Hivi kukaa bondeni ni kosa?

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,322
Wakuu, Tumesikia na kuona live ama kupitia vyombo vya habari kuwa wanaokaa mabondeni wanatakiwa kuondoka kwa hiari au kwa mabavu, hii ni kutokana na athari za mafuriko yaliyotokea hivi karibuni, je kukaa bondeni ni kosa kisheria hata watanzania hawa masikini watishiwe kufurushwa? naomba mchango wako.
 
Mi nadhani ni kosa la serikali iliyo ruhusu urbanisation hapo, sio kosa la wakaaji.
Hata hivo kwa serikali ya kuwajibika hakuna ubaya, waweke tu drainages za ukweli.
Hollang iko sea level or under sea level ila serikali umejenga water canals, na inahakikisha pumps zinatoa maji kila wakati.
Kwa hiyo kukaa bondeni sio kosa kama serikali itawajibika.
 
Kwa maana hiyo serikali yetu haiwajibiki kwa wananchi! inawajibika kwa nani?
 
she didn't say haiwajibiki kwa waninchi... the question was: je ni kosa kujenga bondeni? she said sio kosa, kama serikali itawajibika.

So wait and see.
 
Wakuu, Tumesikia na kuona live ama kupitia vyombo vya habari kuwa wanaokaa mabondeni wanatakiwa kuondoka kwa hiari au kwa mabavu, hii ni kutokana na athari za mafuriko yaliyotokea hivi karibuni, je kukaa bondeni ni kosa kisheria hata watanzania hawa masikini watishiwe kufurushwa? naomba mchango wako.
Kukaa mabondeni siyo kosa kisheria, ni sawa na kunywa maji yasiyo safi na salama pia sio kosa kisheria ila ikitokea watu wengi wakaanza kufa kwa maradhi yatokanayo na kunywa maji machafu Serikali yaweza kuingilia kati hata kwa mabavu
 
we endelea tu kukaa huko huku ukisubiri jibu sahihi.sio kosa:eyebrows:
 
Ku2muliwa na vizur ili kuepuka Unnecessary costs coz the areas ar highly prone of Floods!
 
Kukaa mabondeni siyo kosa kisheria, ni sawa na kunywa maji yasiyo safi na salama pia sio kosa kisheria ila ikitokea watu wengi wakaanza kufa kwa maradhi yatokanayo na kunywa maji machafu Serikali yaweza kuingilia kati hata kwa mabavu

Hata hivyo serikali itapaswa kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kisha kuwashawishi wananchi kuyaepuka maji machafu kwani maji safi yapo, KWA KIPINDI MAJI SAFI HAKUNA, WANANCHI WATALAZIMISHWA KUCHEMSHA MAJI, NA SI KUZUIA KUYATUMIA MAJI PEKEE AROUND.
 
Mbna pakistan,india,japani kuna mafuriko tena wanakufa maelfu ya watu hapa 20 tu mmekufa mnalalama
 
Jamani! Sio kila kitu ukimbilie kusema ni kosa au sio kosa kisheria! Kukaa pale ni sawa na mtu anayeplan au anacommit suicide! Kwani wale wazarama hawakuyaona hayo mabonde miaka ya nyuma! Wao wakajenga magomeni mapipa, makuti,mwembechai na kuendelea,sasa mtu anatoka bush na hela zake anaona kawahi pale faya! Eti karibu na mjini! Ukimuondoa mtu anaeplan kujiua akipona unaweza kumshtaki! Pale ni hatari kwa maisha yao hilo halina ubishi tuache ligi!
 
