Kombe la Dunia la FIFA 2026: Je Afrika Italinyakua?

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
303
518
Na Deus M Kibamba

Baada ya kutembelea Morocco na kushuhudia hamasa ya Wananchi wa taifa hilo kwenye soka na miundombinu mizuri na ya kisasa waliyonayo, nimeanza kushawishika kuwa inawezekana Afrika ikanyakua Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2026 au 2030. Endapo utabiri wangu utatimia, sherehe za miaka 100 ya maisha ya kombe la dunia tangu kuasisiwa kwake zinaweza kufanyika Afrika na ninaweza kuhisi kuwa Morocco itakuwa mwenyeji wa sherehe hizo. Pia, kwa urafiki unaoendelea kukua kati ya Tanzania na Morocco, watanzania tunaweza kupewa heshima ya kuongoza itifaki yote ya shughuli yenyewe, Ishaallah !
IMG-20230208-WA0008(1).jpg

Kwa wasiokumbuka, kombe la dunia lilianza kushindaniwa mara tu baada ya kuanzishwa kwa shirikisho la soka Duniani (FIFA) mnamo mwaka 1930.

Tangu wakati huo, michuano ya kombe la dunia imefanyika kila baada ya miaka mine ispokuwa mwaka 1942 na 1946 kwa sababu ya Vita kuu ya pili ya Dunia. Kwa hakika, michuano ya kombe la Dunia ni mikubwa kuliko michuano yote duniani ikifuatiliwa na mamilioni ya wapenzi wa soka ulimwenguni. Wakati Fulani, idadi ya watu waliotazama mtanange wa kombe la dunia walikadiriwa kuwa ni Zaidi ya milioni 700.

Kwa bahati mbaya, Afrika haijawahi kufanikiwa kubeba kombe la FIFA kwa miaka yote 93 hadi leo. Mara zote, kombe limezunguka Ulaya, Marekani kusini na kwingineko.Kwa mfano, Nchi ya Uruguay ndiyo iliyokata utepe wa kulibeba kombe la dunia mwaka 1930 ikifuatiwa na Italia iliyoshinda kombe hilo mwaka 1934. Kwa miaka iliyofuatia baadhi ya nchi zilirudia kunyakua kombe hilo hadi mara tano kama Brazil (1958, 1962, 1970, 1994 na 2002).
IMG-20230208-WA0010.jpg

Pia, Ujerumani ni mshindi wa kombe la dunia mara nne (1954, 1974, 1990 na 2014) huku Italia akifuatia kwa ushindi mara nne pia (1934, 1938, 1982 na 2006). Wengine walioshinda kombe la dunia Zaidi ya mara moja na miaka yao ni pamoja na:Argentina (1978,1986 na 2022); Uruguay mara mbili (1930 na 1950); pamoja na Ufaransa (1998 na 2018). Kombe pia liliwahi kunyakuliwa nan chi mbili za ulaya kila moja mara moja ikiwemo Uingereza (1966) na Hispania (2010). Katika orodha hiyo, nchi ya Afrika kuanzia Cairo mpaka Cape haijawahi kulibeba kombe hilo adhimu.

Cha kusikitisha Zaidi ni kwamba hata katika nafasi ya mshindi wa pili, Afrika haijawahi kutokea katika ramani ya FIFA kutokana na ukweli kuwa ili ifike hapo, Nchi hiyo ingepaswa iingie katika fainali. Kwa bahati mbaya, hakuna nchi iliwahi kucheza mechi ya fainali ya kombe la dunia katika miaka yote tangu 1930. Hii ndiyo sababu watu waliojaribu kubeza ushindi wa Morocco katika michuano ya kombe la Dunia Qatar mwaka 2022 walikuwa wana dhambi kubwa kwa Morocco na labda walifanya hivyo kwa kukosa uelewa wa historia ya michuano hiyo. Ukweli ni kwamba Morocco ndiyo nchi ya kwanza kufikia hatua ya nusu fainali za kombe la dunia tangu kuasisiwa kwa kombe hilo mwaka 1930.
IMG-20230208-WA0015.jpg

Je hilo ni jambo dogo kwa Morocco na kwa Afrika? Hatua pekee ambayo iliwahi kufikiwa na nchi chache za Afrika kwenye kombe la Dunia ni hatua ya makundi na robo fainali. Katika hatua ya robo fainali, ni nchi za Senegal, Cameroon na Ghana pekee ziliwahi kufikia. Hizo nazo zimeingia katika vitabu vya mataifa yenye soka bora duniani kwa hatua walizofikia katika kombe lenye ushindani mkubwa kama la FIFA. Morocco ni wa kupongezwa kwa kuvuka mstari uliowahi kufikiwa na Afrika!

Hata kuhusu miundombinu ya mchezo wa soka, FIFA inaikubali Morocco kama nchi inayonyanyua viwango vya soka barani Afrika. Tangu shirikisho la Soka la Morocco lianzishwe mwaka 1956, kazi imekuwa kazi kuhusu kuboresha mpira. Kwanza, Morocco ilijiunga na FIFA na CAF kufikia mwaka 1960. Shirikisho la soka nchini Morocco linahusika na kuandaa, kuratibu na kuongoza ligi ya soka kitaifa, ushiriki wa timu zake katika michuano barani Afrika, ligi inayoitwa batola na michuano ya kimataifa.

