Hivi Mahakama ni Kisutu tu?

Cko deep sana na mifumo ya kimahakama bt what I'know ni Mahakama ya kinondoni ni ya wilaya Kinondoni same to Samora ambayo ni ya Ilala na mahakama ya Temeke ambayo ni ya wilaya ya Temeke.. Kisutu inapata Power ya kusikiliza kesi ambazo zingefaa kusikilizwa high court under extended jurisdiction sec 173 CPA(Nimeuliza wajuzi)
Sehemu ndogo uko sahihi. Kinondoni ipo Mahakama ya wilaya na ya Hakimu Mkazi. Kama umefika pale unapoingia getini mkono wako wa kushoto ni District court na kulia ni Mahakama ya Hakimu Mkazi kama ilivyo kisutu. Extended Jurisdiction haipewi Mahakama anapewa Hakimu mhusika. Mahakama moja yaweza kuwa na Hakimu mmoja au wawili wa hivyo. Mfano pale kisutu namfahamu In charge tu Mhe Mkeha ndiye Mwenye extended jurisdiction.
 
Hakuna mahakama ya mkoa kwenye muundo wa mahakama. Kuna mahakama ya wilaya ambayo ndiyo hiyo hiyo mahakama ya hakimu mkazi. So ukisikia mahakama ya wilaya basi ujue hakimu wake ni hakimu mkazi na anaweza kaa kwenye mahakama yoyote ya hakimu mkazi. Siku hizi hata mahakama za mwanzo wanaajiriwa mahakimu wakazi. So Kisutu na mahakama ya Wilaya Kinondoni zote zina mamlaka MOJA kisheria. Suala la kwanini kesi nyingi zinafunguliwa Kisutu ni masuala tu ya Kijiografia (Territorial jurisdiction) na Kisutu ndio ina territorial jurisdiction ya Dar (Ufafanuzi wa kina wahitajika so tafuta mjuzi akuelekeze)
Mkuu umechanganya kidogo.Ipo mahakama ya wilaya na ina mamlaka yake na ipo mahakama ya hakimu mkazi na malaka yake pia.Mahakama zote hizi zima mamlaka tofauti.Kenobi hakuna kitu kinaitwa mahakama ya mkoa ktk muundo wa mahakama nchini na rufaa toka mahakama ya wilaya unaenda direct High Court.
 
"Mamlaka" ni nini? tuanzie hapo. Na yataje "mamlaka" unayosema yanatofautiana.
 
Hata hakimu wa Kinondoni anaweza kupata nguvu hiyo (Extended Jurisdiction) coz ni hakimu mkazi na yeye kama yule wa Kisutu. Hii nguvu haipewi MAHAKAMA anapewa HAKIMU mkazi anayekuwa akisikiliza shauri husika.
Unapsikia Kisutu hakuna hakimu mmoja, ukienda pale kuna kesi hata nane zinaendeshwa kwa wakati mmoja na mahakimu tofauti
 
Ni hivi, mahakama ya Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu 2, (nitaanzia ya juu kabisa)
1. Mahakama kuu ambayo inahusisha (a) Mahakama ya Rufani (Court of Appeal) na (b) Mahakama kuu (High court) hizi zote mbili zipo katika kundi la mahakama kuu, Mahakama ya Rufani in mamlaka bara na visiwani, lakini mahakama kuu ina mamlaka yote kwa Tz bara.

2. Mahakama za chini (subordinate courts)
i. Mahakama ya Hakimu mkazi wa mkoa
ii. Mahakama ya wilaya
iii. Mahakama ya mwanzo

I. MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI (COURT RESIDENT MAGISTRATE)
Hii ipo moja katika kila mkoa, kwa maana ya kuwa na mamlaka juu ya mashauri yote yanayotokea ndani ya mkoa katika kiwango (jurisdiction) kilichowekwa

II. MAHAKAMA YA WILAYA (DISTRICT COURT)
Hii ipo moja katika kila wilaya kusikiliza mashauri yanayoangukia katika mamlaka yake ndani ya wilaya hiyo

III. MAHAKAMA YA MWANZO (PRIMARY COURT)
Hizi zipo katika kila wilaya na zinaweza kuwa zaidi ya moja kulingana na ukubwa wa eneo husika, na husikiliza mashauri madogo (yaani kesi ndogondogo)

Linapotokea suala ambalo mtu atahitaji kwenda mahakamani, mtu huyo haamui tu kuchagua mahakama gani aende kufungua shauri (case) lake, kila kesi ina uzito wake iwe ya madai au ya jinai (isipokuwa masuala ya mirathi na ndoa za kiislam) mfano mtu anayekudai milioni 20 hawezi kwenda fungua shauri lake mahakama ya mwanzo, kwa kuwa haina nguvu ya kusikiliza kesi za madai zinazozidi millioni 10, hivyo mtu huyo atatakiwa kupeleka shauri lake mahakama ya wilaya ambayo makubaliano ya kupeana hizo hela yalifanyika, mkataba ukifanyikia Arusha, hamuwezi fungua kesi Iringa kwakuwa wote mnaishi Iringa, kesi itatakiwa ifunguliwe Arusha, hayo nayo ni mamlaka.

Kimsingi kuna vitu vingi vya kimamlaka vya kuangalia kabla hujafungua kesi katika mahakama fulani, na ukikosea ukafungua kesi kwenye mahakama isiyokuwa na mamlaka, basi kesi yako itatumbiliwa mbali.

