Hivi Managers wa kiume mkoje?

katoto kazuri

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
6,083
5,659
Mdogo wangu yupo kwenye kampuni halafu ameshaniletea matatizo Manager wake anamtaka taka na yeye hana muda naye. I mean hawaendani; amemsumbua kuanzia mwezi wa kwanza hadi huu wasita na mpaka now amempa matatizo kabisa.

Sasa leo kaja home kasema haendi tena shughulini kisa huyo Manager, sasa mimi nifanyaje, na kazi kupata ni shughuli?
 
Anase tu suhahidi wa video halafu amuonye kuwa akiendelea kumletea matatizo atamchukulia hatua.
 
Pole sana dada
Hiyo ni changamoto kwa kwa baadhi ya watu wanaopewa madaraka ambao hawajitambui;
Napendekeza yafuatayo;
1. Kama anayemfuata ni line manager na sio Director (top director) au mwenye kampuni ASIACHE KAZI
2. Awe mjasiri na kuweza kumfuata na kumwambia kuwa, anasikitika hawezi kuwa na yeye kwa sababu amesha chumbiwa na anasubiri taratibu zingine ziendelee.
3. Kama kampuni ina wamama wenye madaraka au hata wa kawaida; aangalie mama mmoja anaye muona ana busara amuambie akijifanya anaomba ushauri kwa changamoto anayopitia. Naamini atampa ushauri unaoendana na muundo wa kampuni
4. Kama kampuni ina HR (anayeonekana ni mtu muelewa); anaweza kuangalia namna ya kufikisha changamoto yake ila awe muangalifu kwani huyo manager akiitwa atakaa
5. Ajitahidi kuwahi kazini na kuwa mchapakazi na kujituma kwa ziada . Hiyo itamfanya awe ana aminiwa sana Kazini na hivyo akisema chochote ataaminiwa na kampuni haitakuwa tayari kumpoteza
6. Suala la takukuru au Polisi sijaliunga mkono kwa sasa; nafikiri ni vizuri atumie kwanza mbinu rafiki kwani mwisho wa siku huyo Manager (hajataka kumbaka) lakini pia anafamilia inayomtegemea na pengine akienda huko takukuru anaweza kuanza kuwekewa Visa vitakavyomfanya aache kazi hapo kwenye shirika
 
Mbona simple tu dada, mwambie aendelee kwenda kazini ila aseti mtego was kukusanya ushahidi usiokuwa na Shaka, hakikisha anakuwa na device ya kurekodia vedio ili atakapokuwa anaendelea kusumbuliwa basi anarekodi tu na mission ikisha kuwa accomplished ndo anampasukia bila mshipa was aibu kuwa akome kuendelea kumsumbua la sivyo utamtia ndani maana ushahidi una.
 
Back
Top Bottom