Hivi mama Salma Kikwete anasema ukweli?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,467

Source: Michuzi

Ukiangalia hiyo khanga iliyokunjwa kama mtandio aliovaa/ aliojitupia mama Salma Kikwete ina maandishi yanasema: "We Cherish Democracy" (yawezekana kule nyuma kuna maandishi mengine lakini haya yamekamilisha sentensi). Maneno hayo anaambiwa mama Bush na Bush na yanatoka kwa 1st lady na mumewe JK ambaye anawakilisha serikali na CCM.

Ukiangalia mchakato mzima wa kupata viongozi hapa nchini - Tume ya Uchaguzi, Vyama vya siasa, Usajili wa vyama vya siasa, nk. je, ujumbe huu ni wa kweli?
 
Tumeshazoea kudanganywa,tuchukue hatua kama MPENDAZOE.

CHIEF MGALULA:
Naomba nikusahihishe kidogo kama ifuatavyo:
Mimi naamini hatujawahi kudanganywa hata siku moja, isipokuwa labda huwa tunalazimika kujifanya kuwa tunadanganywa wakati tunajua kuwa "TUNAJUA TUNAGANYWA". Vile vile, na wanaotudanganya, pia nao wanakuwa wameshajua kuwa "tunajua kuwa wanatudanganywa". Unadanganywa pale ambapo utashindwa kujua kuwa unadanganywa, ukishajua kuwa unadanganywa, hapo hudanganywi tena, aidha unakuwa UNALAZIMIKA kudanganywa au UMELAZIMISHWA kudanganywa na siyo otherwise!
 
Tutaacha lini ku assume?
Michango mingi hapa JF kuhusu mama Salma imelenga kumbeza kwamba hajui hiki wala kile.Kwa wale wasiomfahamu kwa karibu naomba mfahamu machache kumhusu huyu mama:
1. Ni mama mwenye elimu yake inayomtosha kuenea kwenye hicho kiti cha u first lady ( FL hupatikani by virtue of a woman's marriage kwa mkuu wa nchi na siyo kwa kuapply, kufanya interview, kuonyesha makaratasi - academic credentials, au kuonyesha uzoefu)
2. Mama wa kwanza anajua kiingereza as a third language kama walivyo watanzania wengi including walio members JF.So kusema ati hajui kilichoandikwa kwenye mtandio wake si sahihi.Wengine hubeza wenzao bila sababu..afterall kiingereza ni lugha tu kama lugha nyingine hakuna cha ajabu kukijua.Kuna mtu anajua kiingereza lakini substance kwenye analoongea ni almost 0!
3. Huyu mama anafanya mengi makubwa hasa kwenye elimu ya wasichana na kupambana na UKIMWI.Tumpe heshima yake.
4. Tumheshimu kama mama, mke wa mtu, mke wa kiongozi.Sidhani kam ndugu unayesoma hii thread na nyingine ungefurahi kuona watu wasiomfahamu mkeo, mama yako, dada yako wakimshambulia na kumponda. TUWE WASTAARABU JAMANI.

Kama kuna la maana la kumpondea liwekwe kistaarabu badala ya kuanzisha thread rejareja zisizokuwa na mantiki.
 
W020100311787745779867.jpg
W020100311787745789518.jpg

H.E. Ambassador Liu Xinsheng explained the performence programme to H.E. Mama Salma Kikwete​

W020100311787745766610.jpg
W020100311787745773081.jpg

2241507373_bbf8c687be_o.jpg

2242304068_c8006e120d.jpg
<SCRIPT type=text/javascript>Y.E.onDOMReady(show_notes_initially);</SCRIPT>
2241536655_540d01c2cf.jpg
<SCRIPT type=text/javascript>Y.E.onDOMReady(show_notes_initially);</SCRIPT>​

WhiteRibbonDay2010_500x417.jpg

GetFile.aspx

safe_image.php

sk.jpg

Mama Salma Kikwete akimpongeza Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kwa zaidi ya silimia 99 kuwa mgombea pekee wa Urais kwa tiketi ya CCM​

NB: ACHENI UTANI NA MAMA....
 
Tutaacha lini ku assume?
Michango mingi hapa JF kuhusu mama Salma imelenga kumbeza kwamba hajui hiki wala kile.Kwa wale wasiomfahamu kwa karibu naomba mfahamu machache kumhusu huyu mama:
1. Ni mama mwenye elimu yake inayomtosha kuenea kwenye hicho kiti cha u first lady ( FL hupatikani by virtue of a woman's marriage kwa mkuu wa nchi na siyo kwa kuapply, kufanya interview, kuonyesha makaratasi - academic credentials, au kuonyesha uzoefu)
2. Mama wa kwanza anajua kiingereza as a third language kama walivyo watanzania wengi including walio members JF.So kusema ati hajui kilichoandikwa kwenye mtandio wake si sahihi.Wengine hubeza wenzao bila sababu..afterall kiingereza ni lugha tu kama lugha nyingine hakuna cha ajabu kukijua.Kuna mtu anajua kiingereza lakini substance kwenye analoongea ni almost 0!
3. Huyu mama anafanya mengi makubwa hasa kwenye elimu ya wasichana na kupambana na UKIMWI.Tumpe heshima yake.
4. Tumheshimu kama mama, mke wa mtu, mke wa kiongozi.Sidhani kam ndugu unayesoma hii thread na nyingine ungefurahi kuona watu wasiomfahamu mkeo, mama yako, dada yako wakimshambulia na kumponda. TUWE WASTAARABU JAMANI.

Kama kuna la maana la kumpondea liwekwe kistaarabu badala ya kuanzisha thread rejareja zisizokuwa na mantiki.

Kikwete amesema kwenye hotuba yake ya kuchaguliwa kuwa mgombea kwa ticket ya CCM,kwamba kunyamazia matusi anayotukanwa yeye pamoja na familia sio kwamba hajui ama hawezi kuchukua hatua madhubuti,ila anatoa uhuru wa maoni.Alisema kama angetaka,hata hao amnesty angewafukuza nchini,akauliza hivi hatuoni hata hizi nchi za jirani?Ni ukiritimba tu wa viongozi kwende mbele na hakuna uhuru wa vyombo vya habari wala nini,na wanapeta tu.

Mimi nadhani Kikwete ka succeed katika uvumulivu wa kisiasa.Maana hapa jamvini wakubwa kwa watoto,wote wanajifunzia mitusi yao kwao hii familia.Halafu nashangaa sana ,ukienda kule kwenye Facebook ya Kikwete..mijitu kibao kama siyo yote inamfagilia,au sijui kwa sababu kule twatumia majina yetu yanayokaribiana na ukweli au majina halisi..HYPOCRISY..am sure ndio sisi tuliomo humu.

Tukosoe sera zake,na sio tufanye character assesment....mimi inanikera kwa sababu nawachukulia kama my daddy n mom..kama ilivyo kwa kiongozi mwingine yoyote.

Peace

Qadhi
 
Tutaacha lini ku assume?
Michango mingi hapa JF kuhusu mama Salma imelenga kumbeza kwamba hajui hiki wala kile.Kwa wale wasiomfahamu kwa karibu naomba mfahamu machache kumhusu huyu mama:
1. Ni mama mwenye elimu yake inayomtosha kuenea kwenye hicho kiti cha u first lady ( FL hupatikani by virtue of a woman's marriage kwa mkuu wa nchi na siyo kwa kuapply, kufanya interview, kuonyesha makaratasi - academic credentials, au kuonyesha uzoefu)

Mama Salma ni mwalimu wa shule ya msingi, na nasikia hana uwezo wa kufundisha zaidi ya darasa la nne. Kwa maana hiyo atakuwa mwalimu wa cheti, yawezekana daraja B. Kigezo cha kuwa 1st lady ni kuwa mke wa rais wa nchi basi.

2. Mama wa kwanza anajua kiingereza as a third language kama walivyo watanzania wengi including walio members JF.So kusema ati hajui kilichoandikwa kwenye mtandio wake si sahihi.Wengine hubeza wenzao bila sababu..afterall kiingereza ni lugha tu kama lugha nyingine hakuna cha ajabu kukijua.Kuna mtu anajua kiingereza lakini substance kwenye analoongea ni almost 0!

Thread haingolei kuwa anajua au hajui Kiingereza, bali je, ujumbe alioubeba na kuwafikishia wageni kutoka US ni kweli. Sio kwamba amebeba ujumbe hasioufahamu. Ungeweza kuwaambia wachangiaji wasitoke nje ya mada. Kwa kifupi Kiingereza hakifahamu vizuri na ndio maana JK alipokaribia au alipopata urais mama JK alipewa crash course ya Kiingereza! Kwanza wewe ndio umeleta mada tofauti na mpya kabisa! Ungekuwa unajibu mtihamu matokeo yako ni ZERO.

3. Huyu mama anafanya mengi makubwa hasa kwenye elimu ya wasichana na kupambana na UKIMWI.Tumpe heshima yake.

Elimu ya wasichana ndio elimu gani hiyo? Elimu ya uzazi? Au msichana alivyo? Au unamaanisha 'wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari? Tuambie mambo anayofanya kwa kutoa takwimu na kulinganisha na waliomtangulia au wa nchi jirani.

4. Tumheshimu kama mama, mke wa mtu, mke wa kiongozi.Sidhani kam ndugu unayesoma hii thread na nyingine ungefurahi kuona watu wasiomfahamu mkeo, mama yako, dada yako wakimshambulia na kumponda. TUWE WASTAARABU JAMANI.

Nafikiri michango imeenda tofauti na mada ya thread hii kama nilivyosema mwanzo, hivyo ulitakiwa kuliona hilo na kuwakumbusha wana JF lakini sio kuongelea ustaarabu, furaha, heshima na mengineyo. JF sio kwa ajili ya kumfurahisha mtu. Katiba yetu inaruhusu uhuru wa kuongea bila kuvunja sheria. Sheria ipi imevunjwa hapa!

Kama kuna la maana la kumpondea liwekwe kistaarabu badala ya kuanzisha thread rejareja zisizokuwa na mantiki.

sifa za Thread rejareja ni zipi? Je, thread hii haina mantiki kwa kuzingatia kichwa na utangulizi wake pamoja na hiyo picha? Unataka nami nifanye upuuzi huu wanaofanya wengine kwenye video hii YouTube - WAMA FOUNDATION ACTIVITIES? mimi nafuata katiba ya nchi yetu tu; 1st lady hayumo kwenye katiba!!
 
Back
Top Bottom