Hivi kwa nini tuliungana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwa nini tuliungana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bishop Hiluka, May 6, 2012.

 1. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Wazanzibar wanalalamika wamemezwa na Tanzania Bara, Watanzania Bara (Watanganyika)
  wanalalamika kuwa wameipoteza Tanganyika yao na wananyonywa kupitia mwamvuli wa
  Muungano wa Tanzania, lakini wachache katika serikali yetu wameapa kuwa wataulinda
  muungano huu kwa nguvu zote!

  Ni ajabu sana kuwa kila upande unalalamika! Inashangaza sana katika vuta nikuvute hii eti
  kuna kundi linasema litaulinda Muungano kwa nguvu zote! Katika kuulinda huu Muungano
  kumekuwepo tafsiri ambayo inahitaji ufafanuzi; kuulinda kwa nguvu zote maana yake nini?

  Kwangu kauli ya kuulinda ni kuzuia watu wasiujadili. Kutoruhusu uvunjike. Kama ni hivyo,
  ya nini kuwa na muungano bila kuujadili? Inafaa nini kuishi kwa mazoea? Na kwa faida ya nani?
  Huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisema kuwa jambo pekee wanalopaswa
  wananchi kujadili kuhusu Muungano ni kuuboresha! Inawezekanaje watu waboreshe kitu
  ambacho hawajakubaliana umuhimu wake?

  Rais amesahau kuwa Watanzania walio wengi wamezaliwa baada ya Muungano? Ingawa
  wamesoma habari za Muungano katika vitabu vya historia lakini hawauelewi vyema, ndiyo
  maana hata shamrashamra za serikali na wananchi juu ya Muungano zimeshuka siku hizi.
  Tunachoshuhudia ni wananfunzi kulazimishwa kwenda kwenye sherehe hizi bila ridhaa yao.

  Kama hatuujui vyema Muungano wetu, kwa nini sasa wanataka kutunyima fursa ya kuujadili?
  Fursa imejitokeza kupitia kmchakato wa katiba mpya lakini viongozi wanatuzuia? Hivi wana
  nia gani? Wanayafanya haya kwa faida ya nani? Wananchi ambao ndiyo wenye nchi yao
  wanataka kuandika upya historia yao tena kwa nyakati zao lakini viongozi wanataka kuwaenzi
  waasisi kinafiki! Nani mwenye nchi? Wananchi au viongozi?

  Ni kufilisika kimawazo kudhani kwamba anayehoji Muungano ana nia ya kuuvunja. Badala yake,
  ni kuchochea mjadala mpana na wa kina kuhusu umuhimu wa Muungano.

  Tusidhani kuwa tuna akili kuliko wengine. Tuna kipi cha ajabu? Tukumbuke Ethiopia ilitengana
  na Eritrea, muungano wa Senegambia ilisambaratika na kubaki Senegal na Gambia, pia iliyokuwa
  Rwanda-Burundi sasa ni nchi mbili za Rwanda na Burundi, India iligawanyika na kuzaa Pakistan,
  na Pakistan ikazaa Bangladesh.

  Inashangaza sana kuona kuwa kundi dogo linataka kubinafsisha mawazo ya walio wengi, vijana
  na wasomi wa taifa hili wanashindwa kuhoji mambo kwa mapana yake. Tunapaswa tujiulize,
  hivi kwa nini tuliungana? Huu si wakati tena wa kuleta sababu dhaifu eti tunaleta umoja au eti
  kwa vile sisi ni ndugu. Mbona hatuungani na Wakenya wakati nchi zote hizi zina undugu?

  Kwa nini hatupewi nafasi ya kuhoji nini sababu hasa ya muungano huu? Wenye majibu wote kwa
  sasa hawapo na yaliyobaki ni majibu ya kufikirika tu, nafasi ya uongo ni kubwa. Bila majibu haya,
  ni vigumu ni bora watu wakajadili na wakaja na aina ya muungano wanaoutaka…
   
Loading...