Hivi Lugha zote zimeanzia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Lugha zote zimeanzia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Annael, Jan 17, 2012.

 1. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,200
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikiangalia baadhi ya maneno kwenye mtandao na nimeshangaa sana kukuta baathi ya maneno karibia lugha zote za duniani huyatumia. mfano:-
  Mama karibia lugha zote duniani hulitumia neno hili na kumanisha mzazi wa kike.
  Kunabaadhi ya maneno menngine
  Mfano Baba kiswahili, Papa ligha ya kitoto kiingereza, Bhabha Kisukuma, kinyamwezi

  Vilevile Dad Neno la kitoto la kiigereza likimanisha mzazi wa kiume, dada Neno la kisukuma la kitoto likimanisha mzazi wa kiume.

  Nina uliza, hivi kati ya lugha hizi ni lugha ipi iliyotohoa neno kutoka kwa mwingune?
  Na kama hivyo lugha zote zimeanzia wapi?
   
 2. Makedha

  Makedha Senior Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeshawahi kusoma makala kuhusu asili ya maneno "baba" na "mama". Mwandishi alikuwa anahoji "m" ndio herufi ya alfabeti ambayo ni rahisi kushinda zote kuitamka, hata haja ya kufungua kinywa hakuna. Ndio maana aghalabu ni mojawapo wa herufi za kwanza mtoto atamkazo. "a" nayo ni mojawapo wa herufi hizo kwa sababu ya urahisi wa kuitamka.

  Sasa, sababu ya mama kuitwa "mama" ni kuwa mtoto huwa anakuwa anatamka sauti mbalimbali randomly ambazo kati ya hizo "ma" ni sauti irudiayo mara nyingi. Kwa hiyo, atumikaye muda mwingi zaidi kwa ajili ya malezi ya mtoto (ambao aghalabu ni mama yake) aliona mtoto often anaitamka sauti ya "ma" repetitively amwonapo, alifikiri ndio jinsi mtoto aliamua kumwita na mama naye alianza kujiita "mama". Hivyo, "mama" likakubaliwa kuwa jinsi mama anavyoitwa.

  Halikadhalika, mwandishi alifanya conclusion kwamba neno "baba" likafika kuwa jina la mtu wa mbili atumikaye muda mwingi na mtoto (ambao huwa ni baba yake) kwani sauti ya "b" utamkwaji wake nao ni rahisi sana (ukilinganishwa na sauti zingine za alfabeti) lakini si rahisi kama sauti ya "m" na "a".

  Sijui kama etymologists wengi wanakubali na hilio, lakini inaonekana kuwa nadharia yenye mantiki.
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wenyewe twaamini zilianzia Babeli
   
 4. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,200
  Trophy Points: 280
  Asante sana. Lakini je ninaweza kupata hicho kitabu ili na mimi nisome?
   
 5. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Katika hili la lugha ni zito sana, hamna uthibitisho wa kisayansi unaosema lugha ghani ilianza kwanza ama lugha gani inanguvu zaidi ya mwingine. Kanachochadiliwa na mapokea na maingiliana baadhi ya lugha mbalimbali. Kama wapare wanaweza kuongea kipare na wakaelewa kama ilivyo kwa wasukuma, waha, wazigua, wasumbwa, wamakonde! Hamna anayeweza sema ananguvu zaidi ya mwingine! Ila inapokuja sasa katika mawasiliano, elimu, na heshima kunabaadhi ya lught, kingereza kikiongoza ndio vimebeba nguvu kwa kujulikana na watu wengi - na kwa kutumika katika mifumo ya uzalishaji! lakini ukija na ungene wako ukaenda kumsemesha mtu ambaye hajui kingenge kunafaida gani!
   
 6. Makedha

  Makedha Senior Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Actually, haya makala nimeyapata hapa JF kwenye thread ya mwaka jana... Ungoje tafadhali, niitafute ile thread nikakuletea link (kama nikifanikiwa kuipata).

  EDIT:
  Turned out to be easier than I thought, here it is.
   
Loading...