Hivi kwanini Burundi watuzidi watanzania?

Hivi kwanini Burundi watuzidi watanzania?

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
19,371
Reaction score
14,515
Wakuu mliobobea kwenye Masuala ya Uchumi Naomba mnisaidie hapa.Sote tunafahamu kuwa thamani ya Shilingi yetu imeshuka kwa kasi sana.

Wataalam mbalimbali wametoa sababu kadhaa Ikiwa ni pamoja na Kuingiza zaidi bidhaa za nje kuliko sisi kuzipeleka nje bidhaa zetu.

Pamoja na sababu mbalimbali;Swali langu ni hivi Juzi nilikuwa Burundi pale mpakani Pesa yetu ipo chini wakati Faranga ya Burundi ipo juu,sasa kwanini inakuwa hivyo wakati nchi yao ipo kwenye Machafuko hivyo hawazalishi?

Aidha wale jamaa tumewazidi ki-viwanda yaani karibia asilimia tisini ya vitu vya viwandani vinatokea kwetu,Kwenye upande wa Chakula ndio usiseme,yaani mimi ninashangaa kwanini Faranga yao ipo juu wakati wao tunawazidi kwa kila kitu?,

Siku nimeenda walikuwa wana-chenji Shilingi mia kwa Faranga 92,

Nawasilisha wakuu.
 
Mkuu nilikuwa bujumbura siku mbili zilizopita nilishtuka pale kabanga mpakani wakati nachange hela wanani faranga 900 kwa buku la bongo nikabaki na maswali lukuki hebu ngoja waje wataalamu waseme
 
Mkuu nilikuwa bujumbura siku mbili zilizopita nilishtuka pale kabanga mpakani wakati nachange hela wanani faranga 900 kwa buku la bongo nikabaki na maswali lukuki hebu ngoja waje wataalamu waseme

Wewe shahidi yangu,ningesema peke yangu wangesema mimi mwongo,afadhari na wewe ulijionea,sasa kale ka nchi kana-import vitu vingi kutoka kwetu sasa sijui ni kwanini wanatuzidi,hebu jamaa watusaidie.
 
Serikali inachapisha pesa hewa ili kulipana nyongeza za mishahara na posho. simple!
 
mtoa mada, naomba nisaidie, dola moja ya marekani ni sawa na kiasi gan hela ya burundi, tutumie kipimo cha kimataifa(daollar). nadhani tutaelewa zaid
 
Bila kupatikana mtu mwaminifu shilingi itapotea duniani
 
Nadhani wachumi wanaweza kutusaidia lakini sidhani kama wanatuzidi kiuchumi sababu nilikuwa Lusaka Zambia sasa hivi kwacha ya Zambia in strong kuliko South African rand kwa asilimia 100% yaani ukitoa Rand 100 unapewa Z-kwacha 50
Sasa basi kiuchumi Zambia ukilinganisha na south Africa Zambia bado sana
Wachumi please njooni mtufafanulie
 
Hii kwa muono wangu,
Wakati mwingine huwa hujuma vile, ili wanunue vitu kutoka nchi husika kwa bei rahisi zaidi.
Nafikiri na kinacho decide zaidi ni ile uwezo wako wa kuwa na dola ktk akiba, na ndio maana akina Gaddafi walikuwa wanakataa hio system wakafanyiziwa. sahizi akina Putin na wachina wanaipinga pia.

Ninavyoelewa ni hivi.
Mfano hapo bongo, kila bank ina account yake kule BoT na kila asubuhi wanaishibisha account yao. Hivyo ukifanya transaction kutoka NBC kwenda Aania bank, BoT wanangalia account ya NBC kama ipo poa na kama ipo poa wanafanya trasact. Hivyo hii accound ndo ina determine mwenendo wa Bank kwa siku hiyo at local level.

Sasa kwa international level, pia BoT nao wana account inayomiliki dola, hii ndo ina determine trasanction kati ya nchi na nchi, sasa kama account ya dola ya TZ ni kiduchu basi ndo hivyo tena shillingi inaporomoka kimtindo.

Sasa wafanya hujuma, kazi yao mkeweka dola kwenye account yenu wanazinunua kwa fujo, zinaiisha mnashindwa kuziregulate na ndo hivo tena currency inaporomoka.
 
