Ni Swali zuri amabalo linahitaji mjadala mpana sana,
Kwanza mimi ninaweza kujibu hilo kwa kuangali pande mbili yaani Chanya na Hasi.
Chanya
Siyo kwamba Kikwete hakuna kitu amabacho hawezi, kuna mengi kama akiamua kuwa na uthubutu wa kukemea na kuyasimamia,anaweza kufanya maajabu makubwa katika kulilitea hili taifa maendeleo maaan kila kitu kipo kuanzia Mbuga za wanyama, maziwa makuu, madini na rasimali watu,mfano mzuri ni ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma.
Hasi
Huyu bwana kitu amabcho kinammaliza ni kuwapa watu kazi amabzo hawana uwezo wa kuzifanya,ama wana uwezo mdogo wa kufanya maamuzi na kusimamia vitengo/idara husika au wanaongozwa na tamaa za kujitajilisha wao na familia zao kwanza, wengi ni mafisadi wakubwa wasiokuwa na hata chembe ya huruma kwa kufuja rasilimali za taifa.
Hii imesababisha idara nyingi sana kufanya vibaya na lawama kwenda moja kwa moja kwa rais maana ndo aliyewateua.
Ushauri.
Rais kikwete anatakiwa kufanya yafuatayo ili akiondoka madarakani apatwe kukumbukwa na hata na vizazi vijavyo
Sekta ya madini.Tanzania mpaka kufikia mwaka jana tulikuwa na deposit ya dhahabu kiacha ~100Moz, hiki ni kiasi kikubwa sana kwa nchi kama Tanzania, kinachotakia ni usimamizi makini wa hii sekta ili tanzania ipate kunufaika na siyo vingivyo.
Hii ni moja kati ya sekta muhimu sana katika kutoa ajira kwa watanzania, lakini nenda huko, ni aibu tupu, unakuta expart mzungu hata jianlake kuandika ni shida
Sekta ya Utalii.Hii ni sekta muhimu sana ambayo ikutumia vizuri na kuondoa uozo/ufisadi uliyoko huko, unaweza kumsaidia sana kupata pesa za kufanyia mambo mengine ya muhimu kama kuwalipa watumish mishahara mizuri ili wawe ni wenye tija kwenye kazi zao.
Kilimo-Hii sekata ianachekesha sana, maana kumekuwa na kauli mbiu nying sana mara kilimo ni uti wa mgongo, mara mapinduzi ya kijani mara Kilimo kwanza, lakini ukichunguza kwa makini watendaji wake wengi hqawana dhamira ya dhati kukikomboa kilimo cha hapa Tz, sikiliza kuna watu wananyimwa ruzuku za pembejeo kisa ni wapizani, kwa mtaji huu hiki kilimo ktaendelea kuwa uti wa mbavu mpaka hapo baadaye, cha msingi hii wizara inatakiwa apewe mtu anayejali maslahi ya taifa mbele,mwenye vision and mission lazima awe ni mtu wa objectives.Tanzania ni kubwa sana na aslimia 80% ya watu wanategemea kilimo, atumie sera ya majimbo katika hili, hakika atafanikiwa sana.
Namalizia kwa kusema wasaidizi wa rais sasa ni wakati mwafaka wa kuona aibu na kuchapa kazi, wengi mtakumbukwa kwa matendo yenu na dhamira zenu za kulitumika hili taifa.