Hivi kwanini Watanzania tunapenda kulazimisha Undugu?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
WATANZANIA TUNAPENDA SANA KULAZIMISHA UNDUGU KUTAFUTA UPENDELEO! PAMOJA NA UNAFIKI!

Anaandika, Robert Heriel.

Ooh! Unajua wewe ndugu yangu!
Ooh! Sisi ni Kama Ndugu!
Oooh! Watanzania wote ni Ndugu!
Ooh! Wakristo wote ni Ndugu,
Ooh! Waislam Sisi ndugu!

Hivi wewe kabila gani? Ooh! Unajua sisi Watu kutoka Kusini ni Ndugu.
Unafiki Mtupu!

Sisi sio Ndugu bhana! Acheni Siasa!
Ogopa sana mtu anayeleta leta undugu! Undugu undugu ni mbaya Sana na umeharibu maisha ya watu wengi.
Unafiki! Kuviziana na kuchomana Kwa hao wanaojifanya ni ndugu zako ukiwa katika hali nzuri ni matokeo ya uhakika.

Ili ujue kile ninachokisema, na unielewe.
Ukiwa masikini na fukara hakuna atakayejinasibisha na wewe, hakuna hata mmoja atakayekuita Wewe ni ndugu yake.
Hakuna atakayejifanya anakujua, na Kama yupo basi huyo mshikilie Sana.

Wakati mwingine mpaka hawa wazazi wetu hawa, ukiwa katika kipindi kigumu baadhi Yao hata hawana habari na wewe.

Undugu gani huo wakati mtu akiwa katika Hali nzuri?
Undugu gani huo nikiwa Nina kazi yenye kipato?
Undugu gani huo nauliza!

Nikiwa masikini sio ndugu yenu, sivyo!
Nikiwa sina kazi sio ndugu yenu,
Mnasubiri nikiteuliwa au nikitusua kwenye michongo yangu ndio mnajilengesha lengesha.

Mnaleta kukutana! Ooh! Huyu nilisoma naye, byebyebye! Ona hata hii picha tulipiga wote. Tena ninyi mnamfahamu Kama Taikon lakini jina lake tulikuwa tukimuita KIBERENGE Enzi hizo akicheza namba Saba. Pumbavu wewe! Trooka!

Yesu aliwahi kulitolea hili maelezo,

Mathayo 12:47
Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.

Mathayo 12:48

Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?

Mathayo 12:49

Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!

Mathayo 12:50

Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

Mmemsikia Yesu Huyo!

Ndugu zako ni Wale ambao wapo na wewe katika nyakati zote, wanaokusikiliza katika shida zako, mnaoshirikiana nyakati za taabu na nyakati nzuri.

Kuzaliwa pamoja siku hizi sio ishu kubwa, kuzaa mtoto sio ishu kubwa hata Panya anazaa. Mimi Taikon ni mwanaume, Kama Baba siwezi leta Ubaba Kwa mtoto ambaye sikuwajibika ati Kwa kigezo cha kuwa nilimzaa.

Oooh! Nina kakaangu sijui Dadaangu sijui mjomba hanisapoti, kwani unaye huyohuyo pekee yake, hao wengine ulionao wanakusapoti?

Kama hawakusapoti Jisapoti mwenyewe. Assume walishakufa miaka mingi huko. Sasa tangu lini mtu mwenye akili akategemea msaada Kwa Maiti zilizokwisha kufa.

Usipende kutegemea watu. Mtu ni maiti inayotembea. Ndio maana vitabu vinasema Ole wake amtegemeaye Mwanadamu.

Taikon msimamo wangu, na ndivyo nilivyo. Na napenda kuwarithisha wale wote mnaotaka kuwa na furaha na Amani, kuwa; usipende kulazimisha Undugu!

Mtu Kama Hana time na wewe achana Naye. Kwani yeye Nani. Ishi maisha yako vile utakavyojaliwa. Mimi huwaga na-assume walishakufa. Nawe fanya hivyo utakuja kunishukuru baadaye.

Sio kujinyenyekeza kisa upumbavu, kulamba watu miguu na kusujudu kisa upuuzi.

Kama mtu haoni umuhimu wako iweje wewe uone umuhimu wake, huko ni kutokujitambua na kujidhalilisha. Kuwa hodari na moyo wa ushujaa.

SIO LAZIMA UFANIKIWE!
Zingatia mafanikio hayaji Kwa kujipendekeza Kwa watu na kushusha thamani yako. Utakuwa mtumwa miaka nenda Rudi Fala wewe.