Burund hawatuzidi kwa lolote. Labda tuongelee mwenendo wa sarafu zetu dhidi ya sarafu za kimataifa. Yen moja ya Kijapan ni sawa na 0.8 Kenyan shilling. Hiyo haina maana kuwa uchumi wa Japan ni karibu sawa na uchumi wa Kenya!
 
Nadhani wachumi wanaweza kutusaidia lakini sidhani kama wanatuzidi kiuchumi sababu nilikuwa Lusaka Zambia sasa hivi kwacha ya Zambia in strong kuliko South African rand kwa asilimia 100% yaani ukitoa Rand 100 unapewa Z-kwacha 50
Sasa basi kiuchumi Zambia ukilinganisha na south Africa Zambia bado sana
Wachumi please njooni mtufafanulie
binafsi sikubaliani na sababu zinazotolewa na hao wachumi wetu, eti tunaagiza sana bidhaa nje ndo sababu ya sh. kuporomoka!, kwani tumeanza mwaka huu kuagiza bidhaa za nje? kwanini sh iporomoke kwa kasi hivi wakati miaka yote tunaagiza bidhaa toka nje? hii sababu ni ya kizembe sana.
 
Swali zuri ila burundi mbali mbona huulizi kenya? Subiri muda si mrefu utajaza kiroba cha hela kwenda kununua mkate mmoja tuu.

wakuu mliobobea kwenye masuala ya uchumi naomba mnisaidie hapa.sote tunafahamu kuwa thamani ya shilingi yetu imeshuka kwa kasi sana.

Wataalam mbalimbali wametoa sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na kuingiza zaidi bidhaa za nje kuliko sisi kuzipeleka nje bidhaa zetu.

Pamoja na sababu mbalimbali;swali langu ni hivi juzi nilikuwa burundi pale mpakani pesa yetu ipo chini wakati faranga ya burundi ipo juu,sasa kwanini inakuwa hivyo wakati nchi yao ipo kwenye machafuko hivyo hawazalishi?

Aidha wale jamaa tumewazidi ki-viwanda yaani karibia asilimia tisini ya vitu vya viwandani vinatokea kwetu,kwenye upande wa chakula ndio usiseme,yaani mimi ninashangaa kwanini faranga yao ipo juu wakati wao tunawazidi kwa kila kitu?,

siku nimeenda walikuwa wana-chenji shilingi mia kwa faranga 92,

nawasilisha wakuu.
 
Swali lako ndio langu naomba ajibu mwigulu nchemba

cc mwigulu nchemba

binafsi sikubaliani na sababu zinazotolewa na hao wachumi wetu, eti tunaagiza sana bidhaa nje ndo sababu ya sh. Kuporomoka!, kwani tumeanza mwaka huu kuagiza bidhaa za nje? Kwanini sh iporomoke kwa kasi hivi wakati miaka yote tunaagiza bidhaa toka nje? Hii sababu ni ya kizembe sana.
 
Wakuu mliobobea kwenye Masuala ya Uchumi Naomba mnisaidie hapa.Sote tunafahamu kuwa thamani ya Shilingi yetu imeshuka kwa kasi sana.

Wataalam mbalimbali wametoa sababu kadhaa Ikiwa ni pamoja na Kuingiza zaidi bidhaa za nje kuliko sisi kuzipeleka nje bidhaa zetu.

Pamoja na sababu mbalimbali;Swali langu ni hivi Juzi nilikuwa Burundi pale mpakani Pesa yetu ipo chini wakati Faranga ya Burundi ipo juu,sasa kwanini inakuwa hivyo wakati nchi yao ipo kwenye Machafuko hivyo hawazalishi?

Aidha wale jamaa tumewazidi ki-viwanda yaani karibia asilimia tisini ya vitu vya viwandani vinatokea kwetu,Kwenye upande wa Chakula ndio usiseme,yaani mimi ninashangaa kwanini Faranga yao ipo juu wakati wao tunawazidi kwa kila kitu?,

Siku nimeenda walikuwa wana-chenji Shilingi mia kwa Faranga 92,

Nawasilisha wakuu.

Mkuu licha ya utajiri wa rasilimali tulizonazo Tz inazidi kuwa masikini kwa sababu ya aina ya viongozi/watawala tulionao na hasa kutoka chama tawala!
 
Mimi nadhani uchumi wa nchi haupimwi kwa thamani ya pesa peke yake sababu kuna choka countries lakini pesa zao zina thamani
 
Back
Top Bottom