Hivi kwanini Serikali isiajiri wahitimu wote kama wanavyoajiri walimu na kada zingine za afya bila interview?

Tatizo kubwa vijana waliomaliza vyuo wanapenda kubet, kubishania soka.
Hawana kipato. Wakati mwingine tuwaelewe tu. Mtu ana elfu tatu ya kutumia wiki nzima na hajui ikiisha atapata wapi ingine anajikuta bora ajaribu kuweka 1000 kwenye kamari.
Sasa unakuta mtu anaomba kazi TRA hajui hata mambo yahusuyo TRA au jinsi alichosomea kinavyohusiana na kazi ya taasisi, wizara au mamlaka anayoomba kazi. Lazima kila interview afeli hawezi kutoboa
Upo sawa, Kwa Huyu aliyeitwa kwenye interview anatakiwa kuchunguza yale mambo ya kawaida kabla hajaenda kwenye interview
Kuna mambo hautafundishwa chuoni unatakiwa ujiongeze. Utakuta ambaye hajasomea mambo ya business lakini mfuatiliaji wa mambo ya uchumi ana ufahamu mkubwa kuliko aliyosomea course za B.com chuoni
Mkuu kijana mwenye 35yrs asiye na kipato, hana mtaji, atasoma kweli sera za biashara? Kwa utulivu upi wa akili? Ukivaa viatu vyake wakati mwingine unamwelewa. Kuna umri ukifika huna kipato na umesoma unapata changamoto ya afya ya akili. Serikali inapaswa kutazama hili. Hawa vijana wenye 30+ wasio na kazi na wamesoma ni wa kuwatazama kwa jicho la kipekee.
Hizi mbanga ndizo zinazowafanya wengi wafeli mitihani ya bodi ya NBAA ya CPA
Mambo si magumu sana boss ila Wamekuwa wengi sana ndo maana bodi zinadhibiti kwa mbinu mbalimbali ikiwemo mitihani migumu. Mkishakuwa wengi mnakosa thamani. CPA zimekuwa nyingi na kazi hakuna.
 
Ungekua na kampuni yako unaweza muajiri mtu bila kujua au kupima uwezo wake?

Serikali haitufahamu kama tunavyojuana mtaani lazima kuwepo na kipimo sahihi kwa watu wote.

Pia lazima ukubali kwamba idadi ya wahitimu ni kubwa kuliko nafasi zikizopo hawawezi ajili wote ko lazima ifanyije fair competition platform
Mbona tamisemi hawafanyi hizo interview
 
Sector binafsi hawaangalii interview tuu ndo waajiri wanaangalia vitu vingi
Age
Appearance
Experience
Language
Skills

Tofauti na serikali ambapo wangeweza kupunguza mrundikano wa jobless Kwa kuwapa training halaf wawekwe kwenye database wawe wanaajiriwa kutokana na uhitaji
Sasa hivi vinaangaliwa wapi kama sio kwenye interview?

Labda ni huko serikali tunachoweza kukosoa ni process nzima ya interview na requitment, haimpi room mtafuta kazi kuonesha uwezo wake katika kazi husika. (Sijawahi kufanya hata moja ila huwa wanasema mara mnafokewa sijui mnakimbizwa kimbizwa, ni namna gani mtu atafanya vyema kwa mazingira hayo akiwa hayuko calm?)

Interviews, tukiziweka pembeni zile za majeshi na vyombo vya ulinzi na usalama, zingine hizi zinatakiwa kuwa comfortable, strictly and yet friendly.

Anyways Interviews ni crucial ndugu, kwa sisi wengine kuna muda tunafanya for fun tu tuone kama bado tuna uwezo wa kupambana sokoni …..

Labda tuzungumze, tatizo lako na interview ninini? Una anykind of speech disorder?
 
Walimu ni Special Group kwanza inabidi ujue idadi ya watumishi wote wa serikali walimu wanafika hata 50% so karibu nusu ya watumishi wote moja.