Unalazimisha undugu ili uwe mvivu. Usifanye kazi!
Unalazimisha undugu ili usiafhibiwe pale unapokosea.
Unalazimisha undugu ili upewe misamaha kilazima.
Unalazimisha undugu ili ukitia hasara kwenye biashara usichukuliwe hatua.

Unalazimisha Undugu ili ukae Kwa Shemeji Ile ugali wa bure licha ya umri wa kujitegemea umefika. Come on! Acha upuuzi!

Sisi Kama Hustlers tutapambana Kama Wanaume mpaka tone letu la mwisho la Uhai wetu. Hatutayaogopa matokeo ilimradi tunapambana Kwa nguvu zetu zote, Kwa akili zetu zote, Kwa mioyo yetu yote.
Hatuiogopi kesho yetu Kwa sababu kesho yetu haijashikwa na watu isipokuwa aliyetuleta Duniani..

Wengi wanaogopa kesho Yao Kwa sababu ya kujipendekeza Kwa watu.
Ooh! Naogopa sitazikwa!
Naogopa uzee wangu watoto sijui mke sijui mume au ndugu zangu wanaweza kunitenga. Akili za kijingajinga tuu!
Utatengwa tuu ikiwa unajipendekeza Kwa watu wasioona umuhimu wako. Nyau wewe!

Mnizike msinizike mtajua wenyewe! Taikon hataacha kufanya wajibu wake kisa kuogopa kutokuzikwa. Never!
Yaani hamuoni umuhimu wangu, Mimi nione umuhimu wenu! Labda sio Mimi, hata nikilogwa siwezi kuona umuhimu wa mtu asiyeona umuhimu wangu dunia ingalipo Mimi nikiwepo.
Mimi napenda HAKI. Na ukweli. Na hivyo ndivyo vinanipa Amani na furaha.

Mnafiki nitampa unafiki.
Mkweli nitampa ukweli.
Anipaye undugu nitampa undugu.
Anipaye upendo nitampa upendo.
Anipaye Chuki nitampa Chuki.
Usiponiheshimu Kwa Hali yangu, sitokuheshimu Kwa Hali yako.

Masuala ya kubembelezana sinaga.
Nafahamu Wabaya huomba mabaya yanipate ili wapate nafasi,😂😂 lakini hilo halitageuza chochote katika kile nilichoandika, hivyo ndivyo ilivyo.
Nafahamu saikolojia ya mwanadamu jinsi ifanyavyo kazi. Hivyo kila neno nilipoandika nimelipima na najua Hesabu yake.

Vijana, pengine nimeandika mengi Sana. Lakini kama unataka kuishi Kwa amani na furaha basi mpe mtu haki yake.

Usije ukadhani kupewa msaada na mtu asiyekuheshimu basi msaada huo utakusaidia. Hasha! Msaada huo utazidisha machungu katika moyo wako, katika maisha yako. Na pengine ikawa ni mwiba katika kizazi chako.
Usijesema utapuuzia, au utavumilia. Hizo ni Akili za mtu ambaye hajakomaa.

Biblia inasema;

Mhubiri 4:6
Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo.

Mithali 15:16

Kuwa na mali chache pamoja na kumcha BWANA; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.

Mithali 15:17

Chakula cha mboga penye mapendano; Ni bora kuliko ng’ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.

Usipende kulazimisha mambo!

Taikon nimemaliza! Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Lkn ukiwa nazo watakuja tu! ......utawafanyaje? kwa mfano unaenda kazini unakuta kuna watu kama kumi hiivi kutoka kijijini wamekuja Mjini nyumbani kwako kama Mugumu town!

wakitokea Issenye mjini na kule issenye ni mbali hawawezi kurudi faster!! ...hadi Bus la kesho asubuhi!...ivo wakikaaa tena siku km tatu hivi wengine haoooo!...sasa mkuu utawafanyaje hapo?

yaani ukiwa na pesa bana na mjumba wa maana heee!! Mbona utakoma??? yaani wanakuja kwa timingi za hali ya juu kweli kweli!! mtoto wa mjomba mara binamu mara shemeji zako..duuuu !!

yaani labda ushike panga usimame mlangoni lkn kazi utafanya saa ngapi??...hata wengine wanakuja kuuguza wagonjwa mfano kalazwa MNH sasa hao! wametoka mkoa si watafikia kwako tu ili mradi tu wanakujua!!

yaani wee acha tu sasa je utamfukuza shemeji yako??......watakusema hukoooo! heee mpaka ulie poo! bora wale ambao hamjakulia vijijini!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom