Hivi kuna wake kama huyu mama kwa tabia?

Hivi kuna wake kama huyu mama kwa tabia?

Haiwezekani ***** wanawake hawapo hivyo toka Enzi za Hawa
inaelekea unakutana na balaa tupu, ila ndo hivyo imekuwa na imewezekana, nilifikiria mara mbili na kumuangalia huyu mke wa jamaa halafu yuko simple sana.
 
... huenda mume kipindi anakazi alimjali nA kumthamini mke wake.....


Kubali tu kuwa huyu ni mwanamke wa pekee. Maana wanwake wengine hata uwatunze vipi ukiyumba kimaisha tu halafu yeye ndiye ana kazi utajuta.
 
Mwanaume miaka yote minne anapanga tu bajet ya pesa ya mkewe ni aibu
 
Kubali tu kuwa huyu ni mwanamke wa pekee. Maana wanwake wengine hata uwatunze vipi ukiyumba kimaisha tu halafu yeye ndiye ana kazi utajuta.
Inategemea nA kipindi una kazi uliishi vp na mkeo
 
Mume aliachishwa kazi miaka 4 imeisha, mke hajawahi lalamika hata siku moja kwanini mwanaume hatoi hela na hajawahi mlalamikia mwanaume kuhusu mahitaji ya pesa ndani,

Mke huwasilisha pesa zote za marupurupu mezani kila anapotoka kazini ili mwanaume atunze na apange matumizi yake,

Mke amekataa kujihusisha na bajeti ya pesa ndani pamoja na kuwa yeye ndiye ana kipato kwa miaka yote hii 4, ila mwanaume akimwambia wapange bajeti ndio anakubali si vinginevyo,

Mke kamuachia mwanaume kuwa mshauri mkuu wa pesa anazo tafuta yeye mke, kitakacho amuliwa na mwanaume na kuona kinafaa basi mke huridhia mke hana neno,

Mwanaume ndiye kaachiwa kadi ya benki kutoa na kupanga matumizi,

Mke hana tama ya kupenda vitu vya hali ya juu huwa mwanaume ndiye anaamua kumchukulia mke vitu vyenye thamani ila mke hataki, mke husema kama mume ataleta au kumnunulia sawa ila sio yeye.

Maswala mengi yanayohusu aina ya vitu, chakula na maisha yao mwanaume ana nafasi kubwa sana pamoja na kutokuwa na kipato,

Mwanamke kila atokapo kazini hufikia kumpa ripoti ya kazi alizozifanya na kipato alichokipata kwa siku hiyo, mke hana password kwenye simu mara nyingi humpa mumewe atumie simu yake na mumewake humpa mkewe simu yake atumie,

mke na mume hawana hata chembe ya siri ndani kwao, mume alipokuwa akifanya kazi alikuwa anamwachia mke walet kujua kuna hela ngapi, mfukoni mwa suruali mke hujua mume wake ana sh ngapi, mke alikuwa anajua benki mumewake ana sh ngapi na password zote anazijua mke


Wana JF nimeliona na nimeshuhudia nimeshangaa sana kwa mke kuwa na tabia hizo zaidi sana anajua mume hana kazi halafu amekataa kuwa msiri mwanaume anajua kila kitu hadi password zote za benki…

Hivi kweli wanawake kama hawa tunao wangapi. Ila huyu mwanaume sio kwamba kalelewa hapana au ameolewa hapana najiuliza je hili lawezekana kumpata mwanamke kama huyu.
ww siumeandika kuwa umeshuhudia sasa kwann unatuliza cc kama mwanamke kama huyo yupo wkt ww ushuhuda unao[emoji57]
 
Mwanaume miaka yote minne anapanga tu bajet ya pesa ya mkewe ni aibu
Haiwezi kuwa aibu kumbuka mkioana mmekuwa mwili mmoja na hakuna cha mtu mali yote ni ya familia yani ninyi na watoto wenu, mkianza tofauti kuwa mali hizi ni za mwanaume au mke hapo ndio mtafaruku huwa unaanza
 
Aiseeeee huyo ndo mwanamke wakupigia goti nakusema """" Asante sana Muumbaji Wa Mbingu na Nchi navyote viijazavyo dunia Kwa Kuniletea mwanamke aliyebaraka ktk maisha yangu".


Hapo unamtizama usoniii ,,unatabasam ,,unamkumbatia ,,unampiga busu kisha unamwambia *Nakupenda sana mke Wangu ,, mabinti wengi wamejitahidi ktk familia zao ,ila wewe Umewashinda wote *

Unamwongeza tena busu huku mikono yako IPO kiunon mwake nakumwambia " Muda Wangu huongezeka thaman niwapo nawewe".

Hapo kamama kawatu kanachekaaa ,,alafu kanaenda jikon, unapikiwa bonge lamsosi ,linanukia hatare[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji8]
 
Usinipe namba ya simu ya jamaa, nipe ya mdogo wake wa kike wa huyo mama,, haya mambo ni GENETICS.
 
Dah, ukipata mke kama huyu hutawaza kusafir kabsaaa
 
Tenda wema ulipwe wema
Mwanaume ukiwa na kazi unarudi asubuhi shat ndani nje

Kelele kejeli dharau zote zako
Halafu unategemea ukikosa uhudumiwe vyema ?
 
Back
Top Bottom