Hivi Magufuli anayajua haya?

nyumbatatu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,076
938
1. Watu kusombwa na malori huku wakilipwa posho kwa lengo la kutengeneza tunachoshindania kwa siasa za sasa " mafuriko!".

2.Kundi watu waliopatikana kwa mtindo hapo juu kutegeshwa njia anayopita na kuwahutubia kwa maelezo wananchi wamemsimamisha (huku kosa la wazi la kiufundi likionekana la kuwavalisha sare za chama, katika joto la siasa za leo Ni vigumu mwanachama wa CCM kuzurura na nguo za chama).

3. Chama kulipa pesa nyingi wasanii ili kuvutia mafuriko ya ziada nje ya waliolipwa posho.Napenda kufahamu kama mh. Magufuli anayajua mambo haya na anayachukuliaje. Kama anafahamu matumaini ya ushindi anaohubiri kila siku huku akipiga push up anayatoa wapi?

Kama hafahamu wanaocheza mchezo huu wanamchukuliaje mgombea wao na wamemuandaaje kisaikolojia atakapobaini kura alizopata hazifanani na ukubwa wa mikutano aliyohutubia.

Nawasilisha.
 
Umesahau na ile mbinu nyingine ya kuchanganya picha zinazoenda kwenye tv ili kuonesha mkutano ulikua na watu wengi
 
Umesahau na ile mbinu nyingine ya kuchanganya picha zinazoenda kwenye tv ili kuonesha mkutano ulikua na watu wengi
Ni kweli, najua yapo mengi, tunaweza kushirikana kuona jinsi walivyoishiwa pumzi.
 
Umesahau na ile mbinu nyingine ya kuchanganya picha zinazoenda kwenye tv ili kuonesha mkutano ulikua na watu wengi
Du ahsante kaka kwa kuliona chili, nilidhani nimeshtukia peke Yang! Wenyewe waache kutumia nguvu kubwa kutupotosha wajikite kutueleza nano aliua viwanda vyetu name watavifufuaje ikiwa mbinu za Maisha bora kwa kila Tanzania, Ari mpya, Nguvu mpya name Kasi mpya zote zimefeli!?
 
Wanatengeneza mbinu yao ya goli la mkono kuwa huko alikopita ati hao wte ni wanachama wao hivyo hawakumpigia kura mtu mwingine ila yeye. Hivyo tukiona kunatokea mahesabu makuubwa huko tusilalamike.
Tz jamani kwa mbwembwe za kitoto ni zaidi.
 
Nimekusoma!. Ahsante!.
 
Back
Top Bottom