Hivi Jamani hii sawa au udhalilishaji wa taaluma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Jamani hii sawa au udhalilishaji wa taaluma?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Jul 13, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Natumai wakuu mpo salama,

  Kuna jambo limeanza kujitokeza nadhani linaweza kutishia mtaala wa elimu kwani limekuwa linakuwa kwakasi kubwa sana. Hili si jengine bali ni suala la tofauti baina ya Honorary Doctorate na PhD. Hebu tazameni taarifa hizi.

  MH.MZINDAKAYA ATUNUKIWA PHD…!!!Posted by Blog Team on July 12th, 2010

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samwel Sitta akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kwela Christant Mzindakaya jana mjini Dodoma mara baada ya kutununikiwa Shahada ya Uzamifu ya Heshima katika Filosofia ya Uongozi wa Biashara( Honorary Doctorate Degree of Philosophy in Business Administration) na Chuo Kikuu cha California State Christian cha nchini Marekani. Sherehe fupi za kumpongeza zilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini dodoma.

  Mbunge Mbunge wa Jimbo la Kwela Christant Mzindakaya akiwashukuru wabunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania jana mjini Dodoma mara baada ya kutununikiwa Shahada ya Uzamifu ya Heshima katika Filosofia ya Uongozi wa Biashara( Honorary Doctorate Degree of Philosophy in Business Administration) na Chuo Kikuu cha California State Christian cha nchini Marekani. Sherehe fupi za kumpongeza zilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini dodoma. Picha na tiganya vincent-Dodoma.

  Source: Mohammed Dewji

  Nyengine hii


  Dk Getrude Rwakatale atunukiwa tuzo na chuo kikuu cha marekani
  Monday, July 12, 2010

  Dk.Mchungaji Kiongozi wa kanisa la TAG Mikocheni B(Mlima wa Moto)Mh. Gertrude Rwakatare akionyesha Tuzo mbili ya Global Leadership Award na Tuzo ya Doctorate ya Divinity(Maswala ya Kiroho) alizotunukiwa na chuo Kikuu kilichopo Marekani kijulikanacho kama United Graduate College and Seminary University katika sherehe zilizofanyika Kanisani kwake jijini Dar es Salaam.

  Source: Michuzi.

  Hii sijui ni PhD au Honorary Doctorate? Na mama Rwakatare si alikuwa na PhD before au nimesahau jamani.

  Pia kuna hii:

  Hongera Mhe. John P. Magufuli kwa kupata PhD 11/28/2009
  1 Comment(s)

  Dr. Magufuli
  Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Dr. John Pombe Magufuri, akipongezana na Dr. John Stanslaus Nduguru ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Ufundi katika Wizara ya Miundombinu, wakipongezana baada ya kuhitimu kozi ya PhD katika mahafali yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Magufuli tunajua amesomea UD PhD na amefanikiwa kuipata.

  Wasiwasi kuongezeka huku kwa Honorary Doctorate kunaweza kuhatarisha taaluma za vyuo vikuu kwani tunashindwa kutafautisha Honorary Doctorate na Doctor of Philosophy. Au pengine sijui labda ziko sawa ndio maaana tuna Dr Kikwete, Dr Karume, Dr Salim, Dr. Shein, Dr. Mzindakaya, Dr Dr Dr Dr..... Je tutafika?
   
 2. J

  Jack Beur JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Ulimbukeni tu mkuu
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Honorary PhD inapotolewa kuna maneno yanasemwa kwamba inatolewa kwa achievements za mtu, na iko sawa sawa na PhD ya kawaida in all other aspects (kwamba mtu anastahili kuitwa Dr and all)

  Ujue hivi vitu ni sisi tu nchi maskini ndio tunaona vitu vya ajabu, nchi za wenzetu ukienda kupata PhD ya ungwini leo, na kitoto kitakacho drop out of college kikaenda kutengeneza an internet empire hiki kitoto kilicho creative kinaweza kuonekana cha maaana zaidi. Hivi Marekani kuna PhD wangapi, halafu kuna Mark Zuckerberg wangapi ? Na kati ya hao PhDs wangapi wame influence Marekani (au hata dunia) kama Mark Zuckerberg ? Vipi that Harvard dropout Bill Gates ? Hivi Mark Shuttleworth ana PhD ya nini?

