Hivi kwa nini ukimtumia msichana sms kama ni mara ya kwanza alafu msg iingie kwenye simu yako roho inapasuka sana

Yaani mara ya kwanza kumtumia demu msg ya kumtaka kimahusiano basi kama dakika 3 hivi msg ikaingia kwenye simu yangu basi kwa ule mshtuko niliopata sikuifungua muda huo kwanza niliendelea kufanya kazi zangu huku kijasho kinanitoka hapo nawazia jibu lipi limerudishwa nikamaliza kazi yangu nikaoga.

Basi nikaenda sehemu nikaagiza kinywaji ile naanza kunywa nikatoa simu mfukoni nisome jibu la msg yangu nakuta simu imezima chaji.

Hivi kuna mahusiano gani ya msg na mshtuko wa mapigo ya moyo kuongezeka?
Hujui namna yakuaza kutongoza au uliaza kutaja kazi yako namshahara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani acha tu. Haya mambo yanaleta mshtuko sana. Mwingine alidondosha simu kwenye maji kabla hajasoma meseji na simu ikafa hapohapo. Hahahahaha
 
Hali hiyo ni kawaida kwa mtu anayetarajia na siyo kwa issue ya mahusiano tu ni kwa kila anayesubiri majibu kutokana na mtihani au application yoyote atakayo kuwa ameifanya na anatarajia kupokea majibu.

Kila apatapo kijumbe ashiria lazima moyo uende mbio, na anapokuta kijumbe hicho akina uhusiano na kitu alichotarajia hasira inamkaba.
 
Back
Top Bottom