Hivi kupingana na CCM ni uchochezi?

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
203
Kuna dhana iliyojengeka miongoni mwa viongozi wengi wa serikali na taasisi zake kwamba yeyote anayetofautiana na CCM au kuikosoa kwenye public basi ni MCHOCHEZI. Mifano ni mingi, lakini tishio la kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mwanahalisi ni mfano mzuri zaidi wa hali hiii iliyojengeka kwenye jamii yetu. Viongozi wa MAELEZO (bila shaka kwa umbumbumbu wao) wanaamini kwamba ukienda tofauti na CCM kimtazamo basi wewe ni mchochezi. Bado wana mawazo mgando na hawajui kwamba tulikwishaondoka siku nyingi kwenye enzi za 'chama kushika hatamu'. Ujinga huu unatoka wapi na tutauondoaje?
 
wangejua mtu anayekukosoa ndiyo anakupenda! sababu hataki upotee ILA UFUATE MIIKO YA CHAMA CHA MWALIMU!
 
TAMWA?MADIWANI NA WABUNGE WA UPINZANI WANAOENDELEA KUBAMBIKIWA KESI MARA WA CUF PANGANI ETI ALIBAKA MWAKA 2008 Jana ndio wanamkamata!
 
tamwa?madiwani na wabunge wa upinzani wanaoendelea kubambikiwa kesi mara wa cuf pangani eti alibaka mwaka 2008 jana ndio wanamkamata!
na mwananchi inatashiwa kufungiwa. Lakini mimi nashangaa sana polisi kwa kuisaidia ccm, kwani ktk wafanyakazi wanaokandamizwa na serikali polisi wanaongoza. Takukuru nao, vijana wasomi, lkn wamedanganywa na posho ya lk 4, kila kila mwezi wanajiona wako peponi.
 
Hapo ndiyo na mimi nashanga!ili uwe raia mwema ni lazima uwe mshabiki wa CCM!Duh this is unfair!
 
hawana lolote...wanahaha tu kuona mwisho wao umekaribia!! dawa yao na sisi "tunafunga vioo" tu!!
 
wanatakaje hawa wafu???
hata vitabu vya dini vinakataza kumsujudia binadamu mwenzio
 
Sababu wamezoea kuburuza waTZ sasa usawa huu wa TZ wamejanjaluka siku hizi ule wakati wa kulamba miguu walio juu imeshapitwa na wakati. They can go to hell come 31st Oct!!
 
Back
Top Bottom