Hivi Kuna rapa wa kitapeli kama huyu jamaa

Hivi Kuna rapa wa kitapeli kama huyu jamaa

Mpaka sasa sijaweza kuamini kuwa hakuna aliyeandika jina lake!!!
 
Kitu kinachofanya hata Dunga mawe nayo nione ni ya kiwaki tuu , melody ya champion ndo hiyo hiyo ya dunga mawe
Hapo kidogo ndiyo kazingua na alivyoirudia tena kwenye Shida alifeli
 
Ufundi na utaalamu wa kucheza na maneno kwenye rap ni kitu cha kawaida na inaonesha ufundi wako wa uandishi,dogo yuko vizuri mi mwenyewe namkubali. Anauliza eti "hivi wanafunzi walevi ndio wanatembea na counter" 😁😁 na huo ndio utamu wa rap bablai
 
Ila huu mziki wa kufokafoka umetoka mbali.. zamani waimbaji walikuwa wanaonekana kama machizi au mazezeta hivi na wao walikuwa wanaona sifa..
😀😀LWP BIG DOG Pose , Manzese crew , King crazy Gk and the likes
 
Anakwambia

"Nshawai kumkuta steve mweusi kitambaa cheupe"

"Nalinda bustan yangu wasimuibe maua sama"

"Jela hakuna amani hata, uingie na frida"

"Mi niliwah kumkuta Joh Makini akifanya uzembe😂"

"Ukimuita Manara Haji"

"Nakunywa soda mbele ya shomari kapombe"

"Yaliyonitokea shekilango sitaki tena urafiki"
🤣🤣🤣 Nimecheka para ya mwisho
 
Anakwambia

"Nshawai kumkuta steve mweusi kitambaa cheupe"

"Nalinda bustan yangu wasimuibe maua sama"

"Jela hakuna amani hata, uingie na frida"

"Mi niliwah kumkuta Joh Makini akifanya uzembe😂"

"Ukimuita Manara Haji"

"Nakunywa soda mbele ya shomari kapombe"

"Yaliyonitokea shekilango sitaki tena urafiki"
Ongezea

Mganga analalamika hapati wateja amerogwa
 
Huyu jamaa mistari yake hapana

Utasikia

1) Wanataka nife Ili Aishi manula

2)Vyombo vya habari vinaoshwa kwenye besen

3) Hata wachawi wanajua mchawi pesa

4)Dirisha la usajili wameweka mapazia

5)Nanunua kanga mbele ya maulidi kitenge

6) Nimeongea na ndugu yangu anaitwa Maneno akasema Hana neno

7)Nimekosa pa kukaa nikakaa kimya

Hiyo ni baadhi tu ila itoshe kusema jamaa ni mmoja kati ya marapa wa kitapeli ambao Taifa limebahatika kuwa nao
View attachment 3554988
Haya tuambie ni nani tena huko Daslamu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom