Hivi kuna kitu kinaitwa Maadili ya Mtanzania?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna kitu kinaitwa Maadili ya Mtanzania??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SnowBall, Oct 10, 2012.

 1. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ukilitazama neno MAADILI kwa kiingereza linatafsirika kama 'ethics' au 'morals'...kwa wenye kujua kiingereza vizuri mnaweza kunisaidia kueleza kinagaubaga nini maana ya morals or ethics.. na wale wajuzi wa kiswahili mtaniambia..Ila kwa tafsiri yangu yangu ya kichina..nadhani inamaanisha mambo ambayo kimsingi jamii imekubaliana kwa pamoja kwamba yakifanyika yanaleta mwonekano mwema kwenye jamii..na hii inaweza kuhusisha namna ya kuvaa, kusalimiana..kufarijiana misibani nakadhalika.................

  Mada iliyoko mezani ni hii..Katika pita pita zangu za kimaisha hapa juzi kati nilibahatika kupanda daladala na ndani ya daladala kulikuwa na watu wa marika tofauti kuanzia wanafunzi na watu wazima wenye umri wa karibu miaka hamsini. Sasa basi mule ndani ya gari nilipaa na siti but kwa mbele yangu kulikuwa na watoto wa shule wawili wakike nadhani ni wa sekondari umri wa kati 15 na 16.walikuwa wamesimama huku wamebanwa na watu wazima...Sasa kwa kuwahurumia wale wadogo nikawaita na kuwaomba wakae kwenye siti yangu kwa kubebana..Of course kama nilivyosema kulikuwa na watu wazima wamesimama but my sense of humour fell on those poor small girls...

  Sasa wakati mie nimesimama nikasikia siti za nyuma watu wakilalamika kuwa 'Maadili ya Mtanzania yameshuka kwamba nawezaje kuwaachia wanafunzi wakae ilhali kulikuwa na watu wazima wamesimama'..Niliupenda mjadala lakini kwa kuwa nilishukia jirani sikujua uliishaje..Baadaye nikiwa zangu njiani nikaanza kujiuliza maswali..Hivi ni kweli kuna kitu kama maadili ya Mtanzania?..na kama yapo hivi yanafundishwa wapi??..Binafsi kwa kuishi kwangu..mara nyingi katika kufanya maamuzi ya mambo yanayonikabili natumiaga busara ya dini yangu na ikizidi kabisa basi nitaconsult wazee wa kabila letu au zaidi nayatafakari tu kwa upeo wangu mwenyewe na kufanya maamuzi..lakini ever sijawahi kujua yapi ni maadili ya Mtanzania..kiasi kwamba naweza kusimama na kujitambulisha nayo...

  Probably kama kuna mtu anayajua haya yanayoitwa..'Maadili ya Mtanzania'..hebu ajaribu kunielewesha basi!!..Manake kila kukicha tunalalamika watoto wa siku hizi hawana maadili..hivi ni kweli zamani yalikuwepo?? na ni kweli kwamba hayo ya zamani ndiyo yanamtambulisha Mtanzania??....lol!
   
 2. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kuna mila na desturi za kitanzania hamna maadili ya kitanzania.
  maadili ni ya Mungu tuu ambeye ndio muanzilishi wa maadili.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,104
  Trophy Points: 280
  maadili my asss***ssssssss.......
  hamna kitu kama hicho bongo.
  Usipofunzwa na baba yako, utafunzwa na SEGEREA
   
 4. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Maadili ya Mtanzania yamegawanyika katika makabila mbalimbali, kila kabila hapa kwetu lina maadili yake, hii ndiyo inareflect Tanzania kiujumla.
   