Tofauti na nchinyingiza Afrika, Morocco ina timu kali katika soka la wanaume na wanawake karibu katika viwango sawa. Uanachama mwingine wa Morocco ukiacha FIFA na CAF ni pamoja na Shirikisho la soka la Nchi za Kiarabu (UAFA) na pia mwanachama hai katika shirikisho la soka la Nchi za Afrika kaskazini likijumuisha: Algeria, Misri, Libya, Tunisia na Morocco yenyewe. Huko nako, Morocco imekuwa kinara wa kuwa mwenyeji wa michuano kadha wa kadha ya soka kwa sababu ya miundombinu bora.

Kwa ambaye hajawahi kufika eneo la kaskazini mwa Afrika, baadhi ya Nchi katika eneo hilo hazina miundombinu ya mchezo wa soka unaofikia viwango vya kimataifa.

Hiindiyo sababu hata mechi kadhaa kama ile ya Klabu ya Simba ya Tanzania na ASEC MIMOSAS ya Abidjan kwenye kombe la shirikisho ililazimika kuhamishiwa Benin katika uwanja wa Jenerali Mathew Kerekou baada ya Ivory Coast kukosa uwanja wenye viwango. Wale tuliosafiri na wekundu wa msimbazi kwa ajili ya mechi hiyo tunakumbuka jambo hili.

Ni kwa sababu hizo zote macho na masikio yangu yanaanza kuelekezwa Marekani, Mexico na Canada kwa ajili ya kufuatilia michuano ya kombe la Dunia la FIFA mwaka 2026. Kwa mara ya kwanza, kura ya kuandaa michuano ya kombe hilo imeelekea kwa ushirikiano wa Nchi tatu za Marekani ya Kaskazini: USA, Canada na Mexico. Hawa kwa umoja wao walishinda zabuni zote zilizowasilishwa kwa ajili ya maamuzi ya FIFA kuhusu mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia 2026. Ni kwa sababu hiyo, mgawanyo wa mechi jumla ya 80 zitakazochezwa kwa ajili ya kombe la dunia 2026 utakuwa ni katika nchi hizo tatu.

Kwa mpangilo uliopo, Marekani itakuwa mwenyeji wa mechi 60 ikiwa ni pamoja na mechi zote kuanzia robo fainali; Mechi kumi zitachezwa Mecicona kumi nyingine Canada. Kwa jinsi miundombinu ya soka ilivyo safi nchini Morocco na kwa usafiri wa moja kwa moja kutokea Casablanca hadi John F. Kennedy niliouona, nina uhakika timu nyingi zitapenda kwenda Morocco kujifua kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia itakapokaribia. Aidha, Morocco yenyewe itakuwa ikisubiriwa kwa hamu kuendeleza ubabe wake FIFA World Cup 2026 baada ya kuzikabili timu nyingi kali kule Qatar 2022 ikiwemo Ureno ambayo haikuamini macho yake kuwa imetolewa na ‘Afrika’katika hatua ya kuingia nusu fainali za kombe la Dunia 2022.

Naota ndoto kuwa miaka isiyo mingi kombe la Dunia litabebwa na Morocco kuelekea Afrika na kwamba kama hilo halitawezekana Marekani 2026 basi inshaallah mwaka 2030. Tayari nchi hiyo ina timu nzuri zenye ubora wa kimataifa zikiwemo: Wydad na Raja za Casablanca, FAR na FUS za Rabat, Hassania ya Agadir, KACM ya Marrakech, Ittihad ya Tanger, Maghreb ya FEZ, RSB ya Berkane na nyinginezo. Aidha timu ya taifa ya Atlas Lions (Simba wa Milima ya Atlas) ambayo inafundishwa na kocha maarufu barani Afrika na ambaye nilipata wasaa wa kuongea naye, Walid Regragui iko imara na inazidi kujifua kwa ajili ya michuano inayokuja kati ya sasa na AFCON 2025 na Kombe la dunia 2026.

Na kutokana na kiwango kizuri cha ualimu alichokionesha kocha Regragui kwenye fainali za FIFA mwaka jana, Shirikisho la Historia ya Soka Dunia (IFFHS) limempendekeza kuwania tuzo ya kocha bora wa soka la wanaume duniani 2022.Endapo ataibuka kidedea, kuna pesa nyingi tu inaweza ikalipwa kwa Morocco kuendeleza soka la nchi hiyo. Kwa uwekezaji, hamasa na maandalizi niliyoyaona Morocco, yamkini ndoto zangu ni za kweli!

Ni wajibu wetu Afrika kuiunga mkono Morocco katika harakati hizi za kututoa kimasomaso kwenye mchezo wa soka duniani. Kidiplomasia, naweza kushauri kuwa namna bora ya Tanzania kuunga mkono juhudi hizo na kuendeleza mahusiano ambayo tayari nchi hizi mbili zimeanzisha ni kwa Nchi yetu Tanzania kufungua ubalozi kamili Rabat ili kuongeza kasi ya mashirikiano.
Mungu Ibariki Afrika na watu wake wote!

Deus Kibamba Ni mtafiti Na mchambuzi wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Pia, ni Mhadhiri wa Masuala ya Diplomasia na Sheria za Kimataifa katika Chuo Cha Diplomasia, Kurasini, Dar es Salaam. Anapatikana kwa nambari: +255 788 758 581 na barua pepe: dkibamba1@gmail.com
 
Taifa stars vipi nasisi lini tunabeba world cup? Tuweke plan wakati ni Sasa!
Tuanze kuweka nyasi bandia viwanja vyetu!
 
Baada ya kulambishwa asali awamu iliyopita, zile kelele zote za kudai Katiba Mpya kupitia ile taasisi yako ya Jukwaa la Katiba, zimepotelea kusikojulikana!!
 
Na Deus M Kibamba

Baada ya kutembelea Morocco na kushuhudia hamasa ya Wananchi wa taifa hilo kwenye soka na miundombinu mizuri na ya kisasa waliyonayo, nimeanza kushawishika kuwa inawezekana Afrika ikanyakua Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2026 au 2030. Endapo utabiri wangu utatimia, sherehe za miaka 100 ya maisha ya kombe la dunia tangu kuasisiwa kwake zinaweza kufanyika Afrika na ninaweza kuhisi kuwa Morocco itakuwa mwenyeji wa sherehe hizo. Pia, kwa urafiki unaoendelea kukua kati ya Tanzania na Morocco, watanzania tunaweza kupewa heshima ya kuongoza itifaki yote ya shughuli yenyewe, Ishaallah !
View attachment 2511628
Kwa wasiokumbuka, kombe la dunia lilianza kushindaniwa mara tu baada ya kuanzishwa kwa shirikisho la soka Duniani (FIFA) mnamo mwaka 1930.

Tangu wakati huo, michuano ya kombe la dunia imefanyika kila baada ya miaka mine ispokuwa mwaka 1942 na 1946 kwa sababu ya Vita kuu ya pili ya Dunia. Kwa hakika, michuano ya kombe la Dunia ni mikubwa kuliko michuano yote duniani ikifuatiliwa na mamilioni ya wapenzi wa soka ulimwenguni. Wakati Fulani, idadi ya watu waliotazama mtanange wa kombe la dunia walikadiriwa kuwa ni Zaidi ya milioni 700.

Kwa bahati mbaya, Afrika haijawahi kufanikiwa kubeba kombe la FIFA kwa miaka yote 93 hadi leo. Mara zote, kombe limezunguka Ulaya, Marekani kusini na kwingineko.Kwa mfano, Nchi ya Uruguay ndiyo iliyokata utepe wa kulibeba kombe la dunia mwaka 1930 ikifuatiwa na Italia iliyoshinda kombe hilo mwaka 1934. Kwa miaka iliyofuatia baadhi ya nchi zilirudia kunyakua kombe hilo hadi mara tano kama Brazil (1958, 1962, 1970, 1994 na 2002).
View attachment 2511629
Pia, Ujerumani ni mshindi wa kombe la dunia mara nne (1954, 1974, 1990 na 2014) huku Italia akifuatia kwa ushindi mara nne pia (1934, 1938, 1982 na 2006). Wengine walioshinda kombe la dunia Zaidi ya mara moja na miaka yao ni pamoja na:Argentina (1978,1986 na 2022); Uruguay mara mbili (1930 na 1950); pamoja na Ufaransa (1998 na 2018). Kombe pia liliwahi kunyakuliwa nan chi mbili za ulaya kila moja mara moja ikiwemo Uingereza (1966) na Hispania (2010). Katika orodha hiyo, nchi ya Afrika kuanzia Cairo mpaka Cape haijawahi kulibeba kombe hilo adhimu.

Cha kusikitisha Zaidi ni kwamba hata katika nafasi ya mshindi wa pili, Afrika haijawahi kutokea katika ramani ya FIFA kutokana na ukweli kuwa ili ifike hapo, Nchi hiyo ingepaswa iingie katika fainali. Kwa bahati mbaya, hakuna nchi iliwahi kucheza mechi ya fainali ya kombe la dunia katika miaka yote tangu 1930. Hii ndiyo sababu watu waliojaribu kubeza ushindi wa Morocco katika michuano ya kombe la Dunia Qatar mwaka 2022 walikuwa wana dhambi kubwa kwa Morocco na labda walifanya hivyo kwa kukosa uelewa wa historia ya michuano hiyo. Ukweli ni kwamba Morocco ndiyo nchi ya kwanza kufikia hatua ya nusu fainali za kombe la dunia tangu kuasisiwa kwa kombe hilo mwaka 1930.
View attachment 2511630

Endelea kuota
 
Utabiri wangu.
Huu uzi utapotea ila 2026 utafukuliwa.
 
Back
Top Bottom