Hivi ipo siku Tanzania tutatembea Usiku wa manane bila shida?

Royal Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2016
Posts
1,467
Reaction score
2,760
Habari wakuu hivi ipo siku Tanzania na viunga vyake tutatembea usiku wa manane iwe kwa shida au raha bila kukutana na vibaka/tatu mzuka?
 
Ushasema usiku wa manane sio usiku wako kuwa mpole tu.
 
Habari wakuu hivi ipo siku Tanzania na viunga vyake tutatembea usiku wa manane iwe kwa shida au raha bila kukutana na vibaka/tatu mzuka
Uko mitaa gani na unajishughulisha na nini? Tujue ili usitupotezee muda.
 
Zamani tulikuwa tunaogopa kutembea usiku tukihofia wanyama kama simba, chui, fisi na tembo lakini siku hizi tunaogopa watu kutembea usiku
 
Juzi kati nilikuwa natembea usiku nikakutana na fisi wala hawakunifanya kitu, ningekutana na watu hakuna rangi ningeacha kuona. Hatutembei usiku siku hizi tunaogopa kukutana na watu
 
Habari wakuu hivi ipo siku Tanzania na viunga vyake tutatembea usiku wa manane iwe kwa shida au raha bila kukutana na vibaka/tatu mzuka?
Bongo kupo salama sana
Sehemu kama jozi, jobergy, Johannesburg kuanzia saa tano usiku makundi ya vibaka ni mengi kuliko raia wema
ukitembea umbali kama kutoka kkoo shimoni mpaka jangwani hakuna namna unaweza kutoboa ukiwa na simu yako pesa raba kali airpods na vitu vyovyote vyenye thamani pia kujeruhiwa au kufa kabisa
 
Bongo ipi ipo salama wakati tunasikia watu wanatekwa kila kukicha hiyo Unga limited ya Chuga unaijua mazee hapo Jozi unapopazungumzia ni wapi mbona Edenville na viunga vyake tunasota muda wowote tu hata Bedford view na Centurion watu wanasota tu muda wowote.
Johannesburg kiwango cha crime kipo juu sana ila vijana wengi wanakaa huko huko kwa wanakokaba unategemea nini..
 
Sidhani kama mtoa mada ameongelea kisiasa
Nadhani ameongelea vibaka na si watekaji
 
Habari wakuu hivi ipo siku Tanzania na viunga vyake tutatembea usiku wa manane iwe kwa shida au raha bila kukutana na vibaka/tatu mzuka?
Mbona watu tunatembea bila shida yoyote, au unazungumzia tanzania ipi?
 
Sidhani kama mtoa mada ameongelea kisiasa
Nadhani ameongelea vibaka na si watekaji
Miaka mitatu nyuma vibaka wengi walikua wanavamia nyumba na kuiba TV maeneo ya Iwambi huku wenyeji wakijua kuwa wanaibiwa pana siku shangazi yangu aliibiwa TV mbili ndani ya mwezi mmoja aliponiambia nikaenda kufunga 55" nilipotoka SA harafu tukaweka mtego wa kulala kwenye majani haikuchukua hata wiki moja wale wahuni walirudi kutaka kuchukua ile TV maana hata milango haikufungwa sana ili wasisumbuke kuvunja walipoingia ndani tu tukaibuka wote na tupo na mizigo walikua vibaka 15 tulichowafanya pale kama walikuja kutembea itakua ni bahati yao mpaka kesho wanalala salama salmini na hii ni Iwambi ya Mbeya ukitaka nikupe matukio ya Arusha yapo mengi tu mkuu..
 
Mbona tunatembea usiku kucha bila shida.
Uko wapi huko?
Mitaa kama Sinza,Unga ltd sehemu nyingi usalama. Ni mgogo

Nadhani Mkuu Arusha unaisikia tuu kwenye Bomba huku kuna matukio mpaka mengine yanatisha
 
Makazi ya kudumu yapo Arusha naisikiaje kwenye bomba mkuu.
 
Back
Top Bottom