Credible Viewer
JF-Expert Member
- May 22, 2015
- 444
- 117
Inaweza kuhisiwa kuwa baadhi ya watu ni public figures kumbe sivyo bali ni myth tu zinazoisumbua jamii!
Kuna swali au maswali ningependa kuyaelekeza kwa great thinkers au wanaJF wakongwe.
1.Hivi huyu mzee anayeitwa Kingunge alihudhuria mazishi ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere?
2.Kama alihudhuria jee alipewa nafasi gani kwenye mazishi?lets say alihutubia au aliweka shada la maua?
3.Na kama hakupewa fursa yoyote kwenye mazishi hayo ...ni kwa nini?
4.Je ni upi uhusiano wa Mwalimu na Kingunge nyakati za mwisho wa maisha ya mwalimu?
5.Je anastahili(ana moral authority) kuwa mmoja wa 'watoa kauli' za busara ndani ya chama baada ya Mwalimu kututoka?
Nitaongeza maswali zaidi kadri mada itakavyoendelea.
Angepewaje nafasi ya kuhutubu/kuweka shada la maua wakati Mazishi ya Mwalimu Nyerere yalifuata taratibu zote za kidini(katoliki)!? Hivi si ni Kingunge huyu huyu amejitanabaisha kuwa ni mpagani asiye na dini!?