Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Kwanza napenda kutoa pole kwa familia ya marehemu Regia Mtema na watanzia wote kwa ujumla kwa kifo cha mpendwa wetu dada Regia. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. AMINA........Nimeanza kuumiza kichwa na kupata kizunguzungu. Kila kukicha kupitia vyombo vya habari utasikia; mara, 'CCM wakabana koo' mara 'CDM yawagaragaza CCM' mara kamati kuu CCM sijui nini....? Hivi demokrasia bila vyama vya siasa katika nchi haiwezekani? Mi naona serikali kavu kavu itapunguza hizi kelele na uhasama kila kukicha. Naona kama mambo ya vyama haya kwa kiasi fulani yanapoteza muda wa watu kufanya kazi, manake tunapoteza sana muda kufuatilia mbwembwe za wanasiasa na kuacha mambo mengine. Kila chama kinapigania kuingia madarakani ili kuongoza serikali. Nauliza tena, je serikana bila chama cha siasa haiwezekani?