Mwana jf unaweza kutoa sababu ya vijana wengu wa tz kukosa ajira ijapokuwa wengine wamesoma lakini hawana ajira?
Ingekuwa wote watanzania wana ufahamu huu nitakaoelezea hapa, basi Tanzania ingekuwa hazina ya Africka kama si dunia yote;
Kwanza, katika nchi inayotaka kuendelea kiuchumi haitegemei ajira za serikali ndo ziwawezeshe watu kufanikiwa kiuchumi na kuinua uchumi wa nchi yao, rahasha;bali hutegemea sector binafsi ya ubunifu na ujasiri wa kuanzisha kazi au kampuni zitakazoibua uwekezaji katika nyanja mbalimbali siyo kutegemea kuajiriwa na serikali.
Ukitazama Nchi zilizoendelea sector binafsi ndizo zinazoongoza si tu kuingiza kipato kikubwa cha kodi serikalini bali kulipa mishahara mikubwa kwa watendaji wake aidha wawe ndo waanzilishi au wale wanaopenda kuajiriwa kwalo ilimradi wakidhi vigezo vya ubunifu na ujasiri katika nafasi zao.
Pili, Vijana tuache uvivu na uharaka wa kuwa na kipato kikubwa kwa wakati mfupi ' haiwezekani' na hakuna principle yoyote itakayokupa nafasi ya kufanikiwa kwa muda mfupi labda uwe jambazi au muuza madawa ya kulevya nako kuna risk zake ambako maisha yako yatakuwa hatarini kila sekunde.
Nakumbuka nilipokuwa namaliza degree yangu ya kwanza, cha kwanza niliangalia mahitaji ya jamii yangu yaani nchi yangu kwe elimu niliyopata, nikaona fursa ni nyingi sana hasa huko wilayani, nikaanzisha kampuni nikavumilia mwanzoni mwa kazi zangu za awali, kadri miaka ilivyokuwa inasonga ndivyo nilivyozidi kupata uzoefu na wigo mpana zaidi, nikaungana na wenzagu tukapata miradi mingi na tukaajiri wenzetu ambao hawako tayari kuwa wabunifu tukawapa TOR (miongozo) yetu ya utendaji; kwanza wawe tayari kufanya kazi wakati wote ufaao na usiofaa, usiku na mchana kwa muda wa miaka mitatu na baada ya hapo watapata share katika kampuni, wengi walikataa, wachache wakakubali wastrive na tukawapa share, sasa wale waliokataa hadi huvi leo wanahaha wanagonga nauli za daladala kila kukicha, wenzao tuko ndani ya viyoyozi hata kama ni Vitz lakini tunamiliki kihalali kupitia ubunifu wetu.
Tatu,Tuache kulalamika na kuinung'unikia serikali ingawa inastahili kupigiwa kelele kwa kuwa na Viongozi wanaoibeza nchi yao kuwa ni masikini na kuendelea kuomba fedha za misaada kwa hao wanaochuma maliasili zetu,hii nchi ina kila kitu tamka unachoweza kutamka kipo katika nchi, fikiri mwenyewe anza sasa hujachelewa nenda wilayani utokako au ulikowahi kufika kaangalie fursa mbalimbali anza polepole,Nina uhakika kama utaanza leo hicho unachofikiri baada ya miaka mitano itakuwa legacy.
Nne; Uspende kuajiriwa penda kuajiri wengine ndipo utakapopata kile unachotamani kuwa nacho katika mawazo yako, inakuweje unafikiria kununua au kujenga nyumba au kuwa na mshahara mkubwa kwa maono ya mwingine hutafanikiwa kwa wakati utakao! huwezi jua labda huyo aliyekuajiri atasitisha au kukuachisha kazi akizidiwa au akifirisika!
Tano, Jamii forum ni maono ya mtu na alianza kama wazo limekuwa kama lilivyo kwakuwa alikuwa jasiri na mbunifu wa nini anataka awe na nini anategemea kupata na sasa anaweza kupanua wigo kibiashara si haba atapata chai ya watoto na atafika mbali kama atakuwa mbunifu zaidi na itafika mahali tutakuwa tunalipia hata haya tunayoyaandika hapa maana hii ni huduma.So be creative my bretheren!
Sita, Usipende kujilinganisha na mtu alivyofanikiwa huwezi jua alivyofanikiwa na amechukua muda gani kufika hapo, wewe chukua hiyo kuwa ni changamoto na ujifunze kuwa na bidii na kuvumilia acha kuwa kama mimi wakati wewe si kama mimi ni wewe na utabaki wewe na una destination yako.
Saba, Mtegemee Mungu naye atakusaidia.
No Vision No Provision.
Ndaga,