Hivi kwanini wanyama hawashindi nje ya temeke?!!

Hivi kwanini wanyama hawashindi nje ya temeke?!!

Ngoja Mkuu Masuke apunguze Machungu naamini atakuja na jibu,jamaa huwa anachambua matatizo ya team yake ki'taaluma sana,namkubali sana jembe langu Masuke
 
Last edited by a moderator:
wanyama kulikoni tena,now hata temeke napo pagumu?????????????
 
wanyama kulikoni tena,now hata temeke napo pagumu?????????????

SIMBA SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Oljoro ya Arusha, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa jioni hii.
Hiyo inakuwa sare ya pili mfululizo wa mabingwa hao watetezi, baada ya wiki iliyopita kulazimishwa sare kama hiyo na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo, yanaifanya Simba itimize pointi 28, baada ya kucheza mechi 16, hivyo kuzidi kuliweka rehani taji lake la ubingwa, kwani wapinzani wao wa jadi, Yanga wanaongoza kwa pointi 33 na mchezo mmoja mkononi, wakati Azam FC ya pili kwa pointi 30 na mchezo mmoja mkononi pia.
 
simba ni la kuvunda,halinaga ubani hilo,na libolo nasikia limeingia kimya kimya bongo bila wanyama kujua,limejichimbia masaki tayari kwa kumshughulikia mnyama
 
Teh! naona na jana wameishia na droo huko Chugga...mwenyekiti wao yupo capital city huko anagombea bendera ya Yanga iwekwe mwembeni...
 
Wamechezesha kikosi B ili wasi underperform kwa LIBORO, siunajua wakioneshwa burudani safi wanaweza kutoa hela ndefu.
 
Ndo zao, na ukiona hivi ujue vipigo vinakuja ksbb hata duru la kwanza walianza kwa droo kisha wakaja kupokea vipigo,ni kawaida kwa Mnyama labda kipindi hiki waokolewe na ujio wa Tajiri wao MUNGU mtu wao Malkia wa Nyuki.
 
Jamani hili swali langu bado halijata majawabu,wanashida gani hawa watu wakitoka nje ya temeke???!!!yani point zao ni za temeke tu?
jibu lake ni kwamba yanga na simba zote hazijui mpira zaidi ya fitina na kuhonga
 
Teh! naona na jana wameishia na droo huko Chugga...mwenyekiti wao yupo capital city huko anagombea bendera ya Yanga iwekwe mwembeni...
Ha haaa haaaa..............

12025_247562755379920_1954944451_n.jpg
 
Back
Top Bottom