Asikudanganye mtu kuwa Umaskini ni jambo la Kujivunia. Jaribu utajiri uone raha yake

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Ni kweli hamuwezi wote kuwa matajiri. Sisi wengine tunakuwa tuna wawakilisha ninyi ambao bado hamjafanikiwa kuzipata.

Utajiri wako uwe wa furaha na amani. Usiibe, Usidhurumu, Usipate kwa Waganga. Pata mali halali. Maskini hana Raha mchana wala Usiku.

Mchana Nzi usiku Mbu. Hamna jema maskini walalamishi, wanyonge na asilimia kubwa wanakuwa wanafiki na roho hiyo ikiendelea hata akizipata kidogo anakuwa bado mnafiki.

Maskini hapati muda wa kupumzika, maskini huwa analala hapumziki ukienda nyumba za matajiri tu ndio utasikia "BABA AMEPUMZIKA" maskini hapumziki analala. Na utakuta amelala bado anarusha mateke au mikono, bado unamwona anapiga makelele ukimuuliza anasema ameota ndoto mbaya.

Ni umaskini tu unaokufanya uote ndoto mbaya. Uote unakimbizwa,uote unakabwa, uote unachomwa moto au unapigwa.

Na sometimes unaota unakabwa na wachawi au majini no. hao ni watu wanaokudai wanakuwa na hasira mpaka wanachange na kuwa na sura hizo za kutisha.

Na hii hupelekea wakati mwingine ukorome n.k ni kwamba huko waliko wanakuwazia kuwa ungekuwa karibu kwa jinsi unavyowazungusha kulipa pesa zao wangekukaba.

Ukiangalia maskini analala huku bado amekunja sura. Analala huku mwili umegangamaa...sababu moyoni ana mambo mengi.

Maskini halali kupumzika.atapumzikaje sasa wakati ana mambo elfu moja hakuna alilotatua? Na wakati mwingine anapotatua hili anatengeneza tatizo lile.

Ndo maana huota ndoto mbaya mbaya... unakimbizwa,watu wanataka kukuua, upo makaburini,sometimes unaota umekufa.ndiyo ni kama upo hai lakini umeshakufa. Huna mchango kwa family wala Taifa.

Huwezi mkuta tajiri anakunywa pombe ili alewe asahau sijui nini. Tajiri anataka akumbuke kila kitu. Anataka akumbuke hata alichoongea jana.so hawezi akalewa ili asahau.

Maskini wanalewa ili wasahau shida zao, halafu baadaye au kesho wakiamka wanakutana nazo tena. Ndo maana wanakuwa na husda, chuki, wivu, majungu, unafiki na roho mbaya. Hawa wana umaskini hadi kwenye akili.

Kuna wengine ni matajiri ila wamechelea tu kuzikamata. Hawa utaona tofauti yao.huwa wanapambana, wana upendo na wanasaidia. Ni Upcoming BILL LUGGIE hao.

Watu wenye pesa hupumzika.na hawa hupumzika kwa amani kuanzia hapa hapa duniani. Hawalali. Wanapumzika.

Wanalala usingizi mtulivu.utamwona mtu kalala huku anatabasamu.mwili umeachia ume relax.

Hana mawazo,hana ndoto mbaya, unajua tajiri hashindwi kulipa deni?huwa anachelewa tu ila anajua atalipa.

Ushauri wangu. Tutafute pesa ili tuwasaidie Maskini. Tusiwatese tusiwanyanyase. Mungu anatupa sisi ili tusaidie Waja wake. Usinichukie sababu mimi nina pesa. Nimezitafuta kwa kile nlichopewa.
 

Mithali 14:20​

Maskini huchukiwa hata na jirani yake, lakini tajiri ana marafiki wengi.

Mithali 19:7​

Maskini huchukiwa na ndugu zake; marafiki zake ndio zaidi: Humkimbia! Hata awabembeleze namna gani hatawapata.

MASIKINI NI MTAJI WA WANASIASA
wanyonge😀😀😀
 
Hizi fact watu masikini huwa awapendi kusikia.. wanapenda story za shida shida furaha yao ni vile mkiwa wenye shida wengi.
 
Back
Top Bottom