Hivi maiti ni lazima kumvalisha sanda?

Sanda: ni kitambaa cheupe. Ambacho hufungwa ktk mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa.
Na hautaulizwa na mtu kama mpendwa wako marehemu hutamvisha kitambaa(sanda) hicho kwani ni utaratibu tu watu tuliojiwekea na sio sheria.
Nguo yoyote ile marehemu anazikwa nayo.. Ila ukimzika bila nguo yoyote(uchi) itakuwa picha mbaya.
 
SANDA ni nguo mfano wa shuka anayo vishwa maiti kabla ya kuzikwa na kuzikwa nayo na huwa zinakuwa 3. Kwani mtume pia alivishwa SANDA TATU.

SANDA iwe nyeupe lkn ikiwa haikupatikana ya rangi nyeupe basi itaruhusiwa ya rangi nyingine. Mtume kasema: Pendeleeni kuvaa mavazi meupe kwani hayo ni katika mavazi bora kwenu na muwavishe maiti wenu kwa hizo sanda).

Mafundisho yanatutaka tuwavishe maiti SANDA na wala sio SUTI au nguo nyinginezo.

Huo ni utaratibu wa UISLAM
 
Back
Top Bottom