Hivi kuendelea kuvaa wigs kwa majaji na maspika wa mabunge ya Kenya siyo ukoloni wa kujitakia?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720
Wanangu hamjambo humu ugani? Leo nimeona bi mkubwa SSH alipohutubia mabunge ya Kenya maspika alikuwa wamevalia wigs. Je, kweli bado kuna haja ya waswahili kuvaa katani na kudai bado wako huru? Wanangu nisaidieni.

Pia hata majaji wa Kenya huvaa wigs. Kipindi cha Dr Willy Mutunga yalipigwa chini yakarejeshwa na David Maraga. Je, tuwasaidieni hawa waswahili wenzetu pamoja na kujidai wamesoma sana wakati si kweli?

Wakenya na waswahili wengine wote wanaoendelea kuvaa wigs mnatuaibisha na kutuonyesha kama watumwa wa kujitakia.
 
Kuna mtu alishawahi niambia kwamba wigi za majaji zinaongeza IQ na busara kwa kichwa lakini zile za bibi na dada zao ni kama helmet au kofia na mwamvuli wa kuzuia jua.

Ilikuwa Nairobi, 2008
Uongo na upuuzi mtupu. Ingekuwa hivyo, maprofesa wangeyavaa kweli kweli. Waangalie wavaa wigs vizuri.
 
Ni ushamba tu na zaidi sana kasumba za kikoloni. Lakini hata hawa dada zetu waache kuunganisha makatani na mawigi ya kihindi vichwani, ni ushamba pia!😫
 
Julius Malema pia alishawahi kuwatolea mfano akiwaambia bado wana hisia za kutawaliwa na Mkoloni.
 
Back
Top Bottom