johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,004
- 142,038
Jaribu kufikiria, Waziri wa fedha anapeleka mswada wa Tozo ya mafuta bungeni na bunge zima linapitisha.
Baadae Waziri wa Nishati anatangaza kuziondoa Tozo hizo ili kuwapa wananchi unafuu wa bei lakini halihusishi bunge.
Wabunge wote wanapata taarifa kwa sababu wote wana magari ya mkopo na wananunua mafuta. Lakini hakuna mbunge hata mmoja aliyeshtuka kwamba utaratibu umekosewa.
Hata wale wabunge 25 wa upinzani yaani Chadema, ACT Wazalendo na CUF nao wakapiga kimya.
Hadi Rais ndio kaona kuna hayo mapungufu na kuirejesha.
Nchi ngumu hii na hili bunge la akina Babu Tale.
Enzi za Tundu Lisu hili lisingewezekana asilani, angempinga Waziri January pale pale anapotangaza kufuta Tozo.
Maendeleo hayana vyama!