Hivi mabilioni yale yanarudi vipi?

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
Nazungumzia mabilioni mengi ambayo Qatar anayatumia katika kujiandaa na uendeshaji wa mashindano ya kombe la dunia. Si mchezo, maandalizi ya gharama kubwa yanaonekana yakiendelea kwa mafanikio ya hali ya juu. Lakini ikiwa mashindano yenyewe ni ya mwezi mmoja tu, najiuliza sana;

Gharama zote zile zinarudi vp? au kwakuwa kuna mihela tu ya bure ya mafuta?

fifa wanagharamia gharama zote zile?

Baada ya mashindano hayo, qatar itavifanyia nini viwanja hivyo ikiwa hakuna ligi yoyote ya maana kwao?

Wenye ufahamu na biashara hii ya mchezo huu tufahamishane tafadhali!
nawasilisha
 
1. Waarabu hawaangalii faida ya mwezi mmoja wakati wa fainali za World Cup bali zaidi ya hapo (viwanja na hotel vitaendelea kutumika kwa tournament nyingine wakati ndege, hoteli, vivutio vingine vya utalii vinapata wateja. Kumbuka Qatar ana shirika la ndege matata duniani.
**Waarabu wanafanya haya si kwa dhiki na kupata faida ya haraka haraka bali PRESTIGE/STATUS, tena QATAR atafanya kufuru ili kuwaonyesha maadui zake (majirani...Saudia, UAE, Bahrain kuwa yupo imara pamoja na kumuwekea vikwazo kibao
 
Kwani viwanja vinabaki au vitaondoka ikijibu nitakuja tena
 
Wanajua watarudisha vipi pesa zao maana wanachofanya Qatar ni uwekezaji wanaweza wasirudishe hela yao yote kwa muda maalum lakini watafaidika kwa miaka itakayokuja nazani unaelewa maana ya uwekezaji?
 
1. Waarabu hawaangalii faida ya mwezi mmoja wakati wa fainali za World Cup bali zaidi ya hapo (viwanja na hotel vitaendelea kutumika kwa tournament nyingine wakati ndege, hoteli, vivutio vingine vya utalii vinapata wateja. Kumbuka Qatar ana shirika la ndege matata duniani.
**Waarabu wanafanya haya si kwa dhiki na kupata faida ya haraka haraka bali PRESTIGE/STATUS, tena QATAR atafanya kufuru ili kuwaonyesha maadui zake (majirani...Saudia, UAE, Bahrain kuwa yupo imara pamoja na kumuwekea vikwazo kibao
anhaa, kama ni hivyo sawa......kumbe kuna akili kubwa imetumika
 
Back
Top Bottom