 5. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mh pacha leo umetoka kivingine leo!hii outing yako ya leo toka asubuhi mimi penda sana
  :focus:maadili ya kitanzania yapo
  kuna kitu kinaitwa mila na desturi,mila zinaweza kuwa ni za kikabila
  lakini desturi tunaweza kuwa nazo kwa kushare yani kama taifa
  kwa desturi zetu tukiwa ni watanzania desturi mojawapo ni wadogo kuanza kuamkia wakubwa,kusimama ili wakubwa wakae
  kunyamaza wakubwa wanapoongea
  kutokujibizana na waliokuzidi umri
  kunyamaza wakati wa kula
  na mengine meengi
  lakini hili la maadili kuwa yapo au hayapo na kilichofanya maadili hayo yasiwepo kwa kweli ni mada pana sana!
  ukimbuka malezi tuliyokulia zamani yalikuwa ni malezi funge yaani malezi ya jamii moja ndo mana kulikuwa na theory za wanawake wa mkoa huu wako hiiv ana wa kabila hili wako vile
  siku hizi watoto wetu tunawalea malezi huria,yaani ni mchanganyiko kwisha kazi!mtoto anazaliwa na mzazi mchaga na mngoni analelewa na housegirl mhehea u mmakonde!
  matokeo yake hata yale tulikuwa tunaamini ndiyo maadili ya kitanzania hayapo
  wakati sisi tulikuwa hatuwezi kuhoji amri za wazazi wetu na walimu au wakubwa zetu watoto wetu wanajiona wana hiyo mandate kuna kamsemo wanakatumia wenyewe mum/dad but its not fair
  jamii imeanza kulizoea hili tukiamini haya ndo maendeleo
  zamani mama anajifungua mtoto wa kiume na mtoto anakuwa treated kama mwanaume since then siku hizi unakuta mtoto wa kiume kasukwa nywele na kavalishwa bangili ,bado tunaweza kutembea kifua mbele kudai tuna maadili ya kitanzania?
  zamani tulikuwa tunaamini watoto wanauzwa hospitali au baharini siku hizi wanetu wameenda mbali zaidi muulize gfsonwin akiwa anafundisha biology anakuatana na maswali gani kwenye topic ya reproduction.
  wazazi siku hizi tumerelax sana kuhusu malezi,sana tumebaki kuwalaumu walimu na kina dada!
  tumewaachia uhuru hawa watoto kiasi cha kutisha kabisa!matokeo yake ndo hayo ya kutokujijua hata kama tuna maadili ya kitanzania au la!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  The difference between ethics and morals can seem somewhat arbitrary to many, but there is a basic, albeit subtle, difference. Morals define personal character, while ethics stress a social system in which those morals are applied. In other words, ethics point to standards or codes of behavior expected by the group to which the individual belongs. This could be national ethics, social ethics, company ethics, professional ethics, or even family ethics. So while a person's moral code is usually unchanging, the ethics he or she practices can be other-dependent.


  When considering the difference between ethics and morals, it may be helpful to consider a criminal defense lawyer. Though the lawyer's personal moral code likely finds murder immoral and reprehensible, ethics demand the accused client be defended as vigorously as possible, even when the lawyer knows the party is guilty and that a freed defendant would potentially lead to more crime. Legal ethics must override personal morals for the greater good of upholding a justice system in which the accused are given a fair trial and the prosecution must prove guilt beyond a reasonable doubt.
   
 7. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hizi mila na desturi ni universal??..mtu wa Kigoma anaweza kuziobserve kama alivyo wa Nachingwea?
   
 8. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo kama huna wazazi ni bora ukafungwe ndio utayapata maadili??
   
 9. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo my pacha wa kuachina ziwa snowhite unaamini zamani kulikuwa na maadili ya Mtanzania?...ryte?...sasa yameenda wapi?....Na mlifundishwa wapi hayo maadili?...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  I got your point buddy...but i still ask the same thing..do we have morals and ethics that qualify to be branded as Tanzanian morals in its generality???...
   
 11. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  malezi my pacha!malezi!
   
 12. s

  sarikoki JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Maadili ya Mtz ni Ufisadi.Tunapenda madili haoo.... hebu jifanye unataka kununua kitu alafu ndenda popote alafu anzakuuliza mtu yeyote utakayekutana nae wapi utanunua hicho kitu...nakwambia hamna mtu atakwambia hajui....hata kama unataka kununua ndege atakwambia anajua......
   
Loading...