Hivi karibuni naongeza idadi ya single mothers mtaani

Hivi karibuni naongeza idadi ya single mothers mtaani

Deva

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
1,238
Reaction score
1,819
Wakuu salam

Ni hivi, huyu binti nimekuwa nae kwenye mahusiano nilipokuwa chuoni, yeye pia akiwa chuo, makubaliano yetu ilikuwa ni kuja kufanya maisha pamoja, nikimaanisha kuoana, hivyo basi nililenga angalau kuwepo na utangulizi wa mimba tu ndio mengine yaendelee, maana siko tayari kuishi na mtu ambaye sitaweza kutengeneza nae familia,kunipatia watoto, kwa maana madada wengi siku hizi wanachezea vizazi wanatoa mimba sana sipendi nimuoe halafu ndio nigundue kwamba hawezi nipatia watoto na nimeshamuoa.

Nikazungumza nae tukapanga kuwa mwezi wa tisa baada ya chuo utaratibu wa mimba ufanyike, baada ya hapo nimtambulishe nyumbani kama mchumba na taratibu nyingine ziendelee, ila katika kufanya mapenzi mimba ikashika mwezi wa 5 akaniomba tuitoe ili mwezi wa tisa ubaki palepale, nikakatalia kabisa, alilazimisha sana, ikabidi nimtafutie watu wa kumshauri asitoe, basi ikawa usumbufu hivyo tukitofautiana kidogo anasema tuachane, siku moja alipiga simu akakuta iko busy akasema ninamsaliti japo nilimueleza kuwa si kweli nilikuwa naongea na mzazi, hakutaka anisikilize alisema mahusiano yaishe nisimtafute wala kumsumbua na wala mimba nisiiulizie, na wala nisishiriki chochote ataamua atakalo.

Ilikuwa kipindi cha mitihani nikatuliza akili yangu nikafanya mitihani yangu muda kama wa wiki tatu, akanitangulia kumaliza mitihani, akaenda nyumbani kwao, hapo mimba ikiwa na miezi minne, akaenda nyumbani, nilipomaliza mtihani nikamtafuta akasema amepata mtu wa kuilea mimba hivyo nisimsumbue, mimi hawezi kunitambulisha kama baba wa mtoto maana hatuendani, akaniblock kote sms, calls,whatsapp nikawa simpati!

Baada ya week mbili kupita, nikaona kanitoa block kote akanisms anaumwa sana na maji yanamtoka ukeni hajui ni ya nini, basi ikabidi nimchukue tu nimpeleke hospital kwanza atibiwe na kucheck afya ya mtoto kwenye ultrasound, mtoto alikuwa salama yeye alikuwa anasumbuliwa na homa, alipopona akaniambia kuwa anaomba kuwa nimsaidie pesa ya mahitaji ale anachojisikia, maana vyakula havipandi vya nyumbani, anashinda njaa muda mrefu, nimnunulie na nguo pana za kulelea ujauzito, nikamuuliza lakini si ulisema una mtu anayekulea na ujauzito, yuko wapi hadi ukose vyote hivyo, akasema ilikuwa si kweli yale maneno, nikapotezea hilo jambo nikamtimizia alilohitaji.

Hapo mimba ina miezi mitano na nyumbani kwao hawafahamu...nikamwambia asijali nitafanya utaratibu kuongea na wazee ili tuje pale nyumbani nifahamike kwanza, ndio awaambie ana mimba yangu ili asigombezwe na kulaumiwa sana...akasema kama sitafanikiwa kwenda mimi kwao ili nyumbani aruhusiwe kuja kujifungulia nyumbani kwetu, ataondoka aende mbali, akajifungulie mbali mkoa mwingine ambapo rafiki yake amepanga getto huko, nikamwambia haitashindikana atakuja aje kujifungulia nyumbani, huko sitaki aende ni mbali ya uangalizi wangu kwa mtoto.

Nikawaambia wazazi kuwa nina mchumba nahitaji tuanze taratibu za kwenda kutoa kishika uchumba, ili aweze kuruhusiwa kutoka kule aje kujifungua huku, maana yeye alisema kujifungulia nyumbani ni aibu hawezi, wazazi wakakubali tukapanga tarehe (Mwisho wa Mwezi huu wa 10). Mimi na yeye mahusiano yakaendelea kama kawaida hivyo namjali nampa anachohitaji, clinic nampeleka, ikafikia mahali akasema anahitaji nimsaidie mtaji afanye biashara ndogo ndogo, nikampa, nikamnunulia simu mpya..yaani kwa kifupi nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kutimiza mahitaji yake.

Jumamosi iliyopita nilikuwa kwenye ibada mida ya jioni, akapiga simu sikupokea, nikamsms kwamba nipo kwenye ibada siwezi ongea, akatuma sms kwamba si kweli, nafanya drama, nilivyomaliza nikamcheck nikaongea nae ila hakuwa anajibu vzuri siku nzima ya jumapili haikuwa nzuri, Jumatatu ya juzi ilipaswa tuamkie kwenda clinic, akakataa kwenda, nilikasirika nikamwambia "Una Maamuzi Ya Kipumbavu" akajibu Kama unataka kwenda, Kusanya vichangudoa vyako uende navyo" basi akaanza kusema kuwa namdharau na kumtukana, simthamini na hiyo mimba anataka aitoe tu maana ananiona ni mtu nisiyemjali na kumuheshimu.

