Hivi kweli kinga ya wabunge ipo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kweli kinga ya wabunge ipo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Rula, Jun 7, 2011.

 1. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  WanaJF nimelazimika kuomba msaada kutokana na ufahamu mdogo wa kisheria juu ya kinga waliyonayo wabunge pindi wanapotuhumiwa kufanya makosa ya jinai au mengineneyo yatayowalazimu kufikishwa katika vyombo vya dola.
  Jana nilimsikia kamishna msaidizi wa polisi CP - Paul Chagonja akisema kuwa mbunge akifanya kosa lolote nje ya bunge basi atakamatwa kama mtu mwingine yoyote tena akatoa mfano wa mtaa maarufu kwa kuchoma kuku kule Dodoma ChakoChako kwa maelezo mbunge akinywa pombe na akampiga mtu basi pale pale anakatwa bila kujali visingizio kuwa yeye ni mbunge au nani! Source hapa ni TBC1 habari 20:00
  Katika kulifuatilia hilo nimesoma Mwananchi la leo nikakuta baadhi ya kipande cha habari hiyo kama ifuatavyo hapa chini;
  "......Chagonja na kuongeza:"Mbunge akitoka nje ya Ukumbi wa Bunge atapigwa pingu tu, maneno yanayosemwa kuwa mbunge ana kinga ni ya kutapatapa tu."
  "Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Peter Kivuyo alisema katika mafunzo ya jeshi hilo kuna aina moja tu ya kumkamata raia: "Ili kumkamata Rais wa nchi kuna taratibu zake, lakini watu wengine wanakamatwa kwa mujibu wa sheria zilizopo."
  Hapo ndipo ninapochanganyikiwa juu ya maelezo ya wanasiasa na wanasheria kuhusu ukamataji wa viongozi hususani wabunge kuwa ni lazima kibali kitoke kwa spika wa bunge. Ushahidi ni kauli ya Prof. Lipumba akimtuhumu spika kwa kukaa kimya juu ya udhalilishaji wa wabunge wa kambi ya upinzani, Tundu Lissu na G. Lema nimeshawahi kuwasikia wakisema kuhusu hiyo kinga.
  Sasa kutokana na sintofahamu hiyo yupi mkweli CP - Paul Chagonja au wanasiasa wanaodai wana kinga na sheria inasemaje kwa ujumla kuhusu hilo?
  Nawakilisha.

   
Loading...