Hivi jamani siku ya kwanza ya wiki ni ipi haswa?

Hivi jamani siku ya kwanza ya wiki ni ipi haswa?

Ni siku ambayo Yesu alifufuka, maana tunaambiwa hivi katika Mathayo 28:1 Hata sabato ilipokwisha, ikapambazuka siku ya kwanza ya juma​, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
 
Jumapili ndiyo siku ya kwanza ya juma hilo liko wazi
 
Niko njia panda

Naamini unataka Siku ya kwanza ya juma kibiblia ? Kama ndivyo ,sikku ya kwanza ni siku inayofuatia siku ya sabato ya wayahudi, kwetu huku siku hiyo huitwa jumapili...kwa Wakristo hiyo ndiyo siku ya Yesu Kristo,siku aliyofufuka na kutangaza Agano jipya lililowajumuisha mataifa kuwa wana wa Mungu.
 
siku ya kwanza si jumamosi jamani, mbona inajieleza yenyewe na ya pili jumapili, ya tatu j3, inafata j4 na j 5, then alhamisi na siku ya saba ni ijumaa...

siku ya ijumaa ndio siku ya saba katika wiki na kwa hivo ukitaka kujua ukweli wa ipi dini sahihi angalia tu hata huu mtiririko wa siku unakueleza..ijumaa ndio siku ya saba na ndio ingepaswa kupumzika kama nchi nyingi zenye waislamu wengi zinavofanya..
haiitaji kamera kuuujua ukweli, ukweli ndio huo mwenye macho na aone..
 
Kwa Lugha yetu ya kiswahili siku ya kwanza ni Jumamosi na siku ya saba ni Ijumaa lakini kwa standadi za kimataifa (ISO 8601) inaeleza kwamba siku ya kwanza ni jumatatu na siku ya saba ni jumapili.
 
Jumapili ndiyo siku ya kwanza ya juma hilo liko wazi

kwa nini isiwe jumamosi manake hiyo jumapili ni siku ya pili katika wiki au unatumia zile hesabu zetu za kisabatoooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Majadiliano mengine mazuri sana, siku ya kwanza ni jumamaosi
 
Inategemea na nini;
1. Ki-shule shule ni Jumatatu

2. Ki-sabato ni Jumapili

3. Ki-kristo ni Jumapili

4. Kiislamu sijui aisee

5. Ki-kazi inategemea na utaratibu wa ofisi zenu mzunguko unaanza vipi na unaishaje
 
Ni siku ambayo Yesu alifufuka, maana tunaambiwa hivi katika Mathayo 28:1 Hata sabato ilipokwisha, ikapambazuka siku ya kwanza ya juma​, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.

Siku ya Sabato ni Jumanne kwa mujibu wa maandiko(Nitakuja kufafanua)Kumbuka majira na nyakati vilibadilishwa.Na matumizi ya kalenda ya sasa ya Gregory ndio ushahidi.Kwa Mungu mwezi una siku 30 tu na masaa yake huhesabika tofauti na jinsi ilivyo sasa ambapo siku huanza kuhesabika saa 7 usiku!Illuminat walifanikiwa kuufanya mwaka uwe na miezi 13 iliyojificha katika miezi 12 ya sasa!Kumbuka kuwa namba 13 ni masonic number.Baadhi ya madhehebu wanaipa heshima mf sabato ya 13,division 13,ahadi 13 za ubatizo nk.Kuna watu wanaamini siku ya saba ni jumamoasi ila wanaweza kushangaa wakijua si jumamosi bali ni jumanne!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kulingana na maelezo yako, bila shaka wewe ndiye hasa Illuminat, ni ukweli usiopingika kuwa wayahudi wana dini yao iitwayo Judaism ambayo wanaabudu siku ya jumamosi na wamekuwa wakifanya hivyo tokea zamani, je nao walipotoshwa huku wakiendelea kushika sabato?
 
Back
Top Bottom