Hivi kwanini wanyama hawashindi nje ya temeke?!!

Hivi kwanini wanyama hawashindi nje ya temeke?!!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,153
Wekundu hao wa Msimbazi,simba a.k.a. wanyama wanadai safari hii wamepania kushinda mechi ya kwanza nje ya Dar es Salaam,dhidi ya mtibwa sugar kesho jumapili huko morogoro kwenye uwanja wa jamhuri baada ya awali kutoa sare katika mechi zake zote za ugenini.Kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Simba ilitoka sare za bila kufungana na wenyeji Coastal Union na Mgambo JKT kabla ya juzi kufungana 1-1 na Polisi, tena yenyewe ndio ikihaha hadi kipindi cha pili kukomboa bao, baada ya Mokili Rambo kutangulia kuwafungia Maafande hao kipindi cha kwanza.

Wakati wanyama (simba)wakidai hivyo upande wa pili Yanga kupitia kwa kiungo wao mkabaji Athuman idd "Chuji" wamesema kwamba mechi yao ya Jumapili dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itakuwa ngumu, lakini watapigana kwa nguvu zao zote washinde ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Chuji anasema kwamba Azam ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri, hususan katika nafasi ya kiungo, hivyo wanatarajia upinzani mkali siku hiyo."Azam wazuri, wana viungo vizuri na mbaya zaidi wanapokuwa wanacheza na sisi wanakomaa zaidi, wazi mchezo utakuwa mgumu,"alisema mtoto huyo wa winga wa zamani wa CDA ya Dodoma, Iddi Athumani na kaka wa mshambuliaji wa Coastal, Pius Kisambale.
Amesema anatarajia upinzani mkali kutoka viungo wa Azam kama Salum Abubakar ‘Sure Boy', lakini watakabiliana nao na watawaonyesha kwamba Yanga ni zaidi.
"Tumepigana sana hadi kufika hapa, tulianza ligi vibaya, sasa hivi tunataka kuiacha mbali kabisa Simba, kwa hivyo tumedhamiria sana kuwafunga Azam Jumapili,"alisema Chuji.
Akiizungumzia Ligi Kuu kwa ujumla, Chuji alisema ni ngumu na wanashukuru wao walianzia mechi ngumu zaidi za mikoani ambako walipokuwa wanapata matokeo mabaya wengi waliwadharau na kuwakebehi.
"Sisi tumetoa droo na Prisons, tumefungwa na Mtibwa na Kagera tukachekwa sana, sasa na wenzetu (Simba) wameenda mikoa miwili tu, lakini sasa tunalingana pointi, kiko wapi sasa walichokuwa wanatucheka, hao hawajaenda Kanda ya Ziwa, hawajaenda Arusha, hawajaenda Mbeya, unategemea nini?"alisema Chuji.

Swali langu ni kwanini simba imekua ikishinda temeke tu?????je itaweza kutuwakilisha vyema kimataifa kweli???

 
Kwani Mtibwa alimfanya nini Yanga???? Kama unalijua hilo mechi ya kesho siyo ya kuisemea kirahisi namna hiyo eti mnyama hashind nje ya Temeke!!!
 
Kwani Mtibwa alimfanya nini Yanga???? Kama unalijua hilo mechi ya kesho siyo ya kuisemea kirahisi namna hiyo eti mnyama hashind nje ya Temeke!!!
Ni kweli hata wewe ukitulia na kutazama sawasawa utaona kwamba jamaa mechi zote walizoshinda wameshindia pale temeke
 
Lakini sidhani kama ni tatizo wapi unashinda, pointi ndo muhimu. Mpaka sasa Mnyama yuko juu. Tukisema maamuzi (km juzi mpira morogoro ulisimama kwa takribani kumi), hazikuongezwa, ubaya wa viwanja (zingatia mpira wa chini wa Simba), hatutakosea ila tu TUTABISHIWA. We jitoe ufahamu na kufananisha michuano ya kimataifa na ligi. Kwenye hiyo michuano ya kimataifa, ukishinda nyumbani mfano, temeke ukashinda 2 ugenini ukafungwa 1, inakuwaje?! Nyumbani ni nyumbani, sioni tatizo mpaka sasa
 
Ni kweli hata wewe ukitulia na kutazama sawasawa utaona kwamba jamaa mechi zote walizoshinda wameshindia pale temeke
Hata msimu uliopita tulikuwa tunashinda Temeke tu, mechi za mikoani zote tulifungwa, asavali msimu huu tumetoatoa droo zitatusaidia kutetea ubingwa.
 
Basi na wazee wa mzungu wa 4 wanabebwa taifa maana naye rekodi yake ya mikoani siyo nzuri, tena yeye ni vipigo kabisa
lakini wao angalau wameshinda na kufungwa sasa wanyama mwanangu kwanza walianza kwa kishindo,mechi tano mfululizo(haijapata kutokea popote duniani)nyumbani wakashinda zote,wakajizolea sifa nyingi,lakini walipoanza kutoka tu,mapungufu yakaanza kuonekana,mara nyingi wamekua wakihaha kukomboa mabao wao ili wapate droo!
 
kwanza acha uongo...simba hakuhaha ...alitawala hiyo mecchi sema tuu ni uzembe wa okwi ndio uliowafanya wapoteze point. pili wao ndio timu pejee iliyocheza mpira katika kiwanja cha jamhuri. wengine wote wamekuwa wakikalamika kuwa uwanja mbovu kumbe hamna lolote....pata data kamili hapa trequatista | Wix.com
 
662_333198656777791_1333080479_n.jpg
 
.....ngoja mechi na Mtibwa imalizike, ndo mtaisoma Simba kwa jinsi inavyotisha.
 
Basi na wazee wa mzungu wa 4 wanabebwa taifa maana naye rekodi yake ya mikoani siyo nzuri, tena yeye ni vipigo kabisa

we maharage skuizi umefuria hadi unamua kuhonga wandishi wa habari pole sana
 
Jamani hili swali langu bado halijata majawabu,wanashida gani hawa watu wakitoka nje ya temeke???!!!yani point zao ni za temeke tu?
 
Back
Top Bottom