Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,766
- 894
Hahahahaha hapo kwenye blue ndugu yangu mbavu sina:sorry:...nikiwa darasa la pili (mwaka Ninteen Kweusi!), tulikuwa tunatakiwa kwenda shule SAA TANO mchana. Siku hiyo wanafamilia wote walikua wametoka (nilikuwa naishi kwa bibi yangu). Baada ya maandalizi mengine yote sikuweza kuona mafuta ya kupakaa (kupaka?). Ikabidi nipekue ndani ya begi la mama yangu mdogo nikakuta kichupa kidogo cha rangi ya blue/kijani hivi. Nilipofungua nikaona kun amafuta nikapakaa toka kichwani hadi miguuni.
Punde si punde nikaanza kujisikia joto lilichnaganyika na msisimko wa mwili pamoja na harufu nzito. Kwa kuwa nilikuwa nimeshachelewa shule nikatoka vivyo hivyo mbio kwenda shule (kama kilomita moja hivi toka nyumbani). Nilipofika nilikuwa nimesweat kupita kiasi na bado nikisikia joto/msisimko na harufu nisiyoijua. Nilipoingia darasani mwalimu wa somo alikuwa ameshaanza kufundisha. Alipona hali niliyokuwa nayo akanisimamisha akauliza kulikoni? Mimi nikaishia kuomba msamaha kwa kuchelewa kuingia darasani. Akanichukua kunipeleka kwenye bomba la maji la shule kuninawisha-nikaja kuelewa baada ya kumsikia akiongea na walimu wengine kumbe nilikua nimepakaa VICKS KINGO nikidhani ni mafuta ya kupaka!!!
nakumbuka nilikuwa darasa la tatu nilienda kumtembelea shangazi yangu wakati wa likizo. jioni moja alipika maandazi na akasema hakuna kula tutanywea chai asubuhi, ilipofika usiku mimi na binamu yangu tukapanga kuiba. ilipofika usiku watu wote walikuwa wameshalala, beseni la maandazi liliwekwa juu ya kabati jikoni sasa tukaanza kubebebana ili tuchukue maandazi, mimi nilichuchumaa binamu yangu akawa ananikanyaga mabegani ili apande juu avute lile beseni achukue maandazi, baada ya kuvuta lile beseni mimi huku nilikuwa nimeshachoka nikatikisika kidogo yeye akayumba na kudodosha lile beseni halafu lilikuwa la bati... basi kishindo cha beseni kilisikika nyumba nzima, shangazi akashituka akauliza mnafanya nini?
alipoamka akatukuta tunahangaika kukusanya maandazi.. alichosema tutaonana kesho akaenda kulala...
kilichoendelea asubuhi nyie acheni tu..........
mimi nakumbuka nilchukuliwa na aunt yangu kwa lengo la kunisomesha maana familia yangu ilkua duni walkua matajiri sana lakini baada ya kuhamia kwake cha moto nilikiona maana nilkua house girl wa familia......... nilkua nawapikia watoto wake japo walkua wakubwa kwangu, nawafulia, nafanya usafi nyumba kubwa ya kifahari ikifika saa ya kuosha vyombo napanda juu ya kiti ili nifkie sink maana nlkua mdogo sana ikifika saa ya kula niko hoi hata kula siwezi nasinzia tuuu.....................................
jamani sitamani kuwa mtoto hata kidogo