Mbili uwalimu hauna specialization yaani unapoona kwenye chuo kikuu Kama UDSM, UDOM Kuna college kwaajiri ya walimu tu mfano DUCE, MKWAWA, COED yaani hio college wanafunzi wooote Ni walimu no specialization yes kozi zao zina majina tofauti mfano Bed Sped, Bed PPM, Bed Pschology nk ila all in all wooote Ni walimu zikitolewa nafasi za walimu wanaomba wote Kama walimu so ni wengi Sana walimu tu, mfano serikali ikisema imetoa mafasi 10,000 ya ajira za walimu waombaji wakawa 100,000 hao lakimoja wote Ni walimu hawana makandokando tofauti na kada zingine mfano ukisikia IFM, TIA ,AII, CBE kwenye hivyo vyuo sio wote ACCOUNTS ni watu kozi tofautitofauti sana.

Kingine sehemu za kazi wanapoajiriwa walimu ni special place ambapo ni shuleni, shule zipo nyingi saan yaani nyingi na mpaka Sasa kwenye hizo shule idadi ya walimu bado ijaweza kufikia idadi ya shule Kuna Report imetoka mwaka huu iliandika "Idadi ya walimu wanaohitajika mashuleni hata ukiajiri walimu wote walio mtaani bado tu uhitaji haufikiwi" so hawaajiriwi wote kwasababu ya serikali haina pesa.

Walimu ni special group, elimu Ni special sector, shule ni special institute ndio maana uwalimu ukaitwa wito lazima uwe na mass employment.

Huezi kuwa na mass employment kwa Accountant wapo wangapi, wanaajiriwa wapi hawana data iliyo clear hawana sehemu special wanayoajiriwa hawana ofisi maalum ila walimu Ni shuleni na shule ni nyingi, madakatari hospital na hospital ni nyingi.

All in all ilibidi ujue haya kabla ujachagua kozi ya kusoma chuoni
 
Mkuu kijana mwenye 35yrs asiye na kipato, hana mtaji, atasoma kweli sera za biashara? Kwa utulivu upi wa akili? Ukivaa viatu vyake wakati mwingine unamwelewa. Kuna umri ukifika huna kipato na umesoma unapata changamoto ya afya ya akili. Serikali inapaswa kutazama hili. Hawa vijana wenye 30+ wasio na kazi na wamesoma ni wa kuwatazama kwa jicho la kipekee.
Kama anapata muda wa kuingia kwenye mitandao kupost, kulike, kucomment na kusoma anakosaje muda wa kuongeza maarifa?
 
Mambo si magumu sana boss ila Wamekuwa wengi sana ndo maana bodi zinadhibiti kwa mbinu mbalimbali ikiwemo mitihani migumu. Mkishakuwa wengi mnakosa thamani. CPA zimekuwa nyingi na kazi hakuna.
Ni sawa unachosema ila wengi wanastahili walichoscore
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Dogo anataka akabidhiwe ofisi kienyeji afanye yake
Hawa vijana wanyoa viduku uwakabidhi ofc bila kuwahoji ni big no
Japo sijawai kunyoa kiduku na sitarajii kunyoa Niku challenge kiduku sio Tatizo...tatizo lipo Kwa mtu mwenyewe mfano atokee Mtu aseme Hawa wavaa baragashia wasipewe office unaona eee

Interview ni muhimu na ni lazima ila huko serikalini niliwai shangaa Huyu mtu bogus ivi UELEWA NA LOGIC ndogo alipitaje interview ikiwa tu hata hajielewi haupati majibu nikaja gundua Kuna wanao ajiliwa Kwa MEMO📝
 
Sasa hivi vinaangaliwa wapi kama sio kwenye interview?

Labda ni huko serikali tunachoweza kukosoa ni process nzima ya interview na requitment, haimpi room mtafuta kazi kuonesha uwezo wake katika kazi husika. (Sijawahi kufanya hata moja ila huwa wanasema mara mnafokewa sijui mnakimbizwa kimbizwa, ni namna gani mtu atafanya vyema kwa mazingira hayo akiwa hayuko calm?)

Interviews, tukiziweka pembeni zile za majeshi na vyombo vya ulinzi na usalama, zingine hizi zinatakiwa kuwa comfortable, strictly and yet friendly.

Anyways Interviews ni crucial ndugu, kwa sisi wengine kuna muda tunafanya for fun tu tuone kama bado tuna uwezo wa kupambana sokoni …..

Labda tuzungumze, tatizo lako na interview ninini? Una anykind of speech disorder?
Sina tatizo lakini naona mfumo ubadilike maana watu wengi ni watendaji wazuri interview zinawafelisha
 
Back
Top Bottom