Hivyo Kuona kisutu kunakuwa na kesi nyingi ni kutokana na ukubwa (siyo wa eneo) wa jiji wa Dar es salaam, ndiyo maana hujawahi sikia mbunge lema amepelekwa kisutu, au BUlaya amepelekwa kisutu.

so hili ni suala la kisheria
Upo sahihi lakini mahakama ya Hakim mkazi zaweza kuwa zaidi ya moja nfani ya mkoa.Kawaida hizi hukutwa kwenye majiji, miji na manispaa.Japo zote zitajulikana mahakama ya hakimu mkazi lakini huwa tofauti.Unaweza sikia mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni.
 
"Mamlaka" ni nini? tuanzie hapo. Na yataje "mamlaka" unayosema yanatofautiana.
Mamlaka ya kuendesha mashauri.Mahakama ya mwanzo ina aina za kesi inazoruhusiwa kusikiliza, kadhalika wilaya, mkazi na High Court. Mfano mashauri yote kuhusu haki za binadamu, mauaji, ubakaji hayawezi kufunguliwa wala kusikilizwa mahakama ya mwanzo.
 
Upo sahihi lakini mahakama ya Hakim mkazi zaweza kuwa zaidi ya moja nfani ya mkoa.Kawaida hizi hukutwa kwenye majiji, miji na manispaa.Japo zote zitajulikana mahakama ya hakimu mkazi lakini huwa tofauti.Unaweza sikia mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni.
...sawa, hiyo nakubaliana na wewe, kiufupi mahakama inaweza kuwa popote pale alipo hakimu kiofisi, lakini hatuwezi kuwa na court of resident magistrate of kinondoni, tunaweza kuwa na Court of Resident Magistrate of Dar es Salaam at Kinondoni

nafikiri hapo ntakuwa nimejaribu kuelewesha. maana yangu kwamba kinondoni haiwezi kuwa na territorial jurisdiction over Dar es Salaam, kwa sababu kinondoni ni wilaya
 
Kisutu ndiyo Mahakama ya Hakimu mkazi ya mkoa wa DSM. Inatwa The Resident Magistrates' Court of Dar es Salaam at Kisutu.
Hata Kinondoni ni ya Dar nzima. Inaitwa Resident Magistrates' Court of Dar es Salaam at Kinondoni. Kisutu inatumika sana kutokana na uwa karibu na Mahakama Kuu kwakuwa hujitokeza logistics za kwenda na kurudi Mahakama Kuu ya Tanzania.

Mzee Tupatupa
 
sasa hiyo siyo ya kinondoni, kinondoni location tu ndugu, ingekuwa Court of Resident Magistrate of Kinondoni at Kinondoni hapo sawa
 
sasa hiyo siyo ya kinondoni, kinondoni location tu ndugu, ingekuwa Court of Resident Magistrate of Kinondoni at Kinondoni hapo sawa
Unahitaji kuelewa au kubishana? Nasema kuwa hata Mahakama ya Kinondoni nayo ni Dar nzima. Resident Magistrate Court of Dar es Salaam ina Kisutu na Kinondoni. Kafanye utafiti kama ulikuwa hufahamu

Mzee Tupatupa
 
...sawa, hiyo nakubaliana na wewe, kiufupi mahakama inaweza kuwa popote pale alipo hakimu kiofisi, lakini hatuwezi kuwa na court of resident magistrate of kinondoni, tunaweza kuwa na Court of Resident Magistrate of Dar es Salaam at Kinondoni

nafikiri hapo ntakuwa nimejaribu kuelewesha. maana yangu kwamba kinondoni haiwezi kuwa na territorial jurisdiction over Dar es Salaam, kwa sababu kinondoni ni wilaya
Sawa mkuu ila mahakama ya hakimu mkazi Dar zipo nyingi mf.Kisutu resident magistrate court,Sokoine drive resident magistrate court kwa uchache upande wa Dar. Kwenye majiji makubwa na manispaa zinakuwa nyingi kurahisisha upatikanaji wa haki.Fanya followups utajua.Kutajwa Dar ni kutambulisha location yake lakini haina tafsiri kuwa ni mahakama ya mkoa japo ni kweli territorial jurisdiction yake ina-cover mkoa mmoja.Hat a kphuundo wa mahakama haitamkwi kuwa mahakama ya mkoa.
 
Naona wanasheria wa kwenye madesa wanapigana vikumbo swali ni kwanini hawajafungua kesi kinondoni wakaenda kisutu...?
 
Soma kijarida cha muundo wa Mahakama
 
Attachments

  • T2 - Muundo Mahakama Book.pdf
    192 KB · Views: 793
Mkuu hujapata faida ya kufahamu mengi kupiga swali ulilolita la kitoto? Kama unafahamu weak majibu sahihi hapa tushare. Wengine hatujui mambo mengi na kuuliza ndio kujifunza.
Huchelewi pia kuuliza kwanini Hosp. MHIMBILI tuu kwani hakuna zingine? Kwann isiitwe TAIFA? Maswali mengine huwa ni ya kitoto sana
 
Kwahiyo mkuu Mahakama ni mtu na sio taasisi?
kisutu ndo yenye territorial jurisdiction over dar es salaam

ikumbukwe pia kuwa mahakama sio jengo bali ni hakimu/jaji

kwa mfano judge wa high court akikaa kisutu on record itaandikwa "in the high court of ..... sitting at kisutu" (emphasis is mine)
 
Back
Top Bottom