dr kashmir al ibadi
Member
- Oct 19, 2015
- 14
- 8
Habari zenu
Naomba msipate tabu na neno Dr kwenye ID yangu, ni jina tu
Mwaka 2005 nilipata ajali mbaya ya Gari nikiwa safarini kikazi, nilivunjika sehemu mbali mbali za mwili, nilikaa muhimbili karibu mwaka mzima, shirika nililivunja mkataba na mm walini terminate baada ya kujiridhisha kwa vigezo vyao kuwa siwezi kumudu tena kazi, nikapewa malipo yangu yote, hayakua makubwa sana, maana nilianza kazi 1999, pia nilikua na mkopo nilichukua kujengea nyumba, walitumia mafao yangu kulipia huo mkopo, nilibaki na kiasi kidogo sana cha fedha
Mke ni mwalimu wa sekondari, na tulikua na watoto wawili hadi hapo napoteza ajira, mkubwa miaka 4 na mdogo mwaka mmoja, ilipofika 2008 nilikua nimepona kabisa, watu walionizunguka hawakuamin kabisa muujiza huo, changamoto iliyonikabili baada ya kupona ni kukosa kazi, nilihangaika bila mafanikio nikipanda ghorofa kwa ghorofa na vyeti vyangu
Wife akaanza visa, kwamba nimekuvumilia na kukulisha tangu 2005 ulipopata ajali, sasa umepona siwezi kukulisha tena, kama hupati kazi hilo sio tatizo langu, nenda hata kabebe zege au kasukume toroli ulete matumizi""
Nilishangaa sana kwa Maneno Yale, maana alijua wazi sikua naruhusiwa kubeba vitu vizito,
2010 nilikua bado sijafanikiwa kupata kazi, wife akaanza kurudi usiku mwingi, akiwa kanywa pombe, na akifika hataki kuguswa, tulikua tunakutana pale anapotaka yeye tu, weekend mzima hashindi nyumbani, kwa kifupi dharau zilikua nyingi mno, lakini nilivumilia, nikasema ipo siku mungu ataniinua tena
2011 nilipata msaada kutoka kwa shemeji yangu alieoa Dada yangu tumbo moja, yeye ni mkulima wa kati siku nyingi, analima mchele na mahindi sengerema vijijini, akanipigia simu niende sengerema ana mazungumzo na mm, kumbe mama yangu alishakwenda kumuona mwezi nyuma na kumuomba anisaidie
Alinigawia sehemu kubwa ya kulima kama heka nne hivi, alinipa mtaji wa kilimo milioni 5 yy ndie aliesimamia zoezi la kulima heka hizo, kusia mbegu, na kupanda, na kuwalipa watenda kazi yy mwenyewe, nilikaa huko shambani miezi mitatu, nilimficha wife kuhusu suala hilo
Alikua tu anashangaa mwezi huu nipo, ujao sipo dar, hivyo hivyo hadi nilipovuna na kuuza, awamu ya kwanza nilipata 13m nilizirudisha zote kwenye kilimo msimu uliofuata, na awamu ya pili nikapata 19 milioni, nimeendelea hivyo hadi sasa napata pesa za kuridhisha, hiyo ni kutoka 2011 hadi sasa, 2015, kwa kipindi chote hiki nime pretend kuishi kama vile sina kitu, ila matumizi ndani natoa na nikawa nalipa shuleni kwa watoto ada,
Mwaka huu, nimefanya makubwa zaidi, nimeizungushia nyumba ukuta na Geti, nimetoa nyavu na kuweka aluminium glass, nimenunua Gari ndogo na mengine mengi, nimetafuta msichana mzuri pembeni ( Mariana) mwenye adabu na Upendo, siogopi kutaja jina lake maana sio siri
Wana Jf kwa kawaida Dereva mzuri ni lazima arudi reverse, ataendesha wee lakini kuna pahala atalazimika kurudi reverse, sasa wife, ghafla bin vuu ameanza kuona wivu, kwamba mbona unarudi saa saba usiku unatoka wapi,!! Anaanzisha fujo usiku kucha, kesho yake mm narudi alfajiri kabisa au nalala huko huko kwa mariana , naondoka Friday narudi Sunday namkuta analia kama mtoto mdogo, nawapakia watoto wangu garini nawapeleka beach jioni tunarudi wakiwa wamefurahi
Ametafuta namba ya Mariana kwenye simu yangu hadi akaipata, sasa hivi anamtukana na kwenda kumfanyia fujo kila siku, weekend iliyokwisha nimeitwa kwenye kikao cha usuluhisho, baada ya wife kwenda kushtaki kwa wazee wake, huko nyuma wakati akinisumbua niliwahi kushitaki kwao walikua wakinipuuza, sasa juzi nimewajibu its pay back time, nikaondoka
Nataka kumuondoa kwangu niachane nae kabisa nilete Mariana ndani, watoto nitabaki nao, kama atangangania kugawana Mali nipo tayari kumuachia nyumba na watoto kama atataka, nitaenda kupanga huku nikimalizia nyumba yangu nyingine iliyopo kwenye linta,
Ingawa mama yangu mzazi ameniomba kumsamehe lakini sioni kama hilo linawezekana, amenitendea mambo mabaya sana ikiwemo infidelity ambayo kwa vyovyote ilifanyika kutokana na ushahidi wa kimazingira, sikutaka kumfumania wala kumfuatilia niliogopa kuumia zaidi moyoni, huwa sina kifua hicho
Wana Jf naomba kuwauliza katika yote Haya kosa langu ni nini hasa?
Nina kosa lolote hapo?
Naombeni mnisaidie