Ukiona simba amelowa...

kwa hyo ni sawa na bomu limetegeshwa tu?
 
Watanzania wamestuka kwani CCM inataka kumtumia Magufuli(Good Person) kama chambo au mtego wa kuwanasia watanzania ili waendelee kubaki madarakani kuwatafuna watanzania. nyuma ya Magufuli kuna kundi la simba wala watu(ccm) wanasubiri
 
Unataka wakurupuke tu?Yanayoendelea ndani ya Ukawa unafikiri kwao yanawapendeza?
 
Hata Ccm Ilivokua Inafanya Mchakato Wa Kumtafuta Mwakilishi Wao Ukawa Ilikaa Kimya Pia,so Every Party Na Mda Wake Wakuongea Na Kujaza Headlines,huu Ni Mda Wa Ukawa
 
CCM ni wapuuzi sana ila si kwa kiwango mnachofikiria. subirini Kipyenga cha NEC kipulizwe ila cha kufurahisha sana ni kuwa huu ni uchaguzi Utaokutanisha matajiri watupu so tushuhudie wingi wa Helicopters, wingi wa Mabango, wingi wa Rushwa, wingi wa Misafara n.k
 
Tangu kuanza kwa drama za watu waliokatwa na wasiotakiwa ndani ya chama kuhama na wengine kutishia kuhama chama..naona ccm wako kimya tu,ukimya wao utakua unaashiria nini?

Kwani walipomuimbia mwenyekiti wana imani na Lowassa walimaanisha nini?
 
Na huo ndio ukomavu wa kisiasa,kelele na fujo sio issue,viva ccm
 
Tangu kuanza kwa drama za watu waliokatwa na wasiotakiwa ndani ya chama kuhama na wengine kutishia kuhama chama..naona ccm wako kimya tu,ukimya wao utakua unaashiria nini?

Watajua wenyewe! Huenda wamelazimika kusikilizia utamu wa sindano ya ukawa!
 
Ccm wanatafakari jinsi ya kumuondolea kinga ya kutoshitakiwa Lowasa.
 
Tangu kuanza kwa drama za watu waliokatwa na wasiotakiwa ndani ya chama kuhama na wengine kutishia kuhama chama..naona ccm wako kimya tu,ukimya wao utakua unaashiria nini?

Wana mengi ya kushughulikia zaidi ya kujadili mambo ya mwanachama mmoja mmoja. Walishawajadili wagombea 38, na mshindi kashapatikana, safari ni moja tu kuelekea 25/10 na nguvu zote wanazielekeza huko.

Kumbuka CCM ndio wako serikalini, mahitaji ya wananchi yanaendelea, miezi miezi mitatu ni kingi ya kuendesha serikali hivyo kujadili mambo ya mitaani hawana muda. Pili hakuna katika hao vinara waliopeleka malalamiko katika vikao vya CCM kuelezea kutoridhishwa kwao na uchaguzi. Tatu hakuna kati yao hata Lowasa aliyeita waandishi wa habari na kutoa tamko ama la manunguniko au kukitupia lawama kikao au uongozi wa CCM.

Sioni sababu kwanini CCM itoa matamko, sijui kama ya mtu na mtu na sio chama.
 
Back
Top Bottom