Hivi kuna wake kama huyu mama kwa tabia?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,343
2,000
Mume aliachishwa kazi miaka 4 imeisha, mke hajawahi lalamika hata siku moja kwanini mwanaume hatoi hela na hajawahi mlalamikia mwanaume kuhusu mahitaji ya pesa ndani,

Mke huwasilisha pesa zote za marupurupu mezani kila anapotoka kazini ili mwanaume atunze na apange matumizi yake,

Mke amekataa kujihusisha na bajeti ya pesa ndani pamoja na kuwa yeye ndiye ana kipato kwa miaka yote hii 4, ila mwanaume akimwambia wapange bajeti ndio anakubali si vinginevyo,

Mke kamuachia mwanaume kuwa mshauri mkuu wa pesa anazo tafuta yeye mke, kitakacho amuliwa na mwanaume na kuona kinafaa basi mke huridhia mke hana neno,

Mwanaume ndiye kaachiwa kadi ya benki kutoa na kupanga matumizi,

Mke hana tama ya kupenda vitu vya hali ya juu huwa mwanaume ndiye anaamua kumchukulia mke vitu vyenye thamani ila mke hataki, mke husema kama mume ataleta au kumnunulia sawa ila sio yeye.

Maswala mengi yanayohusu aina ya vitu, chakula na maisha yao mwanaume ana nafasi kubwa sana pamoja na kutokuwa na kipato,

Mwanamke kila atokapo kazini hufikia kumpa ripoti ya kazi alizozifanya na kipato alichokipata kwa siku hiyo, mke hana password kwenye simu mara nyingi humpa mumewe atumie simu yake na mumewake humpa mkewe simu yake atumie,

mke na mume hawana hata chembe ya siri ndani kwao, mume alipokuwa akifanya kazi alikuwa anamwachia mke walet kujua kuna hela ngapi, mfukoni mwa suruali mke hujua mume wake ana sh ngapi, mke alikuwa anajua benki mumewake ana sh ngapi na password zote anazijua mke


Wana JF nimeliona na nimeshuhudia nimeshangaa sana kwa mke kuwa na tabia hizo zaidi sana anajua mume hana kazi halafu amekataa kuwa msiri mwanaume anajua kila kitu hadi password zote za benki…

Hivi kweli wanawake kama hawa tunao wangapi. Ila huyu mwanaume sio kwamba kalelewa hapana au ameolewa hapana najiuliza je hili lawezekana kumpata mwanamke kama huyu.
 

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,343
2,000
chini ya jua hawa wananwake wamebakia wachache sana, may be kwenye sayari nyingine watakua wengi
Ameniacha mdomo wazi, mume wake amekuwa akinieleza yote haya nimeshangaa sana, sasa sijui wa sasa hivi wamejifunza wanayoyafanya kwa nia gani, jamaa kaniambia huyu mkewake amezingatia malezi ya wazazi wake anasema kuwa ameiga yale wazazi wake walio kuwa wanayafanya na walimsihi asitoke nje ya mstari.
 

Dr Chew Ing Gum

Senior Member
Aug 7, 2017
161
250
Dependent personality disorder?, halafu kweli mtu miaka minne yote huna kazi kabisa, hata kuanzisha biashara yaani huwezi. Hongera zao.
 

kasulamkombe

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
2,232
2,000
kuwa na hela tujue tabia yako au kosa hela tujue tabia ya mke wako.wanawake wengi ukifulia mazarau yanaanza anaweza hata akaanza kuondoka nyumbani bila hata ya kukuaga au ndugu zake ndio wakawa ndio watawala wakuu wa nyumba yako.Hata chakula anaweza akawa anakula na watoto bila ya kukuambia na mchezo wetu ule wa kupapasana usiku ndio anaweza akawa anakunyima pia.Unajua ndio maana hata kwenye vitabu vya dini tunashauliwa kuishi nao kwa akili.HATA MUNGU ANAJUA NDIO MAANA NI WACHACHE NDIO HUWA WANAKUWA NA HELA NYINGI KUMZIDI MME WAKE.WAKIWA NA HELA NYINGI NI SHIDA.MKE KAMA HUYU NI WACHACHE SANA KULIKO WANAWAKE WASIOLALAMIKA MME WAKE MWENYE KIBAMIA!!!
 

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,343
2,000
Dependent personality disorder?, halafu kweli mtu miaka minne yote huna kazi kabisa, hata kuanzisha biashara yaani huwezi. Hongera zao.
si kila mtu anaweza biashara kuna kazi zingine zinahitaji uvumilivu maana huenda mtu unaomba ila bado hujafanikiwa si unajua urasimu wa kazi za watu kila mtu anatka ampe dnugu yake kwanza
 

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,343
2,000
Mwanamke aina hiyoo mwanaume lazima uwe mpiganaji.
Sikuzikija tena lazima umjali mkeo na familia maradufu.

Mungu awape maisha marefu wanawake aina hiyoo.
Mwanaume ndiye aliyeanzisha mke akaona iwe hivyo hata hivyo mke anasema wazazi wake walimuelekeza kuishi maisha ya uwazi na mumewe ili maisha yawe mazuri zaidi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom