Hivi kwa michepuko kuna nini?! Inawezekanaje?!

Hivi kwa michepuko kuna nini?! Inawezekanaje?!

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,138
Reaction score
10,852
Ukiongea na wachepukaji lazima watakushuhudia kuwa huko mchepikoni kuna raha na furaha fulani, No stress, Satisfaction na eti wana-enjoy sana to the Uhuru Peak.

Na mbaya zaidi hili hasa utalikuta kwa married couples (wanandoa).

Niliwahi kusimuliwa kwa coincidence na wanandoa wawili kwa nyakati tofauti, kila mmoja akishuhudia jinsi anavyo enjoy na kurdhika na mchepuko wake na Hindi anavyokuwa under served nyumbani.

Yaani una baki why why why!
 
seems hujaoa bado ngoja uoe kwanza.
 
Nawashangaa sana wanaume wanaosifia michepuko kuliko wake zao.[emoji57] [emoji57] kama Huyo Mchepuko anamridhisha na kumpa furaha si angemuoa
 
Ngoja huyo mwanaume apate maradhi ya kumlaza hata mwezi kama atauona huo mchepuko hata ukimjulia hali tu.

Wanaume wenyewe ndo Hawa akiumwa mpaka mnatia huruma mnahitaji uwepo wetu sana sasa ushamfanyia visa wife michepuko ya kutosha sijui mnategemea nini raha ya nusu saa inawapa wazimu mnasahau wake zenu.
 
Kuna vitu vingi vinavyomfanya mwanaume kuwa kiongozi....na kimoja wapo ni kuweza kuhimili mihemko yake........

Tukiwa kama wanadamu kuna nyakati tunavutiwa na vitu fulani nje ya wenzi wetu.......lakini hiyo hali haikuhalalishii wewe kuliendea jambo hilo na kutimiza haja za nafsi yako....bali ukiwa kama mwanaume aliyekomaa kifikra unapaswa kupuuzia kwa kuwa nyumbani yupo malikia wako.....ambaye umemteua kati ya wale wengi........

Migongano na misuguano kwenye ndoa ni vitu vya kawaida kwa kuwa hakuna mkamilifu kati yenu......na wanandoa wanandoa wanaojitambua na kutambua majukumu yao hushughulikia tofauti zao na kutafuta mbadala nje......

Kuwa au kuamua kuingia kwenye ndoa kunahitaji utayari wa kimwili na kiakili......lakini kwa haya yanayoendelea kwenye ndoa nyingi ni dhahiri kuwa vijana wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa tayari kimwili lakini si kiakili.......

Na hiyo inadhihirishwa na uwezo wao mdogo wa kushughulikia mambo madogo kwenye ndoa zao na kuamua kutafuta mbadala......jambo ambalo ni hatari kwa afya ya ndoa zao na miili yao kwa ujumla........
 
Wazinzi sehemu yao ni kwenye Jehanam ya Moto. Biblia inasema anayezini na mwanamke hana akili kabisa. Sasa wewe unayechepuka ni miongoni ya watu waso na akili katika ulimwenguni huu. Mwisho wa yote ni majuto hapa duniani na kuzimu.
 
Back
Top Bottom