Unamshangaa Magufuli Badala ya Kumshangaa Mgombea mmoja aliekuwa anasema Jakaya ni Visionary Leader mwenye kipaji Pekee aliejaaliwa na Mungu lakini alipokatwa Dodoma akabadilisha Maneno.
Personally najua Magufuli ana mapungufu kadhaa lakini kwa kulinganisha na Wagombea Wengine naona anafaa Zaidi.
1995 Mwl Nyerere aliona Kikwete ni Bora kuliko Lowassa ndio sababu Lowassa alikatwa katika hatua za awali kabisa na ukiwauliza kina Kingunge Sababu gani Mwl Nyerere alimkata Lowassa ili tu assess kama bado ina hold au laa watapata kigugumizi. Kama JK huyu alievurunda mambo kadhaa bado alionekana Bora kwa Lowassa 1995 na baadae Lowassa na Rostam 2003 walikubaliana JK aanze kugombea 2005 kwa kuwa ni bora Zaidi tutegemee nini akipewa Dola Lowassa?
Tunamchagua Magufuli sio kwa kuwa ni bora la hasha tunamchagua Magufuli ili kuepusha Taifa letu kukabidhi wapiga Mission town. Tuliawasikiliza, tukawaamini 2005 lakini wakafanya Uhuni leo wanakimbia Kivuli chao
Lowassa, Kingunge, Makongoro, Mgeja, Msindai, Masha hawa wote walikuwa wanamtandao walioshiriki kwenye kila Ovu Mungu alilowah kulishusha Duniani ili Mtu wao JK ashinde 2005 na Kweli Mzee Mkapa akazidiwa Ujanja japo alijua ni Genge la wahuni akawapa Nchi leo tena wanabadilisha Sidiria wanakuja na M4C et tuwape Nchi labda ya kwenye Bongo Movies. JK akamalizane nao huko Mtaani akisha staafu kama hawakuheshimu makubaliano yao ya kurithishana Vyeo haituhusu.
Huu ni Uchaguzi wa kukataa Wahuni sio wa kuchagua Magufuli bali wakukataa Genge la Lowassa. Kura zitapigwa kukataa Wezi
Mwaka huu ni watoto wa viongozi na familia zao dhidi ya wanyonge.
Lowasa anaungwa mkono na wanyonge.
Magufuli anaungwa mkono na matajiri ndani ya CCM na watoto wa viongozi na mawaziri wanaotaka kuendelea kutunyonya.
Nchi ni mfumo sio Magufuli.
Ukiweka pembeni unafiki na ushetani wa kisisiem utakubaliana nami kuwa ndani ya UKAWA hakuna mabilionea hata watano tu wanaogombea udiwani na ubunge.
Miaka yote tumeona kuwa waliomuangusha Kikwete ni watendaji na sio yeye mwenyewe. Watendaji walikua ndio hao hao wanarudi tena kama wabunge na madiwani wa CCM.
Mabilionea na wafanyabiashara wakubwa sana wote wanagombea kupitia CCM.Leo hii Magufuli anaamini kuwa atawashinda watu waliompa urais.
Na umesahau kuwa sababu kubwa ya CCM kumpitisha Mkapa mwaka 1995 sio tu uadilifu bali ni ili chama kishinde uchaguzi.
CCM miaka yote wanachoangalia ni ushindi na sio vinginevyo. Nitaweka unafiki pembeni na kusema ukweli .Mwaka 1995 CCM waliona wazi kuwa Mrema alikua tishio na alikua muadilifu na ilikua ni vigumu kumshinda kutokana na hali iliyokuwepo.
Kwanza rais aliyepita alikua ni muislam yaani mzee ruksa.
Hivyo rais aliyefuata ilibidi awe mkristo jambo ambalo Mrema alikua ni wa dini hiyo.
Msuya na Kikwete ,Mkapa na Lowasa walikua na kila sababu ya kupita ndani ya CCM.
CCM wakatizama ushindi zaidi na kuona hatari ya kupoteza kura endapo wangemchagua mtu tofauti na Mkapa kwani mbali na Mrema kuwa mkristo lakini alikua wa dhehebu la Roma lenye waumini na wasomi wengi kuliko madhehebu mengine.
CCM wakatumia karata ya Mkapa kugawa kura za wakristo na hasa waroma ambao kwa kweli angesimama mtu mwingine pamoja na kuwa na sifa kama alivyokua Salim ama JK mwaka huo chama kingeweza kupoteza ule uchaguzi.
Hizo ni mbinu za ushindi za CCM.
Suala la kumkataa Lowasa na Hatimaye Msuya na Kikwete kutolewa pamoja na nguvu aliyokua nayo halikuwa kama tunavyodanganywa bali ni mbinu za ushindi.
Hali ikajirudia mwaka 2005.
CCM hawakumpitisha Kikwete kwa sababu ya mtandao kama tunavyodanganywa bali kwa sababu ya ushindi.
CCM iliona mziki wa Kijana Mbowe wa Chadema na CUF ya Lipumba ulikua mkubwa .
Wakaja na mbinu ya Rais Kijana anayekubalika. Mbali na ujana na kukubalika lakini pia JK alikua ni Muislam na rais aliyokuwa ametoka alikua ni mkristo hivyo ili kuvunja nguvu ya kipropaganda ya CUF ilibidi CCM ishindwe kumkwepa Kikwete. Na hapakua na namna kwani alikua amejaa ndani ya mioyo ya watanzania ukizingatia kuwa mwaka 1995 alishindwa ndani ya chama kimizengwe mizengwe.
CCM waliangalia namna rahisi ya kushinda. Na ni wazi kuwa endapo Mkapa angatumia ubabe kukata jina la Kikwete kama walivyofanya kwa mtu mpole Lowasa asiyejua kujitetea zaidi ya kutetewa na umma na Mungu bila shaka naye chama cha mapinduzi kingeporomoka na kufia mbali mwaka 2005.
Mwaka 2015 tetesi zilianza kusikika muda mrefu kuwa kama Lowasa atakatwa basi Magufuli ndiye angeweza angalau kuuzika kwa watanzania waliokua wameichoka CCM. Sio sifa za uadilifu zilizoangaliwa bali nani atawapa CCM ushindi.
Kama ni uadilifu Samweli Sita ,Mwakyembe,Nyarandu,Pinda ,Bilal,John Ramadhan na Mwandosya walikua wadilifu zaidi. CCM iliwatumia wazoefu wa siasa za ushindi wa mbele kwa mbele na kugundua kuwa Magufuli anatokea kanda ya Ziwa yenye wapiga kura wengi. Pamoja na ukweli kuwa rais wa awamu ya kwanza naye alitokea ukanda huo huo.
Sio tu sifa ya ukada wenye watu wengi bali mkristo wa dhehebu kubwa la Roma.
Jambo la kumshukuru Mungu ni kuwa watanzania wameshagundua mbinu hizo za CCM za kuwapatia ushindi kitapeli na kijanja kijanja huku wakiwaumiza kwa kuwachafua kwa maksudi na kimkakati watu wengine wenye sifa nzuri kiuongozi .
Mwaka huu wote wapo na Lowasa kutafuta mabadiliko kama alivyotabiri Nyerere.Watu hawajali tena ghilba na mbinu za udini,ukanda za CCM.
Mwaka huu watu wa dini na madhehebu yote wameamua kumchagua Lowasa ili kuuonyesha umma kuwa tanzania hatubaguani kwani sote ni ndugu na tuna haki sawa.
Watanzania wote tumechoka kuchonganishwa na kujengeana chuki kwa maslahi ya makada na viongozi wa CCM na familia zao.