Hivi kwanini watu wanapenda kutoa taarifa kwa kutisha?

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
50,282
70,688
Hivi kwanini watu wanapenda kutoa taarifa kwa kutisha, ili huyo mtu achanganyikiwe, akose raha, halafu anakupa habari nusu na ukimuuliza kuna nini hasemi ooh! Nitakutafuta tu.

Hawa watu huwa wana matatizo yaani huwezi ukanyoooka tu na kusema hivi na hivi ilikuwa hivi, mpaka uanze kumzungusha mtu kwanini usiseme hapo hapo au ukasubiri mkaonana ndio ukamuambia.

Kuna watu wana vitabia vya ajabu kabisa na vinakera.
 
kuna jirani yangu mmoja ni mvivu anakaa ghorofani atakuita wee miss natafuta miss natafuta unakuta umepumzika zako ndani ukitoka anakuuliza jamani unaenda dukani nikutume? kama ningekuwa naenda dukani si ungeniona nikitoka getini? anakera kweli jana nimemuambia asinizoee sili kwake silali kwake kama anajiona yeye ni bora ni kimpango wake
 
Mwingine umefua nguo zako ukaanika kambani,na yeye anakuja kufua na kuzikusanya nguo zako hata hazijakauka anaanika zake.

Au wale wanaanua nguo za wenzao hasa kanga,vitenge usipokitafuta imetoka hio.
wengine wanafua wakikuta vibanio vya wenzao kwenye kamba wanavitumia halafu wakianua nguo zao wanavichukua! wewe vibanio hujawai kununua sasa unachukua vya nini?
 
Kuna mwingine anakupigia simu wahi sehemu fulan utanikuta kuna bonge la ishu(unahisi dili la hela)unakurupuka kuwahi eneo husika(huku ulipotoka umeacha mambo yako kibao muhimu) kufika unamkuta amekaa hana wasi wasi wala nn eti eeh umewahi kuja nilitaka kampani tu.
 
kuna jirani yangu mmoja ni mvivu anakaa ghorofani atakuita wee miss natafuta miss natafuta unakuta umepumzika zako ndani ukitoka anakuuliza jamani unaenda dukani nikutume? kama ningekuwa naenda dukani si ungeniona nikitoka getini? anakera kweli jana nimemuambia asinizoee sili kwake silali kwake kama anajiona yeye ni bora ni kimpango wake
Jana si umeniambia nljua yameishia pale pale kumbe mwenzangu umeleta hadi huku. Sijapenda kwa kweli
 
Mwingine umefua nguo zako ukaanika kambani,na yeye anakuja kufua na kuzikusanya nguo zako hata hazijakauka anaanika zake.

Au wale wanaanua nguo za wenzao hasa kanga,vitenge usipokitafuta imetoka hio.
Hii hasa kama unaishi hostel
 
kuna jirani yangu mmoja ni mvivu anakaa ghorofani atakuita wee miss natafuta miss natafuta unakuta umepumzika zako ndani ukitoka anakuuliza jamani unaenda dukani nikutume? kama ningekuwa naenda dukani si ungeniona nikitoka getini? anakera kweli jana nimemuambia asinizoee sili kwake silali kwake kama anajiona yeye ni bora ni kimpango wake
Eti we miss natafuta miss natafuta utadhani jina lako kweli...
 
Back
Top Bottom