Mkuu hatufanyi ligi, kusingekuwa na maana ya kuwa na sheria kwa mtazamo wako. nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria, kumbuka kwa reginald mengi maji yalijaa na kuhatarisha maisha, kwa said mwema pia maji yalitinga, godown la kajima maji yalifurika, klabu ya yanga iliathirika, sihitaji ubishane weka facts za uwepo wa sheria katika utekelezaji wa zoezi zima. kumbuka magari yanafanya ajali kila siku na kusababisha vifo vingi sana, kwa takwimu mafuriko yameua watu hawafiki elfu moja kwa miongo mitano nchi nzima, niambie magari yamechinja wangapi! lini angalau serikali ilifikiri kupiga marufuku matumizi ya magari zaidi ya kuboresha matumizi hayo kwa kuamuru mabasi yafungwe vidhibiti mwendo, kuhakikisha kuwa kila abiria anafunga mkanda, magari ya mizigo hayaruhusiwi kupakia abiria n.k. iweje hawa ndugu zetu wanaoitumia ardhi ambayo katiba imewatambua watiwe msukosuko kisa mafuriko?
 
Wakuu, Tumesikia na kuona live ama kupitia vyombo vya habari kuwa wanaokaa mabondeni wanatakiwa kuondoka kwa hiari au kwa mabavu, hii ni kutokana na athari za mafuriko yaliyotokea hivi karibuni, je kukaa bondeni ni kosa kisheria hata watanzania hawa masikini watishiwe kufurushwa? naomba mchango wako.

Siyo kosa...ili mradi uwe unalipa kodi.
 
Mimi nadhani sio kosa kukaa mabondeni, ila serikali inapoona kuna hatari kwa binadamu kuishi huko inaweza kutumia mabavu kuwaondoa(japo sina hakika kama kuna sheria inayoilinda serikali kufanya hivyo).
 
kwa kuwa si kosa, nguvu zatumika kwa maelekezo ya sheria ipi?

Mkuu kwa hiyo ukishaambiwa kuwa sheria ipo ndo utaondoka bondeni?
Mimi nadhani, ni wajibu wa serikali kuchukua hatua madhubuti regardless kuwa sheria ipo au haipo ikionekana kuwa kuendelea kukaa bondeni kutaathiri raia wake. Ni wajibu wa serikali kutoa security kwa raia wake inapobidi hata nguvu ya dola yaweza kutumika.
 
Mkuu hatufanyi ligi, kusingekuwa na maana ya kuwa na sheria kwa mtazamo wako. nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria, kumbuka kwa reginald mengi maji yalijaa na kuhatarisha maisha, kwa said mwema pia maji yalitinga, godown la kajima maji yalifurika, klabu ya yanga iliathirika, sihitaji ubishane weka facts za uwepo wa sheria katika utekelezaji wa zoezi zima. kumbuka magari yanafanya ajali kila siku na kusababisha vifo vingi sana, kwa takwimu mafuriko yameua watu hawafiki elfu moja kwa miongo mitano nchi nzima, niambie magari yamechinja wangapi! lini angalau serikali ilifikiri kupiga marufuku matumizi ya magari zaidi ya kuboresha matumizi hayo kwa kuamuru mabasi yafungwe vidhibiti mwendo, kuhakikisha kuwa kila abiria anafunga mkanda, magari ya mizigo hayaruhusiwi kupakia abiria n.k. iweje hawa ndugu zetu wanaoitumia ardhi ambayo katiba imewatambua watiwe msukosuko kisa mafuriko?

nielewe mkuu! Magari ni utaratibu wake kubeba watu! Na huko kwa akina Mengi kujaa maji inatokana na furry of nature,kama vile elnino,sunami n.k,lakini maeneo waliopo sio hatarishi kama mabonde ya jangwani,mto msimbazi,bonde la mkwajuni n.k hakukuwa na nyumba kule! Wala mipango miji hawakuwagawia hao watu ardhi hiyo! Wamekwenda kwa shida ya ardhi ya kukaa karibu na town! Ndn hapo tunaposhindwa kwenda sawa! Kuwa pale ni kuhatarisha maisha yao kwa makusudi kabisa mkuu. Nawahi bar!
 
Back
Top Bottom