  Ni vile tu sisi hata mwanafunzi wa chuo kikuu tunamuita "msomi". Wenzetu washaacha mambo ya kuitana "Dr" nje ya academic settings, unless you are a medical doctor, ku flaunt PhDs in the name of "Dr" nje ya University na mikutano academic ni ushamba.

  Waacheni watindiga walimbuke na wao, sasa hivi wajanja wanatafuta vitu vikubwa zaidi ya mikaratasi ya PhD.

  We kama msomi wa kweli na unataka kuji distingusish kutoka hawa jokers gundua kitu, lete constructs mpya za Artificial Intelligence, gundua patterns mpya katika uchumi etc.

  Ama sivyo wewe na Mzindakaya mnaweza kuwa wote paperchasers tu, hamchekani, na unamuonea Mzindakaya kwa sababu kapata shortcut na wewe umekaa/ unatakiwa kukaa darasani miaka 10.
   
 4. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Na mwaka huu wa uchaguzi kila mtu anataka kuitwa Dr. Kweli wacha walimbukeni walimbuke! Mtu hata haoni aibu kuitwa Dr, wakati huna fani uliyobobea zaidi tu ya kuwa mbea!
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  hahaha ni kweli but achievement ipi Honorary doctor amefanya katika ulimwengu wa literature? na je tuwaajiri wote university
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Umezungumzia akina Mark (mzee wa facebook), Bill Gates (Microsoft) na wengineo but ukasahau kuna Stiglitz, Nash na wengineo ambao mchango wao ndio unaotufanya tunaishi na kula na kuajiriwa katika dunia hii. Au hiyo sio michango? Na je nikuulize ni wangapi wamekuwa kama akina Gates? au Mark?,. unataka kutwambia mtu akishakuwa na Honorary Doctorate kisha tumpe Honorary Professor?
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Literature ina achievement mazee? Utaandika kipi ambacho wagiriki hawajaandika? Hata hiyo sayansi mengi yanayogunduliwa leo tayari ukiangalia kina Edgar Allan Poe, kwenye ma Bhagavad Gita and some other ancient texts vishaandikwa.Huyo Mpemba wetu kaja "kugundua" Mpemba effect kumbe kina Aristotle walishaiona huko zamani kwenye antiquity.

  University yoyote yenye maana itaangalia track record.The only way Mzindakaya anaweza kufundisha University ni kuonyesha tricks zake za Ufipa za kutundika koti hewani, labda anaweza kupewa department ya uchawi, other than that hakuna kitu.

  Hawa Wamarekani wengine vyuo kwao ni biashara, wanatoa degree hata kwa mbwa (Chuo cha Almeida alichochukulia MBA Mustapha Mkulo) na usikute wanalipwa na hawa jokers kutoa hizo honorary PhDs.

  Watu wanao matter hizi PhD haziwatishi, watu zinaowatisha hawawezi ku matter.

  Msikilize Dr. Mahiga kwa mfano alivyokuwa anahojiwa na BBC katika suala la serikali ya Tanzania kuhusika na biashara ya silaha with rebels in the Great Lakes region, halafu msikilize "Dr" Mzindakaya, wala huhitaji chuo kukueleza nani ni real PhD na nani kanunua.
   
 8. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ajikwezae hushushwa, real PhD holders achaneni na hawa wajikwezao kwa Doctorate degree za kupewa ipo siku historia itawashusha tu! kwani zamani si University graduate pekee ndio walikuwa wakivaa graduation gown! na watu wali hustle kikweli ili tu wapate ile fahali ya kuvaa lile gauni, lakini siku hizi hadi kindergaten graduate wanavaa hayo majoho, lakini huwezi sema eti kwa vile wao wanavaa joho na uni graduate anavaa joho basi wako sawa nooo!
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Good point Kiranga but ujue hakuna hata literature moja imeisha mpaka leo? Kusema kwamba hakuna kitu cha kugundua sio kweli otherwise basi tusingelikua na akina Newton au wasingelijua dunia ni duara kwani before them kila mtu alifahamu dunia iko flat na pembe nne. Hivyo kila literature haijakamilika kwani ulimwengu uko so complex to fully explain everything. Kuanzia tabia mpaka mazingira tunajaribu kumbanua baadhi ya mambo but mengine tunayaacha kwa wengine kuyaendeleza. Hivyo ndio maana wanaosoma PhD wanayatafuta hayo mambo yaliyobakia na kuyaendeleza. Sasa Honorary Doctorate wanatafuta nini cha kuendeleza? Siasa?
   
