Hivi mahakama inaweza kutengua amri ya Serikali ya kutokukusanyika ?

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Mimi nadhani mahakama haina uwezo wa kutengua amri ya serikali katika hili.

Uchaguzi wa mwaka huu una "tension" au nadhani wanaita mhemuko sana na wakati wa kampeni yameshuhudiwa matukio ya baadhi ya makundi kudhani yanaweza kutumia nguvu kubadili itikadi za makundi mengine.

Haya yanamfanya yeyote aliyepewa dhamana ya kulinda usalama wa watu wote kutabiri mikusanyiko inaweza kusababisha wengine kunyimwa haki yao au kuleta uvunjifu wa amani. hata kama mwenye dhamana huyu anakuwa na ajenda ya siri lakini kwako wewe kujumuisha kitu haramu katika mpango wako wa kujilinda unakuwa umeharamisha mpango mzima na unampa sababu ya kukupambana na mpango wako.

Sheria ya uchaguzi inaweza kuibana tume lakini serikali kwa ujumla wake inayomamlaka ya kuzuia mikusanyiko hata kama mikusanyiko hiyo imehalalishwa na sheria lakini kama itaonekana kutaka kuvunja amani, sembuse jambo ambalo halijatajwa na sheria kuwa halali?

Wananchi wanaweza kudai na kupata haki zao ikiwa hawa watahakikisha kuwa njia zao za kudai haki hizo haziingilii haki za wananchi wengine na kama madai ya haki yakionekana yanaingilia haki za wengine serikali inaweza kuamua lolote ama kusimamia haki wa wanaodai na kuwatimizia au kusimamia haki za wanaoelekea kukwazwa na madai.


Busara za makundi yote yanayohusika ndiyo hujenga amani au kubomoa amani.

Makundi yote yanaweza kuwajibishwa kwa matokeo ya zoezi zima kama limesababisha uvunjifu wa amani.

Walio andaa mchakato wa kudai haki kama madai yao si sahihi au madai yao ni sahihi lakini wametumia njia haramu kudai haki wanaweza kufikishwa kwenye sheria kuwajibishwa kwa matokeo.

Waliokuwa na dhamana ya kulinda usalama kama badala ya kulinda usalama wao walifanya matendo ya kuchochea uvunjifu wa amani basi wanaweza kufikishwa kwenye sheria kuwajibishwa.

Kwa wananchi wao malipo yao ni kwenye mchakato moja kwa moja, wengine wanaweza kuumia, wengine wanaweza kupoteza maisha na wengine wanaweza kupoteza mali.

Kila mmoja akitafakari mwenendo wake tunaweza kubaki na amani yeu milele.
 
Wewe unazungumzia ideal systems,systems ambazo haki na sheria inatawala,sio Tanzania.Katika nchi hii hakuna separation kati ya mahakama na serikali,vyombo hivi ni kama chombo kimoja.Kwa hiyo kila jambo linaamuliwa on convinience basis na vyombo vyote viwili, sio kwa kufuata haki na sheria.
 
Back
Top Bottom