Kwahiyo tuachane na wala nisiulizie chochote kuhusu mimba maana ameshasema tuachane, na hata mtoto nisiulizie, kwetu pia hawezi kuja aje aishie kuwa housegirl,kama kulea anaweza kulea mwenyewe bila kunishirikisha mimi lolote, na hata nikitaka pesa zangu zote nilizompa arudishe yupo tayari, nikamwambia kaa nazo...kuhusu suala la mimba sijajua atafanya nini akiamue kuzaa na azae, akiamua kutoa na atoe, nimefika uwezo maximum wa kumhandle, potelea mbali, mimba ina miezi mitano sasa.

I do not care anymore.

Ndio nimeamua hivyo wakuu, au mnasemaje.
 
Pole sana Mkuu,

Kuhusu kutoa mimba nikosa la kisheria na wewe unauthibitisho wa clinic kua huyo mpenzi wako ni mjamzito,so ikifika muda dai mtoto wako,kama hana mtoto muulize mimba aliipeleka wapi? kama hana majibu mazuri sheria ifuate mkondo wake japo si amini kua mimba ataitoa,

Vijana someni mjiweke sawa kimaisha kwanza,mapenzi yapo tu siku zote.
 
Sawa mkuu
 
Pole sana mkuu Devion huyo mdada mpaka na mi kanichefua angekuwa karibu na makofi angekula(kama unayoyasema ni kweli lakini)

mwanzoni nilivyoona heading nilijaa sumu kukuelekea kuja kusoma nikanyweaaaa

pole sana mkuu achana naye endelea na Maisha yako,umemsihi sana kuhusu huyo mtoto ajaye ila anajifanya kichwa maji,let her be hata akiitoa haatia ni yake mwenyewe wewe umefanya part yako na naamini Mungu anathamini jitihada zako za kutoka kuuokoa uhai wa kiumbe kishicho na hatia

Tulia zako utampata tu ambaye mtaelewana na kuyajenga

One thing and my take tou you Usimwadhibu mwanamke mpya utakayepata kwa ajili ya ushenzi wa huyu wa sasa,maana watu waliotendwa hawachelewagi sitokaa nipende tena,hiyo sio fair aliyekukosea ni mwingine unapoenda kumtreat mwingine kutokana na hasira zako kwa liyepita sio saw hata kidogo,kila mmoja ana akili na utu wake,ukimpata mwingine mtreat kwa kadri unayoweza uyafurahie Maisha,usiache huyu kichwa maji wa sasa adetermine mahusiano yako yajayo

Asante
 
Hana tatizo mchukulie madhaifu yake zero IQ ashasema ukimchukulia sana serious mwanamke soon unakufa. Hayo ni mambo madogomadogo sana, mimi nikikuelezea ya kwangu je utahimili kweli mkuu
Daah yaani mkuu pamoja na kwamba siyafahamu yako ila huyu ni shida, kuna mambo nimepunguza...nitaslide pm yako mkuu
 
Pole sana mkuu Devion huyo mdada mpaka na mi kanichefua angekuwa karibu na makofi angekula(kama unayoyasema ni kweli lakini)

mwanzoni nilivyoona heading nilijaa sumu kukuelekea kuja kusoma nikanyweaaaa

pole sana mkuu achana naye endelea na Maisha yako,umemsihi sana kuhusu huyo mtoto ajaye ila anajifanya kichwa maji,let her be hata akiitoa haatia ni yake mwenyewe wewe umefanya part yako na naamini Mungu anathamini jitihada zako za kutoka kuuokoa uhai wa kiumbe kishicho na hatia

Tulia zako utampata tu ambaye mtaelewana na kuyajenga

One thing and my take tou you Usimwadhibu mwanamke mpya utakayepata kwa ajili ya ushenzi wa huyu wa sasa,maana watu waliotendwa hawachelewagi sitokaa nipende tena,hiyo sio fair aliyekukosea ni mwingine unapoenda kumtreat mwingine kutokana na hasira zako kwa liyepita sio saw hata kidogo,kila mmoja ana akili na utu wake,ukimpata mwingine mtreat kwa kadri unayoweza uyafurahie Maisha,usiache huyu kichwa maji wa sasa adetermine mahusiano yako yajayo

Asante
Yanayosemwa ni kweli asilimia zote na mengine nimepunguza kufupisha uzi, nwanamke ana kiburi imefikia mahali kwamba nimeona si mimba ni hulka yake
 
Mkuu ukisikia mwanamke kiroporopo ndio huyo anajifanya anaweza kuishi pekeake kumbe ukimuacha pekeake awezi kuishi hata theluthi yawewe unavyomuhudumia.

Ushauri: usimchukulie serious sana kama unampenda naunamalengo nae. In short ajiwezi kuhandle hiyo hali ila anajitutumua2
 
Anae ile inaitwa kichaa cha mimba kama sio hicho basi kitakuwa kichaa cha panya buku
 
Mkuu ukisikia mwanamke kiroporopo ndio huyo anajifanya anaweza kuishi pekeake kumbe ukimuacha pekeake awezi kuishi hata theluthi yawewe unavyomuhudumia.

Ushauri: usimchukulie serious sana kama unampenda naunamalengo nae. In short ajiwezi kuhandle hiyo hali ila anajitutumua2
Kweli mkuu anajitutumua tu
 
Subiri hadi ajifungue ndipo uwe na maamuzi maana wakati mwingine mimba sio poa inawasumbua sana wanawake na inaweza kukuharibia ya hela yote aisee
 
Mkuu, ktk kila kituko anachofanya mwanamke mjamzito chukulia kuwa anafanya kwa sababu ya 'ujauzito'.
Jishushe, mthamin, mpende, mpe faraja ili kumjengea confidence.. Mbna kabla ya ujauzto mlikuwa mnaelewana vzur, hujiuliz? Jifunze kuish na mjamzito, ushshndane naye.
Mmhh hivi kumbe wanaume wa aina hii bado mpo?? Basi maajabu!!
 
Back
Top Bottom