Hivi kumchukia mtu bila sababu ni jambo la kawaida?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,368
50,737
Wasalam,

Labda nielezee kwa kutumia mifano hai miwili. Kuna huyu jamaa ni mtu mzima tu katika kupiga stori na wenzake namskia akisema kuwa hampedi diamond huyuhuyu msanii.

Mimi nikamuuliza unaanzaje kumchukia mtu ambaye hana athari za moja kwa moja na maisha yako? Akasema ooh hajui mziki borea alikiba.
Nikabaki nashangaa ina maana kila anayefanya kazi zake aidha za Sanaa au zozote kama hazikufurahishi ni lazima umchukie?

Wangapi wanafanya vitu ambavyo huna interest navyo lakini huna habari nao huwapendi wala huwachukii?Lakini inatokea mwingine hupendi kazi zake na jitihada anazofanya lakini inatokea na ye mwenyewe unamchukia.

Aina nyingine ya chuki nimeshangazwa nayo kuna binti nimekaa nae ofisini katika mazungumzo akapita mfanyakazi mwenzetu ni mgeni yule mdada akaniambia kuwa hampendi huyu jamaa?
Kwanini? Basi tu sina sababu
Inatokeaje unakuwa unamchukia homosapiens mwenzako tena bila sababu. nini kinaleta hisia hizo? Akili, maroho?

Eti wengine wanadai kuwa damu hazijaendana. Kuna ukwel hapo? Nini kinacontrol hisia za chuki? NI kawaida?
 
Last edited by a moderator:
sababu lazima iwepo....hata kama haina uhusiano na huyo anayechukiwa moja kwa moja....
 
Ni jambo la kisaikolojia lakini lazima lina sababu...
 
Huwa naamini watu ambao huwa wanawachukia wenzao wakisema hawana sababu ama damu hazijaendana wana maumivu ya ndani...maumivu haya hupelekea chuki na wivu usio wa msingi.Watu hawa mara nyingi ni wakosoaji sana na huwa hawaoni chema ndani ya mwenzao.Yaani akiona mtu kafanya kazi nzuri hatasema nzuri ataanza kuitafutia kasoro ama atasema hampendi flani kwa kuwa anajisikia sana ama anajiamini sana na hata hana mazoea naye..Watu hawa hujisikia vizuri watoapo kasoro hizo.

Kwa upande wangu huwa naona ni watu wanaotamani kuwa kama hao wanaowachukia ila hawawezi..hizo damu kutoendana ni kisingizio tu..waweza chunguza kwa nini huyo mfanyakazi hampendi mwenzie utakuta kuna vitu kamzidi.
 
Back
Top Bottom