Hivi kwa nini Mme na Mke waliofunga ndoa na pengine kupata watoto huwa wamenuna wakiwa kwenye gari?

Mchokozi

JF-Expert Member
Feb 9, 2012
215
29
Wana JF nimejaribu kufanya utafiti kidogo na kugundua kuwa asilimia kubwa ya mme na mke huwa hawana maongezi ya furaha wakati wakiwa kwenye vyombo vya usafiri wakiwa wanaelekea sehemu mbali mbali za kujenga taifa ???, ukiona wanaongea kwa furaha basi watakuwa ni hawara. Mwenye sababu ya msingi amwage data ndani ya JF
 
Mnanuniana nyie wenye magari. Sie tusio na magari hatuna nafasi ya kununiana. Tuko bize kufikiria namna ya kupata mkate wa kila siku. Na hasa sisi wenye familia zenye watoto, nakwambia kwetu wakati wote ni wakati wa Bunge la Bajeti ya familia.
 
Umenifanya nicheke kwa nguvu maana hua nashuhudia situation kama hizo pia..nadhani hua inasababishwa na aina ya maisha wanayoishi wanandoa,kama familia imetawaliwa na mfumo dume kupita kiasi kuna kua na hali ya mke kumuogopa mumewe to the extent wakiwa pamoja wanashindwa kuinteract..
Pia migogoro ya kifamilia inaweza kua chanzo cha kununiana..
 
Ahhaha huwa mwanamke amekurupushwa alikuwa bado anajiremba akafokewa kidogo anaingia na kisirani chake...na anahisi huyu akiwa na vidosho anawakimbiza hivi au ananiona nimeshajichokea??"Nami nitanunua la kwangu usinibabaishe"hhaha napita tu
 
kweli kabisa aisee. Huwa nashuhudia kila siku. Hata mie leo asubuhi imenitokea.
 
Wana JF nimejaribu kufanya utafiti kidogo na kugundua kuwa asilimia kubwa ya mme na mke huwa hawana maongezi ya furaha wakati wakiwa kwenye vyombo vya usafiri wakiwa wanaelekea sehemu mbali mbali za kujenga taifa ???, ukiona wanaongea kwa furaha basi watakuwa ni hawara. Mwenye sababu ya msingi amwage data ndani ya JF

Hapana! Kwanza nikukumbushe yakwamba furaha kati ya mtu na hawala ni ya
  1. ni furaha ya muda (without peace)
  2. Mara nyingi nifuraha ya hira/sababu ndani yake (mfano we ukijua unakwenda kupata hera za bure si utajichekeshachekesha!)
  3. watu wengine ni professional wahuni.....wanakuwa na tabasamu na maneno mazuri kwa yeyote wanayekutana nae. (sasa ukiwa mshamba utazani umepata kumbe hata mwenzio afanyiwa hivyo hivyo!)
  4. Maawala (hao wapenzi) mara nyingi wanakuwa wamefahamiana muda mfupi amawanakaa pamoja kwa muda mfupi na main ajenda yao ni kufanya ngono tu basi si kupanga na kuangalia mabomengine kimaisha
  5. Mahawala wanaongozwa na kumtamani mtu, kumtaka mtu, kutaka kuona utupu wa mtu ama anavyofanya/angaika kitandani....katika haya hakuna UPENDO
  6. Kwa ufupi si sahihi kulinganisha vitu viwili vilivyo tofauti, yaani mahusiano ya hira na mahusiano ya kwenye ndoa

Kwa ufupi mahusiano ya watu waliooana wakati mwingine wanapendana kama mtu na dada yake. kati ya Kaka na dada kuna upendo na hakuna kumamaniana
 
Mnanuniana nyie wenye
magari. Sie tusio na magari hatuna nafasi ya kununiana. Tuko bize
kufikiria namna ya kupata mkate wa kila siku. Na hasa sisi wenye familia
zenye watoto, nakwambia kwetu wakati wote ni wakati wa Bunge la Bajeti
ya familia.

teh,teh,hilo nalo nenoo! unajua wenye magar ndio hao wenye kipato kizur,na kama ujuavyo pesa ndo inaleta nyumba ndogo,ujirushe club na bia kwa sana had unachelewa kurud hm,kwa hiyo ukirud hm unakuta mama yoyo kanuna na kesho asbh mnapanda gar moja,we unafikir kuna tabasam humo wkt jana kuna bifu na pengine hata k ulinyimwa?
 
Hapana! Kwanza nikukumbushe
yakwamba furaha kati ya mtu na hawala ni ya
  1. ni furaha ya muda (without peace)
  2. Mara nyingi nifuraha ya hira/sababu ndani yake (mfano we ukijua
    unakwenda kupata hera za bure si utajichekeshachekesha!)
  3. watu wengine ni professional wahuni.....wanakuwa na tabasamu na
    maneno mazuri kwa yeyote wanayekutana nae. (sasa ukiwa mshamba utazani
    umepata kumbe hata mwenzio afanyiwa hivyo hivyo!)
  4. Maawala (hao wapenzi) mara nyingi wanakuwa wamefahamiana muda mfupi
    amawanakaa pamoja kwa muda mfupi na main ajenda yao ni kufanya ngono tu
    basi si kupanga na kuangalia mabomengine kimaisha
  5. Mahawala wanaongozwa na kumtamani mtu, kumtaka mtu, kutaka kuona
    utupu wa mtu ama anavyofanya/angaika kitandani....katika haya hakuna
    UPENDO
  6. Kwa ufupi si sahihi kulinganisha vitu viwili vilivyo tofauti, yaani
    mahusiano ya hira na mahusiano ya kwenye ndoa

Kwa ufupi mahusiano ya watu waliooana wakati mwingine wanapendana kama
mtu na dada yake. kati ya Kaka na dada kuna upendo na hakuna
kumamaniana

duh,kaka we itakua ni padri tena baba paroko kabisa,point zako zimenigusa!
 
We Mchokozi peleka uchokozi wako huko. utafiti wako siyo kweli. Kwanza kuna wenye magari wengine hawatoi lift kwa wanawake na ikitokea anamuweka kiti cha nyuma ili kumpa salamu kuwa hapa pana mwenye nyumba.

Na ikitokea wapo mke na mume ni jambo la kawaida kuwa una utulivu lakini siyo kwamba ni utulivu wa chuki.
 
kuishi 'two as one' na mtu mwenye utashi na akili timamu, 24/7, si kazi ya kitoto ati. Unless mmoja yuko off. KUA UYAONE.
 
story zote wamepiga nyumbani sasa kwenye gari waongee nini? Je ulishawaona wakiwa nyumbani pamoja wanakuwaje?
 
Back
Top Bottom