Hivi lile shindano la #ChinaMade limeishia wap?

kokakola

Member
Nov 25, 2015
30
17
Siku chache zilizopita hapa JF liliwekwa shindano la ChinaMade ambalo nadhani ni kwa udhamini wa China radio international ikishirikiana na jamii media group.

Mimi sikushiriki kutokana na deadline ilinipita. Ila nilisoma stories za watu wote walio post hapa JF.
Kwangu Mimi moja ya stories zilizonivutia ni kama zifuatazo.

1: Kuna mtu aliweka stori kuwa alijifunza kusoma na kuandika kwa kutumia penseli zilizotengenezwa nchini China. ( Hii inatugusa wengi maana wengi wetu tangu chekechea penseli tulitumia. )

2: Kuna stori ya mtu ilikuwa ikielezea kwamba yeye ni online freelancer anafanya kazi na watu wa nje kwa kupitia mtandao. Kukatika katika kwa umeme kulikuwa kunaathiri kazi yake hivyo aliagiza power bank ya laptop ambayo ni bidhaa kutoka china ambayo ndo ilikuwa kwenye majaribio akasema ilimsaidia sana.

3: Kuna watu waliweka stories kwamba madawa ya kichina yaliwasaidia kutibu maradhi yao hasa maralia. ( kwa madawa napo wachina ni kiboko )

4: Kuna mtu aliweka stori kuhusiana na jinsi alivyonufaika kwa mashine ya kusaga kama sikosei maana yeye ni mtoto wa mkulima. Kutokana na mashine ile aliweza kusomeshwa hadi chuo kikuu na ana kazi yake.

Hizi ni baadhi tu kati ya stori nyingi zilizonivutia. Je wewe ipi ilikuvutia?
 
Naona unakumbushia cri international
 
Last edited by a moderator:
We acha tu kaka. Wangetoa muda wa kutosha nasie tungetupia stori zetu kama kawa.

Za namna mlivyosafirisha ngada na meno ya tembo kwenda
china bila ya kukamatwa kwa miaka kadhaa mpaka alipoingia JPM
dio ikawa mwisho wa janja yenu ya nyani.
 
Za namna mlivyosafirisha ngada na meno ya tembo kwenda
china bila ya kukamatwa kwa miaka kadhaa mpaka alipoingia JPM
dio ikawa mwisho wa janja yenu ya nyani.

He! Yamekuwa hayo mkuu. Hebu nenda duka la jirani kapate cocacola ya bariiiiiiiidi ukate kiu
 
Kwa upande wangu sijaona update yoyote aidha kutoka kwa JF au CRI. But from the look of things it seems hakuna kinachoendelea.
 
Habari zenu ndugu zangu? Wakubwa zangu shikamooni..

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 21 mwanafunzi wa chuo kikukuu cha dodoma mwaka wa kwanza nachukua masomo ya sayansi ya jamii. Wiki mbili zilizopita Radio china international walifungua thread yenye shindano la kiuandishi likitaka mshiriki aelezee chochote anachofahamu kuhusu utamaduni wa china mshindi atajishindia simu ya smartphone.

Mimi nilikua miongoni mwa washiriki katika shindano hili kinachonitatiza mbona mpaka leo matokeo ya washindi hayapo?? Nini ilikua dhamira yao kutuambia tushiriki??

Kama mshindi alipatikana kwanini akuwekwa wazi maana shindano lili husisha watu wengi kwa wakati mmoja?? Endapo mpaka sasa mshindi hakupatikana nitawezaje kufuatilia hili swala katika vyombo vya sheria???

Msaada tafadhali..

Anthony Daniel,
Mwanafunzi Chuo kikuu Dodoma..
 
Kuna hili shindano wadau tulishiriki kwa kuandika story zetu juu ya bidhaa za kichina kama mwezi mmoja uliopita ila mpaka sasa hatujapata habari za washindi.
 
Habari zenu ndugu zangu? Wakubwa zangu shikamooni..

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 21 mwanafunzi wa chuo kikukuu cha dodoma mwaka wa kwanza nachukua masomo ya sayansi ya jamii. Wiki mbili zilizopita Radio china international walifungua thread yenye shindano la kiuandishi likitaka mshiriki aelezee chochote anachofahamu kuhusu utamaduni wa china mshindi atajishindia simu ya smartphone.

Mimi nilikua miongoni mwa washiriki katika shindano hili kinachonitatiza mbona mpaka leo matokeo ya washindi hayapo?? Nini ilikua dhamira yao kutuambia tushiriki??

Kama mshindi alipatikana kwanini akuwekwa wazi maana shindano lili husisha watu wengi kwa wakati mmoja?? Endapo mpaka sasa mshindi hakupatikana nitawezaje kufuatilia hili swala katika vyombo vya sheria???

Msaada tafadhali..

Anthony Daniel,
Mwanafunzi Chuo kikuu Dodoma..
walishatangazaga washindi mkuu. Ila kutoa zawadi ndo bado
 
Back
Top Bottom