Hivi Mawaziri hawastaafu?

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Bado naendelea kujiuluza hilii swali jamani hivi mawaziri hawastaafu?

Na vipi wabunge wawe na kikomo cha uongozi badala ya kuendekeza mtu mmoja anakufa unasikia alikuwa mbunge miaka 30 unawaza hapo kwake ndie alikuwa na elimu kuliko wote ama? Tunaomba hasa wabunge wapewe kikomo miaka 10 tosha.

Otherwise tunawe mikono Waganda wamekimbia lockdown wako Mwanza Bukoba, Arusha na sasa Dar

Hali sio nzuri sana
 
Shida yako unadhani labda wakiwa na ukomo na wewe utapata nafasi, hakuna pambana umtoe, hata huko tunakojifunza democrasia hakuna ukomo kwa Mbunge
Mkuu mpaka wanijue lazima wavuke boda labda waanze na weewe huko!!
Kazikwenu uliza nafanya nn HUKU..MAPAMBANO Muhimuu
 
Waziri, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya, DAS na RAS hawa hawastaafu. Huondolewa kwenye nafasi zao!
 
Siku kukipambazuka tutawakuta wenzetu wako mwezini
Mkuu sisi acha tuendelee kunywa alkasusi ilitukomeshe akina mama majumbani. Mfumo mbovu wa utawala Africa ndiyo adui no 1, angalia nchi ina watu zaidi ya milioni 50 lakini inategemea mawazo ya mtu mmoja na siyo mawazo ya watu wengi.

Ndugai anaogoza chombo kikubwa sn lakini angalia the way alivyo unategemea nini? bila kubadilisha mfumo wa kiutawala tutaendelea kusindikiza wenzetu.
 
Mtela Mwampamba aliyekuwa DAS wa Kisarawe kastaafu lini?
Utakuwa na shida kichwani wewe, tofautisha kustaafu na kutenguliwa, kwani alifikisha miaka 60? RAS, DED na DAS wakitenguliwa huwa wanapangiwa kazi nyingine kwenye utumishi mpaka watakapo fika umri wa kustaafu, pia elewa hata mhudumu wa ofisi anaweza kufukuzwa kazi kama ilivyo kwa DAS, RC na DC akitenguliwa hapangiwi kazi yoyote kwenye utumishi wa umma ndiyo maana hawakatwi PSSSF kama ilivyo kwa RAS na DAS na wala hawapo kwenye mfuko wa matibabu NHIF kama watumishi wengine.
 
Back
Top Bottom