 10. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu msipoteze mda na hicho kizee, kwa taarifa yenu hiyo ni Honorary Ph.D ya pili anapata ndani ya miaka mitano!!!. (kumbuka huyu ni mtu ambaye alishindwa kumaliza hata middle school!). Hivi anaweza kutueleza amefanya kitu gani cha kujivunia ktk biashara? kumbuka miradi yake yote ni ya kibabaishaji ameshakopa mabilioni kifisadi na haielekei kama ataweza kuzilipa!.

  Yah, kama alivyo sema mkuu mmoja labda alitunikiwa hiyo Ph.D baada ya kutundika koti hewani!. All-in-all hii trend ikiendelea kwa kasi hii basi huko mbeleni hata watoto wa mafisadi nao wataanza kununua Ph.Ds na wale wanaosoma kwa bidii watakuwa discouraged na mwishowe kwa ujumla haka ka'nchi katajikuta pahala pabaya sana kielimu.
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  This is my point!!!!. Juzi nilisoma makala moja the Guardian I was shock to find out that 60% of university of dar-es-salaam lectures are supposed to be retired. Sasa wakiondoka hao wataajiri kina nani? Au ndio tutaajira wakenya
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jul 13, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Normally digrii za heshima hutolewa siku ya commencement ceremony. Kwa vile digrri zote hutolewa kutokana na recommendation za maprofesa ( na wahadhiri), ni kawaida mpokeaji ma atoe mhadhara au mafanikio yake yasomwe mbele ya kadamnasi ya maprofesa wa chuo husika pamoja na wahitimu wengine kabla digrii hiyo haijatolewa; nashangaa kuwa hawa wa kwetu zinawafuata majumbani kwao tena hakuna profesa mwingine wa chuo anayeshuhudia ikitolewa. Digrii za heshima huwa hazitolewi katika mikondo ya kitaaluma. Hivyo, kwa vile Ph.D ni degree ya kitaaluma, huwa haitolewi kama honoris causa, badala yake doctorate ya heshima hutolwea kwa jina tofauti. Kwa mfano badala ya Ph.D in Law, basi ile ya heshima itaitwa Doctor of Laws (siyo Law), Badala ya Ph.D in Science, ile ya heshima itaitwa Doctor of Science, kuna nyingine nyingi kama Doctor of Humane Letters, Doctor of Letters, Doctor of Divinity, na kadhalika

  Ingawa digrii hii ya heshima hutolewa with all the rights and privileges pertaining thereto, siyo kawaida ya wapokeaji wa digrii hizo kujitambulisha kama madaktari ingawa wanaruhiswa kabisa kujiita hivyo kutokana na rights and priveleges za degree zao.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Good point Kichuguu, but labda niulize inakuwa vp Honorary Doctorate ikawekwa sawa PhD Degree? Maana katizame katika web ya Mohammed Dewji ameandika ni PhD but ukitazama ni honorari. Sasa which is which?

  Yes Doctorate of Philosophy inatolewa na approval of the professa so as the Honorary but are they equivalent if not why is TCU allow this to happen in Tanzania? What is so special with Dr title?
   
 14. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  hata mimi hii honorary PhD ya huyu bwana inanishangaza!!! kafanya biashara gani ya maana au uongozi gani wa biashara? basi ielezwe ili watu waone achievements na si blabla tu.

  hivi TCU wanasemaje kuhusu hili au mpaka mtu alalamike/lifikishwe kwao hahahahahahhaha

  ni kama wale jamaa wa kudhibiti chakula na madawa wanazuia kitu kikishaleta athari kwa watumiaji.
   
 15. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Na tatizo linakuja pale shahada hizo zinapotumika kupimia watu kwa ajili ya ajira au kuonyesha ubora wa mtu kitaaluma katika sekta ya umma. Unakuta mtu mwenye honorary au sub-standard PhD anajiona yuko sawa kitaaluma na waliozisomea katika mifumo inayoeleweka au yuko juu ya mwenye Masters. Angalau basi ingekuwa honorary PhD kama ya Nyerere ambaye amekuwa na mchango (intellectual contribution) mkubwa katika uchambuzi na utekelezaji wa dhana mbalimbali za kiitikadi.
   
Loading...