Hivi kwanini Kanisa lisiruhusu waumini kuoa mke zaidi ya mmoja? Sioni sababu ya kukataza

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Wakuu ni kwanini tu kanisa lisiruhusu waumini kuoa mke zaidi ya mmoja? Maana kusema kweli watu wengi wanaishia kuwa na vimada wengi nje ya ndoa.

Sio hayo tu, kwa taratibu za ndoa za kikristo ni kuwa hakuna kuachana labda kifo kiwatenganishe, means kuna watu wanateseka mno kwenye ndoa ishu ya talaka ni mwiba nzito mno usioruhusiwa.

Nina marafiki kadhaa ndoa zimekua mzigo kwao, hawana machaguo, mtu anapitia mateso makali sana na ukizingatia ndio hakuna kuachana jamaa wanapigwa na msongo mkali sana wa mawazo.

Mwingine anawaza watoto wake itakuaje, anatamani walau dini ingeruhusu mke zaidi ya mmoja ajiongezee bi mdogo ili walau tu ajue atamanage vipi mambo.

Nasema haya kwasababu sioni sababu yoyote ya kuendelea kuzuia watu kuwa na mke zaidi ya mmoja kihalali kwa ndoa, ukisema eti ni dhambi.

Sioni sababu ya kuzuia mapadri wasioe kwasababu ya kutafuta utakatifu, lakini unakuta hao hao mapadri wengi wanapitia magumu mengi kihisia na wengi unakuta wana familia kisirisiri.

Mwisho, haya mambo ya kidunia ya huko Ulaya, dini kuruhusu hadi ndoa za jinsia moja kufungwa kwanini wasiruhusu tu mtu kuoa?

Kama wanaweza kuruhusu ndoa za wanaume kwa wanaume wanashindwa vipi kuruhusu mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja?Wanashindwa vipi kuruhusu mapadri kuoa?

Nawasilisha.
 
Sipo kidini, mtazamo wangu tu, huwa sishangai nikiona mwanamke akipinga ndoa ya Mke zaidi ya mmoja, kwasababu kimsingi wanawivu Na huo wivu wao ndio ukamilifu wa mapenzi(mahaba) Na ukiona mkeo hakuonei wivu basi kuna tatizo hapo....

Ila huwa nashangaa hadi nakosa jibu na kuamua kukaa kimya kibisa pale ninapomuona mwanaume anapinga ndoa zaidi ya Mke mmoja

Only few men (say 5%) wanaweza kukinaika na Mke mmoja, wanaume wenzangu ili tunalijua wala sihitaji majibu kutoka kwenu wala sihitaji lijadiliwe hapa wala sihitaji kuwalazimisha wanawake kuliamini
 
Mzee ndoa sio kuteseka inahitaji uvumilivu kuachana ni hatari...Hata waislamu Kuna talaka ila unaambiwa ile kutoa talaka mbingu na ardhi zinatikisika yaani sio jambo zuri kabisa, ila kama mmeshindwana kabisa Bora kutengana.
 
Hayo ndio madhara ya kukimbilia kwenye Mila na desturi zisizoendana na utamaduni wetu. Wenye hizo tamaduni za mke mmoja sasa hivi wanatuambia ni sawa kwa watu wa jinsia moja kuoana lakini sio sawa kwa mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja, hawa pia ndio wanatuambia kuna motoni na peponi. Akili kichwani mwako, za kuambiwa changanya na zako
 
Mkuu mbona umepungukiwa hekima? Unajua hata maana ya Kanisa? Niambie ni Kanisa lipi lililozuia watu kuoa wake wengi? Je, hao marafiki zako ndio kipimo cha imani ya Kikristo?

Fahamu kwamba Ukristo ni zaidi ya kujiita Mkristo.

Mathayo 7
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹³ Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
¹⁴ Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.


Hao rafiki zako ni genge la wahuni
 
Wewe ni mkristu au ni Muslim?
Kama ni mkristu mpaka hapo ulipo huna mafundisho ya dini

Ila tuachana na hayo kwanza vipi yule mdudu roast unatumia?😬
 
Weledi wa mambo ya dini naomba mnifumbue mamcho, hivi kuna andikoo lolote kutoka kwenye BIBLIA linalokataza mwanaumebwa kikristo kuoa zaidi ya mke mmoja??

Au ni kujinyima tu??
Kwani dini ya kikuristo kwenye bibulia iko wapi? Tafadhari ni onyeshe kama hiyo dini ilitajwa popote kwenye Bibulia
 
Wewe ni mkristu au ni Muslim?
Kama ni mkristu mpaka hapo ulipo huna mafundisho ya dini

Ila tuachana na hayo kwanza vipi yule mdudu roast unatumia?
Baada ya dhihaka bila shaka nafsi imetulizana.
Sasa Mpe andiko kama alivyoomba.
 
hata la padiri kutooa halimo
Una uhakika na unachosema. Ila sio shida maana ni tabia ya wabongo kuongea bila kuwa na uthibitisho.
Mathayo 19: 12
"Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: Wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.”
 
Back
Top Bottom