nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 11,726
- 12,006
Unapoamka asubuhi mpaka unapofika jioni muda wa kulala,uliyoyafanya ni sawa kwa utashi wako au kuna kingine ambacho unatakiwa ukifanye wewe kama wewe lakini mazingira yana kuzuia?
Je, wajua ile sauti unayozungumza nayo(kimoyomoyo) ni nani hasa unayezungumza nae?
Sababu ya wewe kuwepo/kuishi ni ipi?
Unapokuwa uzingizini ukaota ndoto,wale usiowafahamu ndotoni ni kina nani hasa?
Macho yako yanapoiona kijani,una uhakika na wengine huiona kijani hiyo hiyo? au toka ukiwa mdogo ulifundishwa hiyo ni kijani na mimi ninajua kweli ni kijani lakini ubongo wangu unaona ni blue lakini naiita kijani na wewe ubongo wako unaiona ni red lakini waiita kijani.(hapa wachache mtanielewa)
''And Why life is taken in a sudden shock''