Hivi Malezi ya aina hii ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Malezi ya aina hii ni sahihi?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Jimmy Romio, Aug 10, 2012.

 1. Jimmy Romio

  Jimmy Romio JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 253
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Mara nyingi nimeona familia ambazo zina jiweza kiuchumi zinawalea watoto kama mayai vile kitu ambacho kwa mtazamo wangu nanona kama ni sio vizuri kwa sababu mtoto anakosa uelewa wa vitu vidogo vidogo vya "kidomestic"

  Kwa mfano unakuta nyumbani kuna msaidizi wa kazi hgirl ambae anafanya kila kitu, kuosha vyombo, kufua kudeki, kupika na kadhalika. Watoto hawagusi chochote hata kama ni mtoto mwenyewe anataka labda kufua au kupika anakatazwa na kuambiwa nenda kasome. Kwa hiyo watoto kama hawa wanakuwa katika hali hoyo ya kujifunza domestic activities na pindi wanapokuja kujitegeme inakuwa issue. Kwa mtazamo wangu malezi kama haya sio sahihi, Mtoto ajifunze kupika, kufua, usafi wa ndani n.k kwa faida yake baadae.

  Regards
   
 2. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Uko sahihi kabisa wala hujakosea,nakumbuka wakati naanza maisha nilikuwa na jamaa hajui hata yai linakaangwa vipi,anasema maisha yake yote hajawahi ingia jikoni alikomaje sasa..
   
 3. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,129
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Hapo umenena Jimmy Romio. Zipo nyumba (wala si lazima za kitajiri) zinazolea watoto kwa makosa. Mtoto ni mvulana hagusi kitu. Mara zote anaambiwa "Usihangaike babangu, kama ni nguo zako ntakufulia" Huyu mvulana yuko darasa la tatu kwa mfano na hafui wala kufanya kazi yoyote hapo nyumbani, anabembelezwa tu. Hata nguo zake za ndani anafuliwa. Chumba chake hagusi;kinafagiliwa na kudekiwa. Hii nimeiona kwa macho wangu na akina mama ndio wadekezaji wakubwa wa watoto wa kiume hasa pale mtoto huyo ndiye pekee wa kiume katika nyumba hiyo, au kama huyo mama alimzaa baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu kushika mimba. Mtoto anageuka kitu cha ajabu hajui kufanya chochote.

  Yupo mmoja aliyelelewa namna hii akamaliza darasa la saba sasa kivumbi kikatokea alipoenda sekondari ya bweni. Ilibidi afuliwe na vidume wenzake ambao walidai malipo! Akawalipa! Mamayake aligundua habari hii kijana wake alipomaliza kidato cha nne kipindi ambacho kijana alishakubuhu kwenye huo mchezo! Mama aliugua presha kali na kusema mtoto wake kalogwa na najirani. Kweli tunaharibu wenyewe watoto wetu bila kujua kwa kisingizio kwamba tunawapenda. Enyi akina mama wa JF wenye watoto wa kiume!Hakikisha mwanao anafua nguo zake mwenyewe na chumba chake (kama anacho) anakifanyia usafi pamoja na kazi nyingine hapo nyumbani afanye. Kazi zinajenga sana tabia za watoto.

  Nakushukuru sana mleta mada,
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  du hasa kwa watoto wakiume jamii zetu bado zinamchukulia mtoto wa kiume hawezi pika,osha vyombo
   
 5. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli wazaz wanafikir wanawasaidia watoto wao kumbe wanawahari,
  kwa mfano mie nna rafiki yangu mmoja ni mdada, huyu kalelewa maisha hayo ya kwamba hata nguo na usafi wa room anafanyiwa na mfanyakaz wa ndan, kwa sasa anachezea 27, ana mchumba na yupo kwenye process za kuolewa lakn bibie, hajui kupika, anajua kufua ila kupasi shughuli..., yaan anaweza kufanya vitu vichache mno na siyo kwa usahh pia, saa hz ndio mwenyewe ameanza kujishtukia.......................
   
 6. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Uko sahihi kabisa that's absolutely reality how to treat our chirldrens.
   
Loading...