Hivi kutongoza ni kosa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kutongoza ni kosa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by St. Paka Mweusi, Nov 16, 2010.

 1. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,897
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wana JF nimekuwa nikijiuliza siku nyingi swali hili na sipati jibu sahihi.Utakuta umempenda mtu unaona ni heri umueleze kilicho moyoni mwako tena kwa upendo na upole tu,lakini matokeo yake majibu utakayokutana nayo inakuwa kama vile ni adhabu,utaambiwa huna adabu,kamtongoze mama yako,utapewa misonyo,pengine hata kichapo toka kwa watu,wengine waliwahi hata kusakiziwa mbwa,na mbaya zaidi unawezakuta mtu hakutaki lakini anaamua tu kukukomesha kwa kukupa shida zake zoote na wewe kwa kuwa umependa basi utamtimizia na bado unaambulia patupu.Mengine tunayokutana nayo wakuu mnaweza kuongezea lakini swali langu ni hilo,je kutongoza ni kosa mpaka wanaume tustahili adhabu zote hizi?
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hizo geresha tu, wengi wao wanapenda kutongozwa. Ila style yako isiwe kingono zaidi!
   
 3. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,897
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145  Mkuu ni sawa lakini wakati mwingine hata kabla hujapewa nafasi ya kutoa yaliyo moyoni mwako unafunguliwa mbwa ni haki kweli?
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni kama pale mtaa wa kongo saa ya kununua kiatu. Ukifukuzwa maana yake thamani yake kubwa, hiy siyo kwamba ondoka. Mara nyingi wanataka kuonyesha kwamba wao hawapatikani kirahisi. Mwanamke anayekukataa kwa ukweli hana sababu ya kuwa na hasira na wewe. Atakwambia vizuri tu au ataweka mazingira ambayo mtongozaji mwenyewe ataona game iko tight.
   
 5. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,897
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145

  Hapo na mimi ndio najiuliza inakuwaje inafikia mpaka hatua ya mwanamke kujikusanya na wapambe wake kukupiga mawe ilhali wewe unatongoza tu?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,417
  Trophy Points: 280
  Kweli hii kali, hadi hatua ya kupigwa mawe lol! Mi nshasakiziwa mbbwa tu ila mawe hiyo ni next level
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole Paka maskini mpaka mawe huo ni unyanyasaji wa jinsia:doh:
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Kadiri ukali unavyokua mkubwa, ndivyo atakavyokubali haraka.
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Blaza tatizo kubwa ni timimg.
  Kila kitu duniani ni timing tu.

  ukisoma alama za nyakati unaweza mpata yeyote umtakaye.

  Uhandsome pekee si hoja Shule mmmh!
  Pesa, nayo wakati fulani haioni ndani.

  Timing ndo kila kitu blaza.

  ukitongoza onyesha kwamba umezimika, siyo kwa masafa mafupi bali ya kati.

  Eti maneno mawili matatu mara unaonyesha nia na dhamira ya kula uroda.

  Wakati mwingine mimacho yako au hata posing yako inaonyesha jinsi unavyotamani.

  Mademu wengi cha kwanza wakipendacho ni mahusiano, ni urafiki siyo majambos.

  Majambozos ni matokeo tu.

  Mimi pamoja na shati langu la kutoboka mabega, enzi zangu nisha wahi tembelea mijiwanja ya nguvu bila nini wala ni.

  Blaza timing blaza.

  Usisukumwe na hamu ya kutaka uroda, ujenzi wa hoja na mfuatano wa mambo ndiyo jambo la kujenga msukumo.

  Usilazimishe mambo hata siku moja.

  Ukiwa huku majuu pochi ndo inatongoza.

  Huku hapendwi mtu kwanja lake wala sura,inapendwa pochi tu.
   
 10. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,806
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Yaap! akiwa mkali we kuwa mlaini baaaaaaaasi! shughuli imeshakwisha hiyo! kama unamsukuma mlevi!:smile-big:
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ahahahah hii ya kufunguliwa mbwa ni kali kuliko!
   
 12. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mweeeeeeeee!!!!!!!
  aya !!!!
   
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  Nov 16, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Duuhhh!!! Mawe tena hii mbona ya kizamani sana!
   
 14. RR

  RR JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Najua wewe ukali huuwezi...
   
 15. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kweli ukali siuwez...nauweza upole2..!!!!!
   
 16. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hutongozi tu kila mtu bara barani soma kwanza alama za nyakati. Mpe muda naye wa kukufahamu sio wewe kwa kuwa umemuona na unajua nyendo zake basi ukadhani naye anakujua. Hata ingekuwa wewe utamkubalia mtu ambaye hujawahi muona?
   
 17. RR

  RR JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Ukiwa mpole digidigi hawaji...:dance::dance:....
  Ya nini malumbano!
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  Conclusion ni kwamba Rose80 ngumu kumpata.....eeh?
   
 19. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa yako
  Mwanamke akikaa wiki hajatongozwa hujiona hajakamilika
  Kumbuka pia
  Hata chui/simba jike huzaa
   
 20. RR

  RR JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Hommie......ngumu ni relative bana...
   
Loading...