Hivi Kingunge Ngombale Mwiru alihudhurua mazishi ya Nyerere?

Inaweza kuhisiwa kuwa baadhi ya watu ni public figures kumbe sivyo bali ni myth tu zinazoisumbua jamii!

Kuna swali au maswali ningependa kuyaelekeza kwa great thinkers au wanaJF wakongwe.

1.Hivi huyu mzee anayeitwa Kingunge alihudhuria mazishi ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere?

2.Kama alihudhuria jee alipewa nafasi gani kwenye mazishi?lets say alihutubia au aliweka shada la maua?

3.Na kama hakupewa fursa yoyote kwenye mazishi hayo ...ni kwa nini?

4.Je ni upi uhusiano wa Mwalimu na Kingunge nyakati za mwisho wa maisha ya mwalimu?

5.Je anastahili(ana moral authority) kuwa mmoja wa 'watoa kauli' za busara ndani ya chama baada ya Mwalimu kututoka?

Nitaongeza maswali zaidi kadri mada itakavyoendelea.

Angepewaje nafasi ya kuhutubu/kuweka shada la maua wakati Mazishi ya Mwalimu Nyerere yalifuata taratibu zote za kidini(katoliki)!? Hivi si ni Kingunge huyu huyu amejitanabaisha kuwa ni mpagani asiye na dini!?
 
hii ndio mada ya great thinkers?
nani walienda kutoa updates za hali ya Mwalimu London?
nani walienda kuuleta mwili Mwalimu alipofariki?
 
Kingunge kweli alikwenda London kumuona mwalimu baada ya kutumwa na Mkapa; hata hivyo enzi za uhai wake mwalimu hakumuamini sana huyu mzee na ndio maana katika harakati zake za siasa alikuwa na kinyongo kwanini hakuteuliwa kuwa katibu kuu wa chama !!!! Kinyongo cha kuukosa ukatibu mkuu wa chama Kingunge anacho mpaka atakapoingia ahera!!!
una uhakika na hayo au una argue kwa hisia?
wewe kwako cheo kikubwa serikalini na chamani ni ukatibu mkuu wa Chama?
 
1.Ilikuaje rais Mkapa kumteua mtu asiye mcha Mungu kumwangalia mgonjwa? Iliwezekanaje? Hapakuwa na wacha M,ungu waaminifu wa kukaa na kumtia moyo mgonjwa?
2.Ilikuaje mtu mjamaa kama Kingunge akubali na kushiriki kumpeleka Mwl.kutibiwa Uingereza,nchi ya kibepari badala ya China/Urusi aliyopendekeza yeye mwalimu? How was it possible?

NB;Niko mbioni sana kukubali kuwa Mwalimu Nyerere hakufa kifo cha kawaida,labda kiliharakishwa kwa makusudi au kwa uzembe na kupuuzia.
Niko mbioni kumwelewa Vicent Nyerere na Makongoro Nyerere.
unamzungumzia mungu yupi? na serikali ilikuwa ya dini gani kiasi cha kuteua wacha mungu wa hiyo dini?
 
una uhakika na hayo au una argue kwa hisia?
wewe kwako cheo kikubwa serikalini na chamani ni ukatibu mkuu wa Chama?
Yaani kwa maelezo aliyopost huyo jamaa ni kuwa 'nongwa' yote ya Kingunge hadi 'kuuasi' ujamaa alioapa kufa nao na kuingia kwenye ubepari wa 'design' ya ufisadi umetokana na 'hasira' zake za kuukosa Ukatibu mkuu wa Chama chake cha Magamba?!
 
Kuungana na Nyerere wakati wa kupigania uhuru haina maana kwamba Kingunge hawezi kubadilika. Always human being is an unpedictable organism. Kwa hiyo usijidanganye eti kwa kuwa alishiriki na Mwalimu kwenye harakati za ukombozi basi anabaki ni msafi. Kumbuka Yuda Iskarioti alikuwa mfuasi mzuri na mtu wa karibu wa Yesu lakini haikumzuia kumsaliti Yesu
Nimezipenda comments zako.

Umempasha vilivyo huyo jamaa aliyeamua kumkingia kifua kwa nguvu zake zote huyo mzee mvaa Cho en lai, ambapo mavazi yake hayo hayaendani kabisa na matendo ya waasisi wa vazi hilo.
 
Ninachokumbuka, Kingunge alipokwenda St Thomas alikaa muda wote na Mwalimu na ndipo Mwalimu alipokata roho. Na Mkapa alimteua kwenda kule ninadhani haikuwa kwa sababu ya ukaribu na Mwalimu, Ukuu wowote ama umaarufu kwa taifa bali ilikuwa ni tabia ya Mkapa kutokuwa na Imani ya Mungu. Aliamiini katika ukwetu na maarifa ya uhomeboy zaidi ukizingatia mzee ni kiongozi maarufu wa wachawi kiasi cha kkuwawakilisha hadi kwenye BMK.

Kwa ninachokikumbuka mimi ni kwamba alikwenda kule kwa utashi wa Mkapa na si utashi wa taifa wala Mwalimu. Lakini pia role yake iliyoifanya kwenye msiba ilikuwa ni kukata Roho kwa Mwalimu mbele yake. Na mara ya mwisho kuonekana kinagaubaga na wakati anashuka kwenye ndege akitoka London alikokwenda sijui kusimamia ama kushuhudia alichokishuhudia au kukisimamia.

Hajawa na hekima wala maarifa yoyte kwa taifa labda kwa Mkapa ndiye anajua zaidi. Lakini pia ndiye mmoja wa waliomweka JK madarakani na sasa anampigania Lowasa watu ambao Mwalimu hajawahi kuwakulbali. Na sikuwakubali tu bali pia wamedhihirisha uharibifu wa hali ya juu na kuagamiza taifa.


Ni prominent figure wa Team lowassa au prominent figure wa kitaifa au ni prominent figure wa ccm,???

Mkuu umeyasoma maswali yangu yaliyotokana na swali moja?

Mkuu jaribu kutulia na uje na majibu.

Ninakushauri upunguze ushabiki au jokes ...

back to topic!!!
 
Inaweza kuhisiwa kuwa baadhi ya watu ni public figures kumbe sivyo bali ni myth tu zinazoisumbua jamii!

Kuna swali au maswali ningependa kuyaelekeza kwa great thinkers au wanaJF wakongwe.

1.Hivi huyu mzee anayeitwa Kingunge alihudhuria mazishi ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere?

2.Kama alihudhuria jee alipewa nafasi gani kwenye mazishi?lets say alihutubia au aliweka shada la maua?

3.Na kama hakupewa fursa yoyote kwenye mazishi hayo ...ni kwa nini?

4.Je ni upi uhusiano wa Mwalimu na Kingunge nyakati za mwisho wa maisha ya mwalimu?

5.Je anastahili(ana moral authority) kuwa mmoja wa 'watoa kauli' za busara ndani ya chama baada ya Mwalimu kututoka?

Nitaongeza maswali zaidi kadri mada itakavyoendelea.

Tarehe 28.09.1999 Mzee kingunge akiwa waziri wa tawala za mikoa aliteuliwa kwenda ST thom hospital kwa ajiri ya kutoa taarifa rasmi juu ya ugonjwa wa baba wa taifa hiyo ni baada ya kusemwa kwamba taarifa zinatolewa holela,nakumbuka yeye na Mzee kawawa walifanikiwa kuwa miongoni mwa waliomshuhudia marehemu hospital.

baadhi ya majibu ya maswali yako tunaweza kutumia lojiki kujibu unless aje mtu na majibu sahihi.

1, 2 & 3 .Akiwa waziri,katibu mwenezi wa CCM wa zamani na mkongwe wa siasa ukiongeza na umuhimu wa yeye kusafirishwa kwenda Uingereza inawezekana kabisa alikuwepo kwenye mazishi Dar au Butiama.Shada la maua tusubiri wenye kumbukumbu sahihi lakini tukumbuke japo,yalikuwa mazishi ya kitaifa na pia viongozi wa kimataifa walikuwepo,so kupewa au kutokupewa nafasi kwa mawaziri wa TZ nadhani sio issue.

4. kuna sehemu nimemsoma kingunge anakiri aliwahi kufukuzwa ukuu wa mkoa baada ya kutofautiana na nyerere kwenye maswala furani, uhusiano wa wawili hao mara ya mwisho inawezekana haukuwa mbaya na ndio maana alitumwa Hospital kuwa naye.

5.Kwa ukongwe wake wa siasa na kama katibu mwenezi wa zamani anafaa kuwa moral authority wa CCM ila kwa sasa wa TZ wameelimika sana, akiwa wrong atapambana na upinzani wa hoja tu. Nakumbuka mimi nilivyokuwa nasoma tulikuwa tunaimbishwa ''zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM,Nyerere na Jumbe wadumu'' na tukaamini hakuna mtu anayeweza kufikiria tofauti na wakubwa hawa lakini leo tunashuhudia hata huo muungano wenyewe unahojiwa.

Nimechagiza tu, najua utakapokuja na sababu za maswali yako tutajifunza zaidi, karibu.
 
inaweza kuhisiwa kuwa baadhi ya watu ni public figures kumbe sivyo bali ni myth tu zinazoisumbua jamii!

Kuna swali au maswali ningependa kuyaelekeza kwa great thinkers au wanajf wakongwe.

1.hivi huyu mzee anayeitwa kingunge alihudhuria mazishi ya mwalimu julius kambarage nyerere?

2.kama alihudhuria jee alipewa nafasi gani kwenye mazishi?lets say alihutubia au aliweka shada la maua?

3.na kama hakupewa fursa yoyote kwenye mazishi hayo ...ni kwa nini?

4.je ni upi uhusiano wa mwalimu na kingunge nyakati za mwisho wa maisha ya mwalimu?

5.je anastahili(ana moral authority) kuwa mmoja wa 'watoa kauli' za busara ndani ya chama baada ya mwalimu kututoka?

Nitaongeza maswali zaidi kadri mada itakavyoendelea.
huyu mzee ni best of the best wa the late mwalimu.
Ni komredi..vyema uulize....mandela alikuwa close sana na mwl. Lakini hakuruhusiwa kuja msibani......
'ukishakuwa mtu mzima utaelewa."
 
Mkuu, hilisikua nalikumbuka kabisa though ule msiba since day 1 amegundulika mzee alikua anaumwa hadi mipango ya safari to St Thomas nilikua nafuatilia; nakumbuka Makongoro Nyerere alikua bado yupo NCCR Mageuzi na hakua na nauli ya kwenda kumuona baba yake, profesa maji marefu ndiye alie finance safari yake.

NCHI Hii bana ni kweli Siku zile Makongoro alibaniwa sana PESA Baada ya kwenda upinzani walimkatia Hadi Maji na umeme ambao Kabla alikuwa akilipiwa na jeshi ...Sasa kwa kuwa jeshi lilikuwa halijalipa Hadi anaacha kukawa na malimbikizo ....hawa kukata Hadi alipojiunga NCCR
 
Yaani kwa maelezo aliyopost huyo jamaa ni kuwa 'nongwa' yote ya Kingunge hadi 'kuuasi' ujamaa alioapa kufa nao na kuingia kwenye ubepari wa 'design' ya ufisadi umetokana na 'hasira' zake za kuukosa Ukatibu mkuu wa Chama chake cha Magamba?!
nipe mjamaa hata mmoja aliyepo ugambani au Upinzani!
 
NCHI Hii bana ni kweli Siku zile Makongoro alibaniwa sana PESA Baada ya kwenda upinzani walimkatia Hadi Maji na umeme ambao Kabla alikuwa akilipiwa na jeshi ...Sasa kwa kuwa jeshi lilikuwa halijalipa Hadi anaacha kukawa na malimbikizo ....hawa kukata Hadi alipojiunga NCCR
lete hiyo bili tuone. au unaandika kwa akili ya kushiba kiporo?
 
wakuu huyu mzee kingunge kazeeka sana sasa na ndio maana hata mawazo na matamshi yake yamekuwa tata wakati wote.

Kuna wakati fulani amekuwa akimuumiza hata huyo anayempigania apate u rais, mfano watanzania wote hawakuwai kubaini kama kuna watu wamekosana na inawalazimu wakutane ili wapatane na ikibidi kama wao imeshindikana basi waite watu wazzima ili wawapatanishe!

Wajumbe wa mkutano mkuu na nec walikwisha aminishwa kwamba hawa watu ni ma swaiba sasa sijui nini kitatokea hapa.

Leo kaja na hili la mangulah, kasahau mwenzie ni makamu mwenyekiti na yeye ni mstaafu, hivi ni nani mwenye mamlaka kwa sasa kuongelea taratibu za chama?

Ni vyema wazee kama yeye waka kaa kimya ili wasichanganya watu.
ikulu sio ya babako
 
Hii kauli ya Madaraka Nyerere, iliandikwa kwenye gazeti la Jamhuri mwaka 2012.


Nakumbuka maneno ya Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru, tuliyekuwa naye London siku Mwalimu alipofariki. Aliniambia mimi na kaka yangu Makongoro kuwa kifo cha Mwalimu kinatufanya sisi sasa kuwa watu wazima kwa sababu tunabeba majukumu ambayo hatukuwa nayo hapo awali. Alisema, “Watu walipofika nyumbani walikuwa wanamuulizia Mwalimu. Lakini leo hii wakifika nyumbani watakuulizia Madaraka au Makongoro.” Na wengine, ambao hakuwataja Mzee Kingunge.
baada ya kunukuu hiyo kauli, nini maoni yako?
 
Back